Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na Samia, yupi Rais bora kwako?

Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na Samia, yupi Rais bora kwako?

weww humjui nyerere umezaliwa 1987 unataka kutuelezea stori za 1969 utayajua
Kama unaona magufuli ni bora kwasababu yakuziba mirija ya mtu huo umri wako mkubwa umekusaidia nini sasa?.Yaani wewe mtu anayetoa matamko ya mdomo ndo unamwona wa maana kuliko nyerere aliyeweka mifumo na misingi inayoishi hadi leo.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Nyerere huyu ambaye ilimshinda akatoka balu!!

Ni wa hovyo tu japo hamfikii Ngosha
Nchi imemshinda vip?.Ulitaka aendelee kuongoza hadi miaka mingapi wakati ameshaongoza zaidi ya miaka 20.au wewe ata historia ya nchi yako huijui unadandia dandia tu hoja.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Daaa MUNGU anakuona na hata hayati magu pia anakuona c kw tusi ili .....
Wewe Magu kwangu ni zero brain,uwezo wake wa akili ulikuwa mdogo ila nyie wenye akili ndogo ndio mnamuona alikuwa shujaa wenu but he was a failure kila sehemu,sitanii namaanisha..

Ni kama Lisu umuulize hili swali yaani utashangaa kura zitakuwa kwa JK,Mwinyi na Samia ila hao wengine kwake ni hamna kitu..
 
Hongera wewe unayeijua.
Ila mimi nnachokijua Nyerere alidhulumu nyumba za Babangu kwa kisingizio cha Azimio la Arusha.
Hiyo ndo historia ya Nyerere nnayoijua mimi
Itakua baba yako alikua fisadi.Pole sana kwakutoka povu kulipa machungu ya baba yako.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Kwangu Nyerere ni bora kwenye Kujenga Utaifa na Tunu za Utaifa .

Mkapa ni bora kwenye kuleta mageuzi ya Uchumi na Uongozi.

JK ni bora kwenye kukuza private sector, Welfare economics na demokrasia..

Samia nae ni bora kwenye mambo ya Welfare economics na biashara ila akipata second term huenda akawa namba 2 baada ya Nyerere.

Mwendazake ni zero brain kuliko wote.[emoji116]
Naunga mkono hoja napigilia misumari nchi 12
 
Wapumbavu mnampambanisha rais magufuli aliyedumu miaka mitano na hao waliokaa miaka kumi!? Ebu oneni aibu basi ....lakini pamoja na hayo yote kawaacha mbali sana marais wengi uliowataja
Urais sio kubeba vyuma.kwamba unavyobeba sana ndivyo unavyojazia sana.ukiwa rais bora ata siku 2 zinatosha kabisa kufanya mapinduzi ya kila kitu.Hiyo miaka 5 ilitosha kabisa kufanya makubwa na ndo maana uongozi ni miaka mitano.ukishindwa kwenye hiyo miaka 5 ya kwanza usitegemee jipya ata ungekaa miaka 50.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Maksi zao ni kama ifuatavyo:
1.J.K.Nyerere-90
2.B.W Mkapa-50
3.J.M.Kikwete-40
4.J.P.Magufuli-30
5.A.H.Mwinyi-10.
NB:S S.Hassan bado hajamaliza hata awamu moja ya urais,hivyo bado ana incomplete.
Yaani Hapo kwa Mkapa na Mwendazake ni 0% juu ya zero. Anzia mkoloni barabara zinajengwa.

Naweza kukusaidia hizo alama tunaweza kusema waliwajengea watanzania ufukara kwa ajili ya tamaa zao za misifa.

JK afafhali na shule za kata.
Nyerere 💯 sawa. Alijitahidi Sana.
 
Alijenga uchumi gani alileta sera za ujamaa upumbavu tu
Alikua na kosa gani kuamua kua mjamaa.zote ni sera na zimeshatumika mataifa mengine zikafanya kazi.Nyerere kwa miaka hiyo aliona ndo mrengo unaofaa kwa mtazamo wake.Basi tuseme nyerere alikosea je mbona waliofuata hadi sasa hatujui ata tuko mrengo gani.Kama bado tuko kwenye ujamaa basi nyerere alikua sahihi kwasababu tulipaswa tujue kama tumeachana na ujamaa na tuko mrengo fulani ila ni kimya kimya tu uku kaubepari uku hatueleweki.Wengine wako azimio la arusha wengine ubepari yaan bora miaka inaenda.Nyerere alifanya makosa yake lakini je waliofuata waliyarekebisha vip ili nchi iwe kwenye msingi sahihi.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Magufuli angekiwa Rais mzuri sana baada ya Nyerere shida approach zake kwenye uchumi na human rights zilikuwa mbovu-kutokana na yeye mwenyewe kukosa exposure.
 
Mchango wa Nyerere kwa wana Africa "wanyonge" unatambulika hadi Vatican.
 
Kwa vyovyote vile hakuna duniani mtu mwenye uwezo wa kurekebisha Historia. Kwa ivo hawa ndiyo walikuwa marais wetu na Samia ndiye Rais wa Tanzania kwa sasa.

Kwa mtazamo wako hawa ukiwaweka kwenye mizani yupi amekuwa Rais bora kwako na kwa nini ukiangalia changamoto alizokabiliana nazo na jinsi alivyozitatua na unadhani kwamba amecha alama (Legacy) gani kwa watanzania wote.
Wote ni bora kwa vipindi vyao!!!
 
Mama samia ni raisi anayejitahidi sana kwa maana kwanza ni mwanamke , pili ni mama tatu ni bibi halafu bado ni raisi so anajitahidi sana sio kila mama anaweza hili hongera sana Rais wetu popote ulip juu mimi nakukubali.

Raisi waliokuwepo wakawa wamekufa wote Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi .
Wote walijitahidi kadri ya uwezo wao.

Nyerere kaleta uhuru

Mkapa alifanya mengi kutukasamehewa madeni akatengeneza uwanja za mipira zikawa zakisasa na mengine mengi

Magufuli alitengeneza miundombinu akanunua ndege akatengeneza hospitali na akanunua meli za kisasa akatengeneza barabara za reli , za kawaida na kufufua reli za zamani kazifanya mpya na akanunua zingine na akawapandishia watumishi waserikali mishahara akahakikisha sekta zote watumishi wanafanya kazi kwa raha kingine alitengeneza chato ikawa kama uzunguni.

Akatengeneza shule , maji , na mambo mengi mengine mazuri .
Viva Magufuli .
Japo alibana pesa sana .

Kikwete nilimpenda aliachia hela zote mpaka akiba yote ikakata huyo ndio niliwahi kumpenda kwa anavyoongea na mwinyi na kwasasa mtotowake. Anaongoza visiwani .

Ila kwakweli maraisi wetu wote na wapenda sana ,,congrats all and especialy mama samia i love u mama samia for our peace of our country beutiful madam .[emoji38][emoji3059][emoji7][emoji8]
Popote ulipo kongole kwako umeupiga mwingi
Ujinga Tu kuwa mwanamke ndio exception
 
Back
Top Bottom