Nyerere alipokuwa anatarajiwa kutoa hotuba, nchi nzima ilikuwa inasubiri kwa hamu. Baada ya Nyerere, leo hii ni Tundu Lissu tu

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Huu ndio ukweli kwa sasa na wala haupingiki:

Nyerere alipokuwa anatarajia kuhutubia, karibu kila mtu anasogea kwenye chombo cha habari iwe ni TV au Redio au kufika kwenye ukumbi husika huku akiwa na shauku ya kutaka kusikia atachosema.

Mbali na wanachi, hata vyombo vya habari vya ndani na vya kimataifa hujiandaa kuipokea hotuba yake na waandishi wanaoshiriki ni wale wahariri maarufu na wenye kuheshimika ndani na nje ya nchi.

Hii ni kwsababu, Nyerere alipokuwa anaongea, alikuwa anaongea kama Raisi Mstaafu na sio kama kiongozi mstaafu wa CCM. Kila mtu alitarajia kusikia speech nzito ikilenga mustakabali wa Taifa na watu wake ikiwemo kukemea hata walio madarakani tena bila woga wala hofu pamoja na kukemea mataifa makubwa yanapoikosea nchi yetu, n.k.

Sasal leo hii, Mama akitangaza kuongea na media, unaanza kujiuiliza sijui leo hotuba yake itaniacha na hasira au machungu gani moyoni.

Leo hii ukisikia Nchimbi anaongea, unajiandaa kisaikolojia kusikia propaganda na mambo mengine ya aina hiyo.

Leo ukisikia JK anataka kuongea na media, hutarajii ataongea kama Raisi Mstaafu kusaidia nchi na watu wake, badala yake utatarajia kusikia hotuba na maneno ya kisiasa kusaidia chama chake na watu wake wa karibu au utajiuliza labda kuna nini huko kimetokea kinachotishia hatima ya CCM na sio nchi.

Hao ni kwa uchache.Lakini leo ukisikika Lissu anaitisha mkutano wa waandishi wa habari, unajiaanda kusikia hoja za kizalendo zinazolenga kutetea nchi na watu wake, kulinda maliasili za nchi, haki za watu masikini, utawala wa sheria, demokrasia, kulipua madudu ya watawala na hata kuwakemea, n,k kama ilivyokuwa kwa Hayati Mwalimu Nyerere.

Mwalimu Nyerere japo alikjuwa na mapungufu yake, ila ameacha gap kubwa sana nchi hii na Tundu Lissu ndio mtu pekee anaejaribu kuliziba pengo hilo.

Huu ndio ukweli, hutaki unaacha.
 
Sio tu kwa hotuba, kiongozi pekee atakayeleta mageuzi ni Tundu Lissu baada ya Nyerere

Hao wengine ni magnge ya ulaji tu
 
Tuache utani, hotuba za Mbowe Huwa ni hatari sana.
 
Lissu anaonekana anapenda mambo ya kupigana pigana hata ikibidi kutoana ngeo au kuchomana visu
 
2025 anafaa vema kuwa rais Tanzania, ni mzalendo, anaipenda nchi yake
 
Bila Mwamba DJ Mbowe leo hii lissu angekuwa shimo la Tewa !!
 
Eeeh team Chadrama

Unajua Jibu ni Hayati Magufuli ndie kinara wa hilo Nchini

Lissu walaaaaaaa

Hata humu inaonyesha.. Anaongelewa kwenye kupitia wengine kizaidi sio yeye pekeee
 
Ni Yeye, Tundu A. M. Lissu 2025..
Ngoja nitoe shingo nje: hii kazi inaweza kuja kuwa rahisi kuliko ilivyo tarajiwa hapo mwanzo. Nalisema hili mwanzo, na naomba Mwenyezi Mungu alibariki liwe hivyo; maisha na uhai wa waTanzania visiwe majaribuni.
 
Lissu anaonekana anapenda mambo ya kupigana pigana hata ikibidi kutoana ngeo au kuchomana visu
Usione aibu, taratibu anza kidogo kidogo kubadili lugha. Hadi kufikia Oktoba 2025 lugha hiyo itakuwa ime nyooka kabisa. Hakuna atakye kumbuka ulivyo wahi kuwa shetani, ukiimba ushetani tu masaa 24/7!
 
Hapana sio Lissu hajawahi kuwa rais na sio rais wa nchi.


Baada ya JK Nyerere ilikuwa ni JPM the rest were just business endorsement
 
Eeeh team Chadrama

Unajua Jibu ni Hayati Magufuli ndie kinara wa hilo Nchini

Lissu walaaaaaaa

Hata humu inaonyesha.. Anaongelewa kwenye kupitia wengine kizaidi sio yeye pekeee
Mkuu vipi sikuoni ukimuunga mikono Mama kama kipindi kile Cha mwendazake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…