Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na Samia, yupi Rais bora kwako?

Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na Samia, yupi Rais bora kwako?

Kwa vyovyote vile hakuna duniani mtu mwenye uwezo wa kurekebisha Historia. Kwa ivo hawa ndiyo walikuwa marais wetu na Samia ndiye Rais wa Tanzania kwa sasa.

Kwa mtazamo wako hawa ukiwaweka kwenye mizani yupi amekuwa Rais bora kwako na kwa nini ukiangalia changamoto alizokabiliana nazo na jinsi alivyozitatua na unadhani kwamba amecha alama (Legacy) gani kwa watanzania wote.
Nyerere bado anaongoza, aliunganisha nchi kwa lugha ya kiswahili akatusomesha wengi tu tena bure kabisa.

Akajenga mamia ya viwanda, akakuza umoja wa kitaifa na akafanya mengi tu ambayo waasisi wenzake walishindwa kuyafanya katika mataifa yao. Alitambua umuhimu wa Mungu kuongoza taifa tangu usiku mmoja kabla ya ule ambao bendera yetu ilipandishwa pale uwanja wa Uhuru.

Walifuatia wamejaribu kadri walivyoweza na sasa tunaye mbeijing Samia katika usukani.
 
Jakaya , maana watu walikuwa na mipunga....Yaani Jakaya angepiga miaka 20 tungekuwa mbali ,enzi za jakaya ukitangaza kuuza kiwanja leo ndani ya wiki ushauza ,enzi za jakaya kabla jengo halijaisha nafasi zote zimejaa.
Dah umenikumbusha enzi hizo kakangu alikuwa anajenga ghorofa Magomeni Idrisa, lilijaa wapangaji waliolipa kodi ya mwaka kabla ya kuisha jengo wakawa wanamghasi amalize haraka
 
Nyerere alifanyakazi nzuri Sana ya lugha. Alivalisha watanzania utanzania japo mababu zetu waliendelea kufa masikini. Angembembeleza mkoloni asiondoke kabisa ili vijana kipindi kile wasome na madarasa yajengwe. Angewaacha wandelee kuendesha sehemu za ujenzi na viwanda ili kuproduce mashina katika nchi yake.

Amelinda Mali Leo hii watanzania wauza mpaka viwanda. Hapa titaona pamoja na kusaidia Taifa kwa lugha alizalisha wezi, matapeli, wavivu wa kufikiria wanafiki, waongo, wapenda sifa, waongeaji kupitiliza kuliko matendo.

Angepata wachapazi wasaidizi wakadili na Elimu ungekuta tukombali Sana.
Kwa hitimisho lako , uzito unalalia wapi?
 
Hongera wewe unayeijua.
Ila mimi nnachokijua Nyerere alidhulumu nyumba za Babangu kwa kisingizio cha Azimio la Arusha.
Hiyo ndo historia ya Nyerere nnayoijua mimi
Zilikuwa mkoa gani??
 
1.Mkapa alikuwa rais bora kwangu, alikuwa jasiri akiyeweza kwenda kubadili sera mbovu za kiuchumi za Nyerere na Tanzania kupaa kiuchumi

2. Nyerere japo alizingua kwenye uchumi lakini ali set vizuri misingi ya nchi na hakuwa mbinafsi kama viongozi wengi wa Afrika miaka ile

3. Kikwete, alikuwa lax kidogo japo chiji yake sekta binafsi ilishamiri, uhuru na demokrasia, miundombinu ya elimu na usafiri

4.Mwinyi huyu simjui sana kwa undani lakini nasikia aliachana na sera za Nyerere na kufungua milango kwa soko huria na wananchi kupata sana ahuen, ila hakuwa mtu wa kuchukua maamuzi magumu, na alikuwa akiiishi sana kwenye kivuli cha Nyerere

5. Magufuli, huyu alikuwa mtendaji mzuri na mfuatiliji mzuri wa miradi, na kuanzisha miradi mingi pia, lakini hakuwa mwana mikakati mzuri, hakuwa na busara za kutosha kuwa kiongozi mkuu wa nchi, alikuwa na maamuzi mengi ya pupa na uelewa mdogo wa uchumi na siasa

Samia, Samia naona kwa sasa hafai kulinganishwa sababu ndio kwanza hajamaliza hata miaka 2, lakini kwa mwendo anaoenda nao anaweza kuipeleka nchi mbali kichumi na kiutawala bora na kuwazidi wengi hapo
Kwa hitimisho lako, jiandae kupigwa mawe
 
Wapumbavu mnampambanisha rais magufuli aliyedumu miaka mitano na hao waliokaa miaka kumi!? Ebu oneni aibu basi ....lakini pamoja na hayo yote kawaacha mbali sana marais wengi uliowataja
 
Kwangu Nyerere ni bora kwenye Kujenga Utaifa na Tunu za Utaifa .

Mkapa ni bora kwenye kuleta mageuzi ya Uchumi na Uongozi.

JK ni bora kwenye kukuza private sector, Welfare economics na demokrasia..

Samia nae ni bora kwenye mambo ya Welfare economics na biashara ila akipata second term huenda akawa namba 2 baada ya Nyerere.

Mwendazake ni zero brain kuliko wote.[emoji116]
Daaa MUNGU anakuona na hata hayati magu pia anakuona c kw tusi ili .....
 
Back
Top Bottom