NYUMA YA PAZIA: CHADEMA ilivyosalitiwa 2015 - Dkt. Slaa

NYUMA YA PAZIA: CHADEMA ilivyosalitiwa 2015 - Dkt. Slaa

Huyu bwana ni muongo sasa Lowasa amesharudi na yuko CCM tayari unafikiri zile siri kama zipo za alichokifanya lowasa atakizungumzia tena humo, sijui kama watakutana uso kwa uso
Alichopinga Slaa Ni Lowasa aliyetangazwa km Ni fisadi na chadema Wenyewe kuwa mgombea urais wa CDM baada ya kukatwa CCM. hakupinga Lowasa kuwa mwanachama wa CDM. hata leo Lowasa karudi CCM km mwanachama na si kiongozi. Dr Slaa ataendelea kuwa mwanasiasa waupinzani makini na Bora kuwahi kutokea TZ.
CHADEMA Ni matapeli wa siasa. Wanachohubiri sicho wanachokiamini.
 
Vipi ameelezea pia uhusika wa Josephine Mushumbuzi kwenye harakati zake na uhusika wake pale 2015??

Ameelezea aliendaje Canada na aliishije.
Vipi Ile press ya pale Movenpick zamani ameelezea nani aliyeilipia?

Ana sababu zipi za msingi zinazomfanya awe ni mtu mwenye msimamo na kusimamia anachokiamini?

Kwanini anaiunga mkono awamu ya tano? Na kwa tafsiri yake je upinzani usiwepo Tanzania??

Kama hayo kaelezea nanunua kitabu..
CHADEMA matapeli hamna hoja. Mbuzi nyie!
 
Sasa Huyo babu mzinzi, si auteme ubalozi baada ya lowasa na rostam kukaribishwa red carpet ikulu.
 
Aisee hiki kitabu kimewaacha uchi matapeli wa siasa. Hata km Ni chungu wajitahidi kunywa kwani Ni dawa. Wasome tu 😂😂
 
Sasa Huyo babu mzinzi, si auteme ubalozi baada ya lowasa na rostam kukaribishwa red carpet ikulu.
Msihamishe magoli. CHADEMA ni matapeli wa siasa. Chukua kitabu soma, Hata km chungu Ni dawa!
 
(Pichani kitabu kikianza kupatikana kwa Wabunge, Dodoma)

Na. M. M. Mwanakijiji

Umpende au umchukie, umkatae au umkubali, umpinge au umuunge mkono Dkt. Wilbrod Slaa Dr Willibrod Slaa anabakia kuwa miongoni mwa wanasiasa wachache Tanzania ambao alama zao katika zama na nyakati za kisiasa ni vigumu kufutika. Unaweza kumuita majina mengi na ya rangi mbalimbali ya kejeli lakini ni vigumu kupuuzia, kudharau au kutupilia mbali mchango wake katika siasa za Tanzania kwa karibu miaka ishirini na mitano. Mchango wake katika kuimarisha siasa za Tanzania akiwa miongoni mwa wabunge wa kwanza kabisa wa upinzani umeacha historia kubwa kuanzia Karatu hadi Dar, toka Tunduru hadi Tarime.

Hata hivyo, matukio ya kisiasa ya mwaka 2015 yanabakia katika historia yetu kama mafundisho makubwa kabisa ya siasa zinavyoweza kuwafanya ndugu wawe maadui, marafiki wake mahasimu, na kutengeneza kile ambacho wenzetu Wamarekani wanasema ni “strange bed fellows” yaani kuwaona watu usiowadhania wamelala kitanda kimoja. Matukio haya yalitokea taifa likiwa katika mwamko mkubwa wa uchaguzi mkuu wa Rais na Wabunge.

Dkt. Slaa akiwa Katibu Mkuu wa chama Kikuu cha upinzani cha CHADEMA, alitarajiwa na alipitishwa na chama chake kuwa mgombea wa Urais huku mtifuano mkubwa ukitarajiwa na hatimaye ulitokea ndani ya Chama cha Mapinduzi. Kwa baadhi ya wachunguzi wa siasa mtifuano au mnyukano uliokuwa unatokea CCM ulifanya kazi ya mgombea wa upinzani uliounganika kuwa ya afueni zaidi.

Hata hivyo, kinyume na matarajio ya watu wengi na kinyume na mantiki zilizozoeleka za kisiasa Edward Lowassa aliyekatwa jina lake ndani ya CCM ambako alikuwa anaongoza kwa mashabiki na kura za maoni alikimbilia CHADEMA na kusababisha chama hicho cha upinzani kulala kitanda kimoja na mtu ambaye walitumia muda mwingi kumhusisha na ufisadi nchini. Ilisemwa “yeyote” isipokuwa CCM. Dkt. Slaa akafyekelewa mbali na chama chake na kusababisha mpasuko wa aina yake ndani ya CCM na CHADEMA.

Dkt. Slaa akaamua kuachana na siasa za vyama na yeye na familia yake wakahamia Canada. Miezi michache baadaye Rais John Magufuli alimteua Dkt. Slaa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden kitu ambacho kilitafsiriwa na baadhi ya watu kwa namna mbalimbali.

Katika kitabu cha NYUMA YA PAZIA Dkt. Slaa anaelezea kwa kina matukio mbalimbali ambayo yalitokea hadi kufikia Lowassa kukaribishwa CHADEMA na kwa nini hakuwa tayari kusimama jukwaani kumnadi Lowassa na akabakia na utimamu wa kimaadili na akili. Hata hivyo, kitabu hiki kinaenda zaidi ya nyuma ya pazia la siasa za 2015. Inatufunulia kumuelewa Dkt. Slaa kwani kwa kiasi chake kitabu hiki pia ni bibliografia (historia ya maisha) ya mwanasiasa huyu nguli, mcheshi, na msomi.

Ndani ya kitabu hiki tunaweza kukutana na mtu ambaye anatufundisha mambo mbalimbali kuhusiana na uongozi. Mojawapo ya mambo ambayo msomaji atayafurahia atakapokutana nayo ni jinsi gani Dkt. Slaa ni mtunzaji mzuri sana wa kumbukumbu. Siyo tu katika akili lakini katika nyaraka na vielelezo mbalimbali. Anataja tarehe, mahali na siku kama shahidi katika kesi nzito. Bila utata anataja pia majina mbalimbali ya wahusika mbalimbali katika ujasiri ambao utawakumbusha watu wengi ile hotuba yake ya “Orodha ya Mafisadi” ya pale Mwembe Yanga.

Kitabu hakigusi siasa tu za 2015 lakini pia kinatudokeza safari ya Dkt. Slaa kutoka upadre hadi kuwa mwanasiasa mbobezi. Wengi watashtushwa, kushangazwa na kuburudishwa na masimulizi yake ya mikutano yake na Baba wa Taifa Mwl. Nyerere wakati huo Dkt. Slaa akiwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu. Pia watakutana na jinsi gani Dkt. Slaa alisimamia kupinga ufisadi ndani ya Kanisa Katoliki kiasi cha kumgonganisha yeye na mmojawapo wa maaskofu waandamizi wa wakati huo. Msomaji pia ataburudishwa na masimulizi yake ya kujaribu kuinua hali na maisha ya watu wa Karatu katika kile ambacho kilimsababishia kuwa mbunge mpendwa sana wa wana Karatu na kuthubutu kufanya kitu ambacho hakikuwahi kufanywa Tanzania – Karatu kuwa Halmashauri ya kwanza ya mji kuongozwa na upinzani.

Kubwa hata hivyo, ni sakata zima la siasa za 2015 na matokeo yake katika upinzani na siasa za Tanzania. Kitabu hiki kinatoa maonyo, mwongozo, na elimu kwa wanasiasa wanaofuatia katika upinzani na chama tawala na wapinzani watarajiwa na watawala watarajia. Mwanasiasa yeyote ni lazima apate nakala ya kitabu hiki, mwanahistoria yeyote ni lazima anunue nakala yake wakati wanafunzi wa shule na vyuo watapata elimu muhimu juu ya uongozi kutoka katika kitabu hiki kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili.

Nyuma ya pazia ni kitabu kinachomfunua mbele yetu na kutujulisha kwa undani juu ya mtu, maisha, zama na nyakati za Dkt. Wilbrod Slaa, Balozi, Baba, Mume na miongoni mwa viongozi maridadi ambao Tanzania imepata nafasi ya kuwa nao na wameacha alama zisizofutika. Umpende au umchukie, umkatae au umkubali, umpinge au umuunge mkono Dkt. Wilbrod Slaa ametupatia hazina ya maarifa ambayo wenye hekima watawahi kuipata katika nakala chache ambazo zimeshaingia nchini.

