Nyimbo za utotoni za zamani ambazo watoto wa leo hawazijui

Nyimbo za utotoni za zamani ambazo watoto wa leo hawazijui

Machungwa mawili mpenzi yapo mezani, ukirudi kazini mpenzi via miwani
Jiwe la utete mwingereza kalitelekeza,mwanamke hakutaki ya nini kumbembeleza,
Umempiga kiss,na barua kumuandikia,anapita analia mchechei na maua yake
 
Hao watoto wenu wa ushuani wanaosoma st anne maria sijui mary....huku kwetu uswazi kama kawa, juzi nimewasikia wanaimba ukuti ukuti saa mbili usiku umeme ulikuwa umekatika.....hawakuacha mpaka uliporudi nikasikia HUOOOOOOOOOOOOOOOO!
Dah mkuu unanikumbusha mtoni mtongani enzi inzo...
Nataka kuzi-document kwa ajili ya watoto wa ndugu zangu walioko nje
 
Ushuani watoto pia wanachelewa kuongea, Huku kwetu Kwamtogole msuto unaanza ukiwa na mwaka mmoja. Ukifisha miaka miwili wewe ni mtaalamu hata matusi unayajua.
Hivi ni kwanini ushuani watoto hukawia sana kuongea kuliko uswazi??
 
Hivi ni kwanini ushuani watoto hukawia sana kuongea kuliko uswazi??
uswahilini watoto wanatukanwa sana, wanatukanwa Na wazazi, house girl, majirani yaani Kila MTU.
Kwa hiyo mtoto anakula Na hasira ya kurudishia matusi hivyo Basi hujifunza haraka sana kuongea Na mtoto wa uswahilini anajua matusi mengi kuliko vyakula. vyakula anavyojua ni uji, chai Na chips. wakati mtoto wa ushuani anajua corn flakes, yoghurt, cheeses, sausages, Na kadhalika
 
Ushuani watoto pia wanachelewa kuongea, Huku kwetu Kwamtogole msuto unaanza ukiwa na mwaka mmoja. Ukifisha miaka miwili wewe ni mtaalamu hata matusi unayajua.
[emoji2] [emoji2] [emoji2] umenichekesha sana kwa hbr ya msuto.
 
Jamani mmenikumbusha mbali sanaa miaka ya 1990-1992, nilipokuwa shule za vidudu MWADUI shinyanga mitaa ya boidi ya chini.

Wale tuliofanikiwa kuishi MWADUI miaka hiyo tutafutane jamani, tujikumbushiee enzi zile za maziwa ya token, hahahaha
 
Kobhyala mwanangosha jilole bhaganda bhaganda , ong'waro oli mwana wa nkema, olemi olisunda sunda
 
"Nilikwambia ukalale,
sijakwambia uvuje kitanda,
Oyaaa yaa, oya yaa mwana kilangeee.."
 
Sungusungu unaenda wapi, naenda mazikoni,
nani amefariki, mzungu na baniani,
kideedee zunguruka, ukitaka inama inuka x2
 
Tatu katatuka
Kapanda juu kaanguka
Kichupi chake kinanuka
.......................................

Cc womanity
 
Mganga wa tausi anaitwaje anaitwaje,
kalumanzila la lala salama ma mama mzazi zi zizi la ng'ombe mbe
mbele ya nyumba mba mbali na wewe we wembe wa kucha cha chakula kitamu mu
mungu mkubwa bwa bwawa la samaki ki kingmajuto to tone la maji ji jitula kale le lenye madevu vu,
vumbua dhahabu bu bubu hasemi mi mimi mdogo go gogo la mti ti tina na mjuba ba baba mkali li mbona wanitesa sa sasa naondoka ka kaa peke yako ko kodi ya gheto to toa nigegede...........
 
Back
Top Bottom