Nyimbo za utotoni za zamani ambazo watoto wa leo hawazijui

Nyimbo za utotoni za zamani ambazo watoto wa leo hawazijui

Namtafuta rafiki rafiki rafikii
Rafiki yako naani naani naanii
Rafiki yangu Meendee Meendee Meendee
Huu mti gani, wa mchongoma
Nikiukata haukatiki
Hata kwa panga, haukatiki
Hata kwa shoka, haukatiki.
Eeembe dodo moja kwa pesa
ukienda shamba, mbili kwa pesa

au
Paulo usije kucheza na sisi
una mikono michafuu
hutaki kunawa sabuni ni dawa una mikono michafu
 
Linanukaje Linanukaje. ...
Fwiii Fwiii kabwelaaaa

Nina ndoo yangu eeeh
Ya kuchoka maji eeeh
Maji ya dhahabu eeeh
Ya kuoga baba eeeh
Pamoja na mama eeeh

Watoto msitizame nyuma.... Yai bovu linapotaa.
ukimaliza hapo, ni kusubiri kuoga kula na kulala. Stress free life.
 
Nipeleke Nipelekee waapiii kwa Mpemba
Kwa Mpemba kuna nini Jamilaaa katobolewa
Katobolewa na nani.. mchaga muoga duka aaah

Waa Jamilaaa shilingi imempoza
Kavaa dontachii namwitaa anadenguuaa.


Matikitii kudondokaaa
Matikitii kudondokeaaa
Matikitii kudondokaaa
Matikitii kudondokeaaa. ...
 
ikii na hookoo na nche nche nche na ntena ncheeee...
Alieye kula Donaa.. na ....(nimesahau) ya kuchomaaa...

adoo msalale, (nimesahau)... kaondoka tenaa...

hizi lugha na haya maneno ya ujanjaujanja sijui asili yake ni wapi? Du....

Huu wimbo tuliuimba wakati wa kabla kombolela haijaanza. Kwa kupitia wimbo huu anapatikana atakaeanza kuwatafuta wengine(atakae anza kurishi kwa lugha ya mwanza)...

kama huu mlefu, ulikuwepo shortcut

"Funguaaa sodaaaa, Kunywa majiiiii"
 
huu uzi umenifanya nimeu-miss utoto wangu[emoji31] [emoji31] [emoji31]
 
Mjini Tanga kuna nyumba mbili,
Nyumba ya kwanza ya mama Salima,
mama Salima ni mtu mwema sana,
kila apitaye bwana pita ndani,
kila apitaye bwana pita ndani,
ukiuliza nini mchezo wa Landani,
Aliya kweche kweche, aliya kweche msumeno.
 
Mimi mama yenu,ee, ninanguvu tele,ee,zakumua simba ,ee,simbanimkali,ee, du utoto raha sana hapo walishashiba menu ya sambili hahahaha
Umekosea bwana. Mimi mama yenu sina nguvu tena za kuua simba, simba ni mkali, aliua baba, akaua mama sasa kimbieniiii!!!! Hao mtakimbia mpaka mmoja akamatwe.
 
Nilikuwa na mwenzanguu, nalimpenda moyoni
tarumbeta ikalia, tukaenda wote pia rafiki na mimiiii raafiki na mimi,
mwendo wetu wote sawa, tulikuwenda vitani, na rafiki karibu karibu yangu, tukaenda wote pia, pamoja na mimi pamoja na mimi.
na risasi ikampata akatoka moyo we, siku wahi kuagana kwa sababu kupiganaa, rafiki kwaheri, raaafiki kwaheri.

Tulifundishwa na mtu aliyepigana vita ya pili ya dunia that was in sixties tukiwa la kwanza. Alipigana Burma.
 
Pajero pajero
Mama kapika ugali
Na kifaranga cha kuku
Tia hapa tia hapa....
Kama hautaki niambie..........
 
Mama wa kambo, mbo
Mbona wanitesa sa
Sasa naondoka ka
Kaa peke yako ko
Koti la babu bu
Bubu asemi mi
Mimi nasema ma

Mwengine aendelee..

Hizi nyimbo hata origin haijulikan..!
Mimi mdogo
Gogo la mti
Tina na mjuba
Baba mkubwa
Bwawa la samaki
Kingi majuto
Tone la maji
Jitu la kale
Lenye madevu
Vumbua dhahabu

Nshavuruga [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] sikumbuki
Nakumbuka mwisho tunaimba ule windo wa TAUSI NI NDEGE WAKO....
 
Amina panda mlima
Siwezi kupanda
Kwann huwezi kupanda?
Naumwa na tumbo
Tumbo hilo kakupa nani?
Kijana hassan
Kwann usikatae ?
Naona utamu
Siku ya kwanza Utamu yes yes utamu
Siku ya pili utamu yes yes utamu
Siku ya tatu utamu yes yes utamu
Siku ya nne ng'aa ng'aa

Hivi akiyetunga nyimbo hii alifilia nn? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wimbo nilikua naupenda huu! Haswa pale kwenye UTAMU!
 
mwanangu kua kua nikutume
nikutume wapi kwa mfalme
kuna ng'ombe zetu 12
mmoja kafa kaliwa nyani
nyani mkinda tumkindule
tusole visiga vya bwana chuma
bwana chuma gani simdodo
simkindu dawa kanabuba..

nadhani na kizaramo ndani humo wala tulikuwa hatujui maneno mengine maana ake nini😀
Kwa kweli aisee [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom