Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Huu ndio ukweli kwa sasa na wala haupingiki:
Nyerere alipokuwa anatarajia kuhutubia, karibu kila mtu anasogea kwenye chombo cha habari iwe ni TV au Redio au kufika kwenye ukumbi husika huku akiwa na shauku ya kutaka kusikia atachosema.
Mbali na wanachi, hata vyombo vya habari vya ndani na vya kimataifa hujiandaa kuipokea hotuba yake na waandishi wanaoshiriki ni wale wahariri maarufu na wenye kuheshimika ndani na nje ya nchi.
Hii ni kwsababu, Nyerere alipokuwa anaongea, alikuwa anaongea kama Raisi Mstaafu na sio kama kiongozi mstaafu wa CCM. Kila mtu alitarajia kusikia speech nzito ikilenga mustakabali wa Taifa na watu wake ikiwemo kukemea hata walio madarakani tena bila woga wala hofu pamoja na kukemea mataifa makubwa yanapoikosea nchi yetu, n.k.
Sasal leo hii, Mama akitangaza kuongea na media, unaanza kujiuiliza sijui leo hotuba yake itaniacha na hasira au machungu gani moyoni.
Leo hii ukisikia Nchimbi anaongea, unajiandaa kisaikolojia kusikia propaganda na mambo mengine ya aina hiyo.
Leo ukisikia JK anataka kuongea na media, hutarajii ataongea kama Raisi Mstaafu kusaidia nchi na watu wake, badala yake utatarajia kusikia hotuba na maneno ya kisiasa kusaidia chama chake na watu wake wa karibu au utajiuliza labda kuna nini huko kimetokea kinachotishia hatima ya CCM na sio nchi.
Hao ni kwa uchache.Lakini leo ukisikika Lissu anaitisha mkutano wa waandishi wa habari, unajiaanda kusikia hoja za kizalendo zinazolenga kutetea nchi na watu wake, kulinda maliasili za nchi, haki za watu masikini, utawala wa sheria, demokrasia, kulipua madudu ya watawala na hata kuwakemea, n,k kama ilivyokuwa kwa Hayati Mwalimu Nyerere.
Mwalimu Nyerere japo alikjuwa na mapungufu yake, ila ameacha gap kubwa sana nchi hii na Tundu Lissu ndio mtu pekee anaejaribu kuliziba pengo hilo.
Huu ndio ukweli, hutaki unaacha.