Nyongeza ya mishahara TUCTA wamasema wamepokea malalamiko, watatoa tamko

Nyongeza ya mishahara TUCTA wamasema wamepokea malalamiko, watatoa tamko

...kadiri mdhahara unavyokuwa mkubwa ndivyo ssilimia ya huo mdhahara inavyopungua hadi juu kabisa...
😂😅Mdhahara?!!!
Ukute huyu ni mtumishi wa ngazi ya juu wa TUCTA🤔 halafu unatarajia maajabu!
 
Kama now hawawez kusimamiwa then hata katiba mpya ikija still hawatosimamiwa

Katiba ni Jambo moja but wazimamizi wa hiyo katiba ni Jambo lingine

Sisi hatuna shida na katiba, Sisi tunashida na wasimamizi wa katiba ambao bado wataendelea kuwepo hata tukileta katiba mpya kila wiki
Katiba Mpya itaainisha namna ya kupata hao wasimamizi kwa haki, so watakuwa ni halali na watatenda HAKI., Siyo hao haramu waliopatikana kwa wizi, unyang'anyi, udanganyifu na hila!!!!
 
Ile nyongeza ya 23.3% iko wapi?
Tunajisikiaje watumishi wa umma wanapodanganywa na Serikali kama watoto wadogo?
Au Unaweza kukuta ni typing error. Yaani walimaanisha 2.33% badala ya 23.3%?. Alafu hesabu za decimal ngumu aiseee.
 
Unakwama wapi?Katiba itaweka mifumo ya checks and balances ambazo sasa hivi inafanywa na uvccm.Wamekuingizia mawazo yao mgando kuwa kama hii Katiba mbovu haisimamiwi vema tusiandike Katiba Mpya ya Wananchi kwa sababu hiyo?Kweli hapo upo serious Ndugu?
Kama now hawawez kusimamiwa then hata katiba mpya ikija still hawatosimamiwa

Katiba ni Jambo moja but wazimamizi wa hiyo katiba ni Jambo lingine

Sisi hatuna shida na katiba, Sisi tunashida na wasimamizi wa katiba ambao bado wataendelea kuwepo hata tukileta katiba mpya kila wiki
Huu ndio ukweli mchungu, maana hata hii iliyopo mtu anaikanyaga na vyombo vya kuilinda vinafumba macho.

Mkuu Gellangi,
Hao ni CHAWA, wapo kazini, wametumwa kufanya KAZI batili ya kupinga Katiba Mpya ili mifumo chakavu iendelee!!!
 
Yaani Tunatumia trilioni moja kama nyongeza kuwalipa hawa watumishi wasio fanya kazi?

Hii ni hasara kubwa mno.
 
TUCTA msitake wafanyakazi wa nchi huu wachukue maamuzi magumu dhidi yenu...

Mmeshirikiana na serikali kuwafanyia udanganyifu wafanyakazi wote wa nchi hii kwa hiki mlichokiita nyongeza ya 23.3% ya mishahara...

Mmewafanya wafanyakazi wa nchi hii wajinga na wapumbavu wa kiwango cha juu sana kwa sababu tu wamewaamini nyie kuwepo ktk nafasi hizo..

Tangu mwaka 2015 hadi sasa, TUCTA hamfanyi kazi yenu ya msingi ya kutetea na kupigania maslahi na haki za watumishi wa nchi hii na badala yake mmeshirikiana na waajiri akiwemo mwajiri mkuu - serikali kukalia na kukandamiza maslahi na haki zao mbalimbali kwa sababu tu nyie mnakula mtakavyo na kutembelea mav - 8...

Nitaeleza kwa mifano miwili namna mlivyoshindwa kushughulikia na kunyamaza kimya wakati wote maslahi na haki za watumishi zilipokanyagwa na serikali...

1. ANNUAL SALARY INCREMENTS - ASI
✓ TUCTA mnafahamu kabisa kuwa, hii ni haki ya kila mtumishi na ni iko automatic kila mwaka kwa kila mtumishi ktk ngazi (salary scale) aliyopo kwa miaka mitatu mfululizo hadi anapobadilishiwa daraja la kiutumishi maarufu kama "kupandishwa cheo" kwa kigezo cha umri wake kazini na vingine...

✓ Lakini kwa ukatili wa hali ya juu kabisa na kwa kuvunja sheria waziwazi, Hayati Rais Magufuli aliisimamisha haki hii ya kisheria kwa watumishi wote wa daraja la kati na la chini kwa miaka sita au saba mfululizo na Rais Samia anaendeleza ukatili huu huku TUCTA mkiwa kimya tu...

✓ Kwa sababu ASI ipo kisheria na sheria imevunjwa na mwajiri yaani serikali, basi ni wajibu wa TUCTA kwa niaba ya wafanyakazi wote kwenda mahakamani na kuidai na serikali ilipe arrears zote za ASI kwa watumishi wote wa umma tangu mwaka 2015 mpaka sasa. Lakini mmefanya nini? Mko kimya ni kama kwamba chama hiki ni tawi la CCM...!

