Kwa hitimisho lako , uzito unalalia wapi?
Ukimtoa Nyerere hapo sioni hata mmoja aliyewafanyia au kuwaongoza watanzania nakuwapa maendeleo. Nyerere aliwaza mbali kuwapa watanzania lugha ya kuelewa ya Taifa na kuwatoa katika lugha zao za kikabila. Ilikuwa kazi ngumu Sana lakini alifanikiwa. Akakubali vyama vingi baada yakuona watanzania wanaelewa. Waliofuata wangekuwa waelewa wangeiimarisha katiba imulike watanzania wote bila kujali wapinzani. Kwa uchungu walionao watanzania tungekuwa mbali hata wizi chuki visingekuwepo. Hawajachelewa embu wavitoe.
Naweza kusema kipindi Cha JK na Lowasa walifanya Jambo ambalo mpaka leo linasaidia Sana watanzania, shule za kata. Huyu ndiyo anaweza kuonekana alikuwa na mikakati ya kusaidia watanzania na vizazi vijavyo.
Tatizo la hiki chama cha CCM ni wabinafsi, wafitini, wana michuki, waongo, wapenda sifa n.k.
Nyerere alituachia zawadi kubwa Sana ya lugha. Tusingekuwa na lugha yetu ya kuelewa kipindi Cha mwendazake tungekufa watu wengi Sana na lingeweza kitokea vita Kali baina yetu sisi wenyewe. Huyu alihatarisha amani, kawagombanisha dola na raia na vyama vya upinzani, kajanga chuki ya vyama na vyama, kajenga chuki baina ya Tanzania na mataifa mengine kajifanya ni mrusi wa pili, kajenga chuki kwa Raia kutokana na vyama vyao. Kasumbua familia za watu bila sababu kwa ajili ya kijenga makaravati. Kaondoa ubinadamu kabisa.
Mkapa hakuna alichokifanya zaidi ya kumfilisi mtanzania kamwacha anatembea na ndala badala ya kumtenge ezea ajira kaja kuuza viwanda na kubi afsisha, pamoja na ukali wake. Tunaweza kusema ni afafhali hata mkoloni angebaki.
TUFANYE JE?
Tuanzie pale kwa Nyerere alipoachia lugha ya Taifa na kupambanua mambo mengine yawe yakitafa zaidi.
Shule tunapambana kila mtu apate elimu.
CCM iondoe chuki na ubinafsi walionao wakubali Tanzania inajengwa na watanzania wote bila kujali kichaa, mpinzani, mgonjwa n.k. Watanye maridhiano ya kurudisha mchakato wa katiba mpya ili kutangeneza mihimili yenye nguvu zaidi. Hata Kama hakutaluwa na serikali ijiendeshe bila usumbufu wa jeshi na kuingia kwenye vita. Mfano kuwe na makatibu amba watachaguliwa na pande mbili za vyama kulingana na katiba mpya itakavyopendekezwa.
Yatengenezwe makundi mawili ya vyama ili kuunganisha huo utitiri wa vyama au vifutwa kuwe na pande mbili za vyama.
Yaani vyama vibaki Kama vilivyosajiliwa viungane viwe upande mmoja ili kuhojiana na upande wa pili wa chama na mihimili itakavyoundwa. Hapa tutapata wabunge.
Ikiewezekana ofisi ya msajili ipigiwe kura na wananchi au ifutwe kabisa kwa sababu inagombanisha vyama.
Hii ndiyo kazi muhimu katika kuleta maendeleo ili kuondoa watu wapenda madaraka na wachochezi wa chuki na wafitini.