Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na Samia, yupi Rais bora kwako?

Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na Samia, yupi Rais bora kwako?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Kwa vyovyote vile hakuna duniani mtu mwenye uwezo wa kurekebisha Historia. Kwa ivo hawa ndiyo walikuwa marais wetu na Samia ndiye Rais wa Tanzania kwa sasa.

Kwa mtazamo wako hawa ukiwaweka kwenye mizani yupi amekuwa Rais bora kwako na kwa nini ukiangalia changamoto alizokabiliana nazo na jinsi alivyozitatua na unadhani kwamba amecha alama (Legacy) gani kwa watanzania wote.
 
Nyerere.
Huyu aliongoza ujenzi wa Taifa pamoja na waliokuwa nyuma yake.
Aliiacha Tanzania kama Tanzania. Na alitaka kila Mwananchi ajivunie popote Duniani Utanzania wake.
Huyu ndie aliyeongoza kusuka misingi mikubwa ya nchi hii.
Jambo moja kubwa ni kwamba hakuwa na Tamaa binafsi. Aliiona nchi kwanza, maslahi binafsi pembeni.
Alifanikiwa kuacha Taifa la Tanzania ambalo hata majirani hawajui mbinu gani alitumia kuunganisha watu wa kabila na aina tofauti zaidi ya 200.
Alikiri makosa mbele ya safari pale alipoteleza.
Kuhusu vitu vinavyoonekana. Unaweza kutaja hadi ukachoka.
 
Wengi wanaona Nyerere alikuwa ni "the best of the best" ila wewe unaona Mkapa ni bora kuliko yeye, KWA NINI?
Mkapa alitengeneza mfumo ambao unaendesha nchi mpaka sasa. Taasisi nyingi za serikali zilianza kipindi chake. Huo ni msingi wa utawala bora.

Mwalimu atakumbukwa kwa kuweka umoja na mshikamano wa kitaifa lakini alikuwa na mapungufu mengi sana kiuongozi na maono.
 
Kwa vyovyote vile hakuna duniani mtu mwenye uwezo wa kurekebisha Historia. Kwa ivo hawa ndiyo walikuwa marais wetu na Samia ndiye Rais wa Tanzania kwa sasa.

Kwa mtazamo wako hawa ukiwaweka kwenye mizani yupi amekuwa Rais bora kwako na kwa nini ukiangalia changamoto alizokabiliana nazo na jinsi alivyozitatua na unadhani kwamba amecha alama (Legacy) gani kwa watanzania wote.
Kwangu Nyerere ni bora kwenye Kujenga Utaifa na Tunu za Utaifa .

Mkapa ni bora kwenye kuleta mageuzi ya Uchumi na Uongozi.

JK ni bora kwenye kukuza private sector, Welfare economics na demokrasia..

Samia nae ni bora kwenye mambo ya Welfare economics na biashara ila akipata second term huenda akawa namba 2 baada ya Nyerere.

Mwendazake ni zero brain kuliko wote.👇
 
Attachments

  • Screenshot_20220329-160315.png
    Screenshot_20220329-160315.png
    205 KB · Views: 3
  • Screenshot_20220730-173546.png
    Screenshot_20220730-173546.png
    137.2 KB · Views: 3
  • Screenshot_20220702-104156.png
    Screenshot_20220702-104156.png
    145.1 KB · Views: 3
Ingependeza kama ungetuuliza ni nani Rais Bora aliyefuata baada Mwalimu Nyerere kuachia madaraka 1985 na si vinginevyo.
Kila mtu ana mtizamo wake. Ukisema "Aliyefuata baada ya Mwalimu Nyerere..." ni kama vile unazuia watu kuwa na mawazo yao binafsi.

Kuna watu humu hawajui chochote kuhusu Mwalimu.
 
Back
Top Bottom