2. PERIODIC SALARY INCREMENTS - PSI

✓ Hii hufanyika periodically i.e mwaka 1, au miaka 2 nk kwa kuzingatia vigezo vingi kubwa ikiwa ni kubadilika kwa gharama za maisha tokana na mfumo wa bei za huduma na bidhaa pamoja na thamani ya shilingi...

✓ Kwa miaka sita ya serikali ya Hayati Magufuli, serikali ilinyima watumishi wa daraja la kati na la chini haki hii licha ya gharama za maisha kupanda kila kuchao huku watumishi wa daraja la juu akiwemo Rais mwenyewe, mawaziri, wabunge na wengine wa aina hiyo wakiogelea kwenye mishahara na marupurupu mengi na ya kufuru. TUCTA mmekaa kimya tu kwa sbb na nyinyi mko huko huko na wafanyakazi wa nchi hii wakiwatumikia ninyi...

✓ Kilele cha uonevu huu dhidi ya watumishi wa umma wa daraja la kati na la chini wa nchi hii umedhihirika kwa UONGO wa nyongeza ya 23.3% iliyotangazwa na Rais Samia Mei 1, 2022 - Dodoma..

✓ Haileweki hakika ni nini kimetokea kwani katika mishahara ya mwezi huu July, 2022 kila mtumishi amepata nyongeza kati ya Tshs. 8,000 hadi 54,000 kwa maana mwenye mshahara mdogo wa kima cha chini amekuta 54,000 imeongezeka..

✓ Hii siyo 23.3% bali ni mtu alikaa sehemu na kuamuru "ongeza kiasi hiki kwa hawa, na hiki hawa". Watumishi pekee walioonja nyongeza kubwa ni wanajeshi yaani JWTZ ambako utafiti mdogo umeonesha kuwa nyongeza yao iko kati ya TZS 150,000 mpaka 350,000. Kwa upande wa majeshi mengine kama polisi, magereza nk nako ni kilio mtindo mmoja. Sijui ni nini hasa maana ya tendo hili baya la kibaguzi...

✓ Uthibitisho wa hili ni kuwa, mpaka sasa hakuna waraka wa kiutumishi kuhusu mabadiliko ya mishahara ya watumishi wa umma wa mwaka 2022 uliokwisha tolewa kama ilivyo kawaida ya miaka yote inapotangazwa nyongeza au mabadiliko ya mishahara...

✓ Waraka uliopo na unaotumika mpaka sasa ni ule No. 7 wa mwaka 2014 wakati wa Rais Jakaya Kikwete ambao uliweka kima cha chini cha TZS 265,000. Huu wa mwaka 2022 uko wapi ambao ndiyo unanyambulisha nyongeza ya kila kada ya utumishi ili kila mtumishi aone kwa sababu hizi ni zama za ukweli na uwazi...?

✓ Waraka unaotembea kwa kasi kwenye mitandao ya kujamii na ulio wazi hadi sasa ni ule wa mabadiliko ya posho za safari za kikazi tu ambao huo nao hauwahusu watumishi wa daraja la chini kama walimu, manesi, madaktari, nk nk maana hakuna safari zozote kwao...!!

## Sasa basi, tunaitaka TUCTA iwaeleze wafanyakazi wa umma wa nchi hii ukweli wa nini hasa kimetokea. Ni udanganyifu wa namna gani huu uliofanyika kiasi cha kuwakatisha tamaa hivi watumishi wa nchi hii? Ni kwanini serikali ifanye udanganyifu wa wazi na mbaya kiasi hiki kwa wananchi wake...??

## Ni kwanini tangu Wizara ya fedha ishikwe na Mwigulu Lameck Madelu Nchemba kumekuwa na mambo ya ajabu ajabu sambamba na tozo na kodi zisizokuwa na kichwa wala miguu...?

Hebu CCM jitokezeni na waelezeni wananchi ukweli. Mnaipeleka wapi nchi hizi...?
 
TUCTA ni backing dog aside na meno
Backing[emoji808]️ barking[emoji818]️
Hawa tucta Wana Upuuzi , Kama wanalalamika waache kazi, mshahara haijawahi kutosha kamwe, tangu lini kitu Cha kupimiwa kikatosha, wafanyakazi wafanye kazi mbadara kwa lengo la kuinua mapato yao

Sasa Hilo tamko litabadiki nyongeza???
 
Majibu yake
 
Tucta ni uhqro sana. Yamezoae kula ela za wafanyakazi na hawana wanalolifanya. Mambo ya Ovyo Sana
 
Mwigulu anamvizia mama 2025. Mama naye hajui hili.
1. Tozo nyingi
2. Kupanda gharama za maisha
3.Upendeleo ajira
4.....
6.....
Rais akusema Waziri hatekelezi. Hasira zinabaki kwa mama.

Tutegemee utendaji kazi mbaya kywahi kutokea.

Bora asingetamka
 
IMG-20220723-WA0000.jpg
 
Upo vizuri, umeandika kitaalam sana. Watumishi wanarudi kwenye ubabaishaji tena, walianza kurudi kwenye mood ya kufanya kazi kwa weredi sasa wanapotea tena.
 
Back
Top Bottom