Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na Samia, yupi Rais bora kwako?

Kwa nini Nyerere na alifanya nini kikubwa mpaka unaona ni Rais bora kwako?
Nyerere alifanyakazi nzuri Sana ya lugha. Alivalisha watanzania utanzania japo mababu zetu waliendelea kufa masikini. Angembembeleza mkoloni asiondoke kabisa ili vijana kipindi kile wasome na madarasa yajengwe. Angewaacha wandelee kuendesha sehemu za ujenzi na viwanda ili kuproduce mashina katika nchi yake.

Amelinda Mali Leo hii watanzania wauza mpaka viwanda. Hapa titaona pamoja na kusaidia Taifa kwa lugha alizalisha wezi, matapeli, wavivu wa kufikiria wanafiki, waongo, wapenda sifa, waongeaji kupitiliza kuliko matendo.

Angepata wachapazi wasaidizi wakadili na Elimu ungekuta tukombali Sana.
 
Kwa vyovyote vile hakuna duniani mtu mwenye uwezo wa kurekebisha Historia. Kwa ivo hawa ndiyo walikuwa marais wetu na Samia ndiye Rais wa Tanzania kwa sasa.

Kwa mtazamo wako hawa ukiwaweka kwenye mizani yupi amekuwa Rais bora kwako na kwa nini ukiangalia changamoto alizokabiliana nazo na jinsi alivyozitatua na unadhani kwamba amecha alama (Legacy) gani kwa watanzania wote.
Wote hao wako sawa kwani wamejaza familia zao kwenye CCM na serikali.
 
Kila mtu ana mtizamo wake. Ukisema "Aliyefuata baada ya Mwalimu Nyerere..." ni kama vile unazuia watu kuwa na mawazo yao binafsi.

Kuna watu humu hawajui chochote kuhusu Mwalimu.

Hiyo sio sahihi huwezi kumlinganisha Nyerere na Marais waliofuata maana wote wamesimama kwnye misingi yake. Halafu Rais wa Mwaka 1961 huwezi kumlinganisha na Rais wa 2020.
 
Rais Bora ni Nyrerere.

1. Kaunganisha wananchi hakuna ukabila.

2. Kapeleka makao makuug Dodoma.
3. Kajenga viwanda.
4. Mfumo wa vyama vingi kautetea yeye.
5. Muungano
6. Kasaidia nchi za kusini mwa Africa kupata Uhuru.

Nk
 
Kwa vyovyote vile hakuna duniani mtu mwenye uwezo wa kurekebisha Historia. Kwa ivo hawa ndiyo walikuwa marais wetu na Samia ndiye Rais wa Tanzania kwa sasa.

Kwa mtazamo wako hawa ukiwaweka kwenye mizani yupi amekuwa Rais bora kwako na kwa nini ukiangalia changamoto alizokabiliana nazo na jinsi alivyozitatua na unadhani kwamba amecha alama (Legacy) gani kwa watanzania wote.

hakuna Rais atakaekuja au waliostaafu au aliyopo atakaemzidi JOHN POMBE MAKUFULI huyu alikuwa ni rais bora kuliko marais woote tanzania na africa. nyerere hana sifa kubwa ila ana bahati ya kusifiwa. mpaka leo watu wanahamu kama mungu angeweza kumfufua tena aje awe rais lakini ndio haiwezekani
 
Acha kumlinganisha Nyerere na vitu vya ajabu. Magufuli amefanya kipi Cha maana?. Rais wa 1961 unataka umlinganishe na Rais wa 2015? Wewe unaona ni sahihi.
 
Kwangu Nyerere ni bora kwenye Kujenga Utaifa na Tunu za Utaifa .

Mkapa ni bora kwenye kuleta mageuzi ya Uchumi na Uongozi.

JK ni bora kwenye kukuza private sector, Welfare economics na demokrasia..

Samia nae ni bora kwenye mambo ya Welfare economics na biashara ila akipata second term huenda akawa namba 2 baada ya Nyerere.

Mwendazake ni zero brain kuliko wote.

pole sana ulikuwa unamirija yako serikalini ikabanwa
 
Kwa vyovyote vile hakuna duniani mtu mwenye uwezo wa kurekebisha Historia. Kwa ivo hawa ndiyo walikuwa marais wetu na Samia ndiye Rais wa Tanzania kwa sasa.

Kwa mtazamo wako hawa ukiwaweka kwenye mizani yupi amekuwa Rais bora kwako na kwa nini ukiangalia changamoto alizokabiliana nazo na jinsi alivyozitatua na unadhani kwamba amecha alama (Legacy) gani kwa watanzania wote.

Tupunguze unafiki:

Kumlinganisha Nyerere na Marais wengine ni unafiki wa Hali ya juu. Nyerere wa 1961 unamlinganisha na Rais wa 2020?. Hili roho ya ushindani sijui imetokea wapi.
 
Kwa vyovyote vile hakuna duniani mtu mwenye uwezo wa kurekebisha Historia. Kwa ivo hawa ndiyo walikuwa marais wetu na Samia ndiye Rais wa Tanzania kwa sasa.

Kwa mtazamo wako hawa ukiwaweka kwenye mizani yupi amekuwa Rais bora kwako na kwa nini ukiangalia changamoto alizokabiliana nazo na jinsi alivyozitatua na unadhani kwamba amecha alama (Legacy) gani kwa watanzania wote.
Magufuli [emoji95]
 
Back
Top Bottom