Nyie wanawake wa siku hizi mnaojitafuta kwanza kabla ya ndoa nani atawaoa?

Nyie wanawake wa siku hizi mnaojitafuta kwanza kabla ya ndoa nani atawaoa?

ukiona mwanamke kakwambia anajitafuta kwanza ujue hakupendi tu mwanetu, kuna koloni lake analisubiri lieleweke maana moja kati ya sifa ya ke ni kuolewa hata kama atakua anategemewa na ukoo wao mzima
 
Wengi wao ni wadangaji tu. Ukitaka kuamini fuatilia tamasha lao la 'super woman' yaani 80% wamelipiwa tiketi za tamasha hilo na wanaume na wamepewa mitaji na maisha na wanaume kuhadaa umma kuwa wao wanajiweza kiuchumi bila wanaume.
 
Naona saiv hili suala la wanawake kujitafuta kiuchumi kabla ya kuolewa lmekua common sasa.

Zamani tulizoea mwanaume ndo anajitafuta kwanza kisha aoe lkn saiv meza imepinduka, kila mwanamke unaekutana nae kwenye mahusiano anakwambia anajitafuta kwanza ndo aolewe, anataka anunue kiwanja ajenge mara aanzishe biashara n.k

Kuna mwingine unamwambia nataka tufunge ndoa mwaka huu au mwakani anakwambia yeye badobado kwanza bado kuna vitu hajaweka sawa hahaah.

Naombeni tu kujua nani atawaoa? au mnataka muanze kuoa?
Mwache atafute wewe endelea na mambo yako
 
Back
Top Bottom