Nyimbo za utotoni za zamani ambazo watoto wa leo hawazijui

Nyimbo za utotoni za zamani ambazo watoto wa leo hawazijui

Kifuku kimefika,kwaheri mvua
Matope yakauka mabarabarani
Nasi twaenda shule kwa raha kuu
Nimeota ndoto nzuri leo.
 
katinganya katinganya kati..midabwada
katinganya katinganya kati...inapepea
katinganya katinganya kati....kama bendera
Hili song nilikuwa nalitumia kubambia..! [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
Hahahaha ..nimekumbuka mbali sana na hzo nyimbo za utoto mpk nimeridisha nyuma miaka fasta najihic nipo katikat ya michezo ...

Ila kuna huu wimbo wa
Tiyari bado ..
Bado .

Wwengne wanaenda jificha
Mmoja anazinga mpira kati kati wakubutua ...kunawale wengne walikua wanajificha unatafuta mpk bac kumbe wanayao
 
Namtafuta rafiki rafiki rafikii
Rafiki yako naani naani naanii
Rafiki yangu Meendee Meendee Meendee
Huu mti gani, wa mchongoma
Nikiukata haukatiki
Hata kwa panga, haukatiki
Hata kwa shoka, haukatiki.

Hahahahaaa wewee Bujobuji weweee hehehehehehehhee
Huu wimbo niliuimba sana nikiwa mdogo. Na tulikuwa tunapenda kuuimba tukiwa tumetumwa dukani.
Umenichekesha sababu hapo ulipoweka rafiki yangu Mendeeeee Mendeeeee Meendee, kuna uzi mmoja jana nilicomment huu wimbo baada ya mshana jr kuweka picha ya vitoto 2 vikiwa vimeshikana na vinaobekana vinatembea barabarani.

Kwenye wimbo asilia wakati tuko wadogo hapo kwenye meendee tulikuwa tunataja majina yetu halisia mfano rafiki yangu atanitaja. ....rafiki yangu Kasie Kasie Kasie. .. na mie ntamtaja rafiki yangu Nyanzoo Nyanzoo Nyanzoo....

Sasa niliyosema hapo umeweka meendee aahahahahahahaa umenichekesha.... unajua Mende ni nani? Achilia cockroach. ..... aahahahahahahhahahahahahahaaa

Halafu ujue Bujibuji siku zote nikionaga avatar yako huwa naona una vituko kama huyo muigizaji wa ki nigeria.
 
Kinyulii kinyulike,
Mwanangu mwa jumbe,
Kavaa nguo mbili,
Ya Tatu kajitandika, ukaka Sina urembo alie juu na aruke... pruuuu
 
Hahahaha ..nimekumbuka mbali sana na hzo nyimbo za utoto mpk nimeridisha nyuma miaka fasta najihic nipo katikat ya michezo ...

Ila kuna huu wimbo wa
Tiyari bado ..
Bado .

Wwengne wanaenda jificha
Mmoja anazinga mpira kati kati wakubutua ...kunawale wengne walikua wanajificha unatafuta mpk bac kumbe wanayao
Kombolela..
 
Linanukaje Linanukaje. ...
Fwiii Fwiii kabwelaaaa

Nina ndoo yangu eeeh
Ya kuchota maji eeeh
Usiku na mchana, eehh
Maji ya dhahabu eeeh
Ya kuoga baba eeeh
Pamoja na mama eeeh

Watoto msitizame nyuma.... Yai bovu linapotaa.

hahaha sisi tuliongezea hapo😀
 
Palikuwa mwenye shamba, akaenda shambani,
akalima lima lima akaona almasi,
loh loh loh baha-hati, loh loh loh baha-hati,
loh loh loh baha-hati kwa mtu mwenye shamba!

akatupa jembe pale akaenda mjini
kununua motokaa, akaona fahari
loh loh loh baha-hati, loh loh loh baha-hati,
loh loh loh baha-hati kwa mtu mwenye shamba!
 
Hahahahaaa wewee Bujobuji weweee hehehehehehehhee
Huu wimbo niliuimba sana nikiwa mdogo. Na tulikuwa tunapenda kuuimba tukiwa tumetumwa dukani.
Umenichekesha sababu hapo ulipoweka rafiki yangu Mendeeeee Mendeeeee Meendee, kuna uzi mmoja jana nilicomment huu wimbo baada ya mshana jr kuweka picha ya vitoto 2 vikiwa vimeshikana na vinaobekana vinatembea barabarani.

Kwenye wimbo asilia wakati tuko wadogo hapo kwenye meendee tulikuwa tunataja majina yetu halisia mfano rafiki yangu atanitaja. ....rafiki yangu Kasie Kasie Kasie. .. na mie ntamtaja rafiki yangu Nyanzoo Nyanzoo Nyanzoo....

Sasa niliyosema hapo umeweka meendee aahahahahahahaa umenichekesha.... unajua Mende ni nani? Achilia cockroach. ..... aahahahahahahhahahahahahahaaa

Halafu ujue Bujibuji siku zote nikionaga avatar yako huwa naona una vituko kama huyo muigizaji wa ki nigeria.
Ubarikiwe sana, Na ziwe wenye heri Na baraka siku zako zijazo
 
Maji ya mdimu maji ya mdim
Saaagasagasagasaga
Kufunika
Kufunua..

Halafu sijui unaendelea aje huko mbele..! Daaah uzee unanikaribia..!
Mdoondoo paaah (mnapiga makofi)
Cha kwanza paaah
Cha pilii paaah cha tatu path
Cha nne..... ( ) hapa ukipiga makofi unainamishwa chini na tunakuwa tumekaa mduara. Halafu mtu ana kupiga konzi ukiinuka unaambiwa sema nani kakupiga ukikosea unainamishwa tena hadi upatie hahahahhahahaaa ukiona mkong'oto umezidi unakimbia.

Hahahahahahaa.
 
Back
Top Bottom