Wote wabovu tu.
Nasema wote wabovu kwasababu makosa yao ndio yameleta matatizo makubwa na kuletea watu umasikini mpaka leo, kifupi makosa yao ndio yameamua mustakabari mbovu.
JK NYERERE - alishindwa kujenga mfumo imara wa maisha ambao ungetumika kuinua maisha ya watanzania milele, kuukumbatia ujamaa ulioshindwa akiamini angeweza kuutumia na kuleta tija ndio chanzo cha matatizo mengi mpaka leo.
AH MWINYI: aliipokea nchi ikiwa imechoka na kuchakaa na matatizo mengi kutoka kwa JK NYERERE, sera yake ya Ruksa na kukumbatia mabepari bila udhibiti kuliigeuza nchi danguro na kuharibu kabisa mifumo ya maisha.
BWM : Huyu sera yake ya ubinafsishaji wa mashirika ya umma bila udhibiti imara ulileta matatizo makubwa ambayo yataendelea kuitafuna nchi milele milele. Kupitia ubinafsishaji kuna jamii ziliutumia mwanya huo na kuishia kuifirisi nchi na ndio ikawa chanzo cha ufisadi mpaka leo.
JK: Huyi alitaka kuleta modern style of management kwa kuwatawala watanzania kwa kufuata basics za uongozi bila kujua anaongoza majitu majinga na mapumbavu matokeo yake alisababisha matatizo makubwa ya wizi na ufisadi usio na kikomo, makosa haya yanaigharimu nchi mpaka leo.
JPM: Binafsi namuita mwamba, huyu makosa yake makubwa ni kutoijua siasa ya dunia na kuamini kwenye theory, Theory aliyosoma darasani na historia za viongozi wapigania uhuru zilimuharibu ubongo wake. Matokeo yake akajikuta anakwenda kupiga pua chini na kuiacha nchi hohehahe.
Kuwa muumini wa ujamaa ambao ukweli pia hakuujua vizuri zaidi ya theory za shule, kujaribu kupractice ujamaa karne ya 21 kwenye nchi ambayo haina msingi wa chochote.
MWISHO KABISA, KILA KITU KINAANZIA KWENYE BASICS, BASICS KWENYE DUNIA HII NI KUWAPA WATU MAARIFA BORA NA SAHIHI... HAO WOTE HAKUNA ALIYEWEZA KUWEKA MAZINGIRA BORA KWA WATU KUPATA MAARIFA SAHIHI NA KUYATUMIA KUJILETEA NA KUILETEA NCHI MAENDELEO, WOTE NI FAILURE TU.