Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na Samia, yupi Rais bora kwako?

Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na Samia, yupi Rais bora kwako?

JF inatakiwa iwe hivi kwa Watu wenye hekima kama wewe, sasa nashangaa kuna Mawatu yanaongozwa na hisia hadi kuandika takataka humu JF kuhusu Marais wetu wa nchi na bado moderators wanawachekea tu.
Hii extremism imekuwa inspired na viongozi wa kisiasa, kiongozi wa kisiasa anapotakamka waziwazi kuwa wanaompinga hawatakiwi kuishi, lazima awagawe sana watu
Nashukuru sasa hivi angalau nchi inarudi kwenye mstari
 
1. Nyerere.
Aliunganisha Taifa na kuweka misingi ya utawala.

2. Mkapa
Alifufua uchumi wa Taifa
 
Nyerere.
Huyu aliongoza ujenzi wa Taifa pamoja na waliokuwa nyuma yake.
Aliiacha Tanzania kama Tanzania. Na alitaka kila Mwananchi ajivunie popote Duniani Utanzania wake.
Huyu ndie aliyeongoza kusuka misingi mikubwa ya nchi hii.
Jambo moja kubwa ni kwamba hakuwa na Tamaa binafsi. Aliiona nchi kwanza, maslahi binafsi pembeni.
Alifanikiwa kuacha Taifa la Tanzania ambalo hata majirani hawajui mbinu gani alitumia kuunganisha watu wa kabila na aina tofauti zaidi ya 200.
Alikiri makosa mbele ya safari pale alipoteleza.
Kuhusu vitu vinavyoonekana. Unaweza kutaja hadi ukachoka.
Kwanza si vema kumlinganisha Nyerere na maraisi wengine, Nyerere ni Baba wa taifa, Mpigania Uhuru. Mwondoe kwenye huu mlinganisho tafadhali. Hakuna wa kulinganishwa nae. Mlinganishe na akina Nelson Mandela ndo Size yake.
 
wakati wa nyerere mkuu wa majeshi alikuwa kutoka kwao mara, waziri mkuu alikuwa kutoka mara mzee wakatiba mpya, kulikuwa na mawaziri kibao kutoka mara, kupeleka makao makuu dodoma hakuweza alishindwa ila alianzisha akaona shida mwamba jpm akatumia akili na maarifa kuipeleka dodoma iwe makao makuu, nyerere viwanda alivikuta enzi za mkoloni akavisimamia, muungano alikuwa na maslahi yake
Mkuu unamkumbuka Waziri Mkuu wa kwanza wa Rais A.H. Mwinyi?
 
Magu kiboko,aliagiza nchi nzima wafanyakazi wapeleke TIN number zao na wakafanya hivyo.sasa sijui akili yake alitaka azitumie vipi maana toka alale sijaona matumizi yake.
Ila kwangu mimi nilikuwa naona angewatoa wafanyakazi hewa kwenye kampuni binafsi.
 
Mkapa alitengeneza mfumo ambao unaendesha nchi mpaka sasa. Taasisi nyingi za serikali zilianza kipindi chake. Huo ni msingi wa utawala bora.

Mwalimu atakumbukwa kwa kuweka umoja na mshikamano wa kitaifa lakini alikuwa na mapungufu mengi sana kiuongozi na maono.
Nakubaliana nawe. Lakini nampinga kwa kuuza NBC kwa wageni wakati wazawa walikuwa wanaweza kuinunua!
 
Nyerere
Kwa vyovyote vile hakuna duniani mtu mwenye uwezo wa kurekebisha Historia. Kwa ivo hawa ndiyo walikuwa marais wetu na Samia ndiye Rais wa Tanzania kwa sasa.

Kwa mtazamo wako hawa ukiwaweka kwenye mizani yupi amekuwa Rais bora kwako na kwa nini ukiangalia changamoto alizokabiliana nazo na jinsi alivyozitatua na unadhani kwamba amecha alama (Legacy) gani kwa watanzania wote.
Alikuwa rais wa hovyo kuwahi kutokea nchi hii!
 
Back
Top Bottom