UNAWEZA KUPATA NAKALA YAKO WAPI?
Unaweza kupata nakala yako kwa bei ya jumla au rejareja. Bei ya reja reja ni shilingi 20,000/- TU na kwa bei ya jumla unaweza kupata punguzo kubwa kufuatana na mahitaji yako.
Maeneo ya posta, mkabala na Jengo la Benjamin Mkapa karibu na Mahali yanapoegeshwa magari yaendayo Sinza yenye michoro ya Rangi Nyekundu.
Mhudumu Genoveva - 0753 059 144
Au wasiliana na Erasto Tumbo kuweza kuagiza nakala zako:
0713 474707/0688 211683
Mods tupe muongozo kama katika hili jukwaa matangazo ya biashara yanaruhusiwa.
 
Kwa anayependa kujifunza, kuna mengi ya kujifunza kutokana na maisha na falsafa ya Dr Slaa, hasa kama kitabu kweli kimetoka kwa Dr mwenyewe na si account ya mtu mwingine kutokana na story za kuunganisha. Kwa upande mmoja, nashawishika kununua kitabu hiki sio tu kwa nitakayojifunza kutokana na mapitio ya Dr, lakini pia ununuzi Wangu uwe kama shukrani kwa mchango wake kwa demokrasia Na siasa zetu kwa ujumla. Kwa upande mwingine, nachelea kuamini kwamba ni wakati muafaka kwa Dr Slaa kuandika kitabu hiki, kwa alipo sasa kwenye maisha yake. Kuna mchangiaji ametukumbusha kuhusu aliyosema Dr kuhusu shambulio la Lissu, kwa hiyo siamini yuko kwenye nafasi muafaka (right frame of mind) ya kuwa huru na honest kwenye anayoamua kushare.

And that is a deal breaker for me, any other time might have been a different story.
 
Huyu mzee laana imemkalia ya usaliti,hakuna laana mbaya kama kuacha kazi ya Mungu kwa tamaa za uzinzi,akaoa ndoa katoliki akamsaliti mke wake wa ndoa,akaoa dada yetu,mara akatudanganya Chadema akatusaliti tena.

Oh namkimbia Lowasa sasa mbona mko chama kimoja. Na mzee babu huyu anatumika kama kondomu,yeye anakula hela za ubalozi bado tamaa ile ile anaichafua Chadema ili auze vitabu na vitadoda kweli.....

Huyu babu atakula kibeliti kibaya sana juu,ila simhukumu basi tu.....akae alale tu.
 
Kuna watu kutoka mikoani nao walikuwa wanaulizia wanaweza vipi kukipata. Angalia kwenye posti ya kwanza nimeweka update ya sehemu nyingine ambazo unaweza kupata nakala yako.
 
Dr. Slaa sina hakika kama ana makandokando ya ufisadi kama aliyonayo huyu rais tuliyempata. Pamoja na hayo, bado ninaamini CCM ni kansa ya kisiasa na kijamii kwa Tanzania. Tanzania inawezekana bila CCM.
 
Mama junior hujambo habari za sweeden, sisi huku bado tunasubiri ahadi ya shule yetu uliyotuahidi kabla ya kukimbilia ughaibuni.

Huku kwetu Ibwera umasikini umezidi maisha ni magumu kuliko wakati wa JK, tunashindia mihogo ukipata tutumie angalau kidogo.

Mpao obashule bona okwo omumahanga
Watafute watu wa Sweden watakwambia anaendeleaje. Kama unashindia mihogo ni matatizo yako binafsi. Shule Zipo ni pesa yako na matatizo yako unataka Mpaka iandikwe Jina unalolijua.
Kwa taarifa yeye yuko Canada
 
Toka jana nakisoma kitabu Nyuma ya Pazia: Chadema ilivyosalitiwa 2015 alichokiandika Willibrod Peter Slaa, PhD. Katika ukurasa wa 54 na 55 anatufahamisha kuhusu kuwepo kwa utamaduni wa Maaskofu wote wa Kanisa Katoliki kuzuru Vatican na wakiwa huko wanapaswa kuzuru makaburi ya Mt. Petro na Paulo.

Kumbe kwenda kusali kwenye makaburi ya wapendwa wetu siyo vibaya wala ajabu ee!

AD LIMINA VISIT
(Visitatio ad limina apostolorum) Refers to the periodic visit to Rome required of each residential bishop (CIC c. 400; Pastor bonus, no. 28) and military vicar approved by apostolic authority (S.C. Consist., Feb. 28, 1959, AAS 51:272). This visit is directly tied to the quinquennial report that is required of each residential bishop every five years in c. 399, as the visit is to be made the same year as that in which the report is submitted (c. 400 & sect.1).

The 1983 Code of Canon Law has made the bishop's obligation to make the ad limina visit personally, and only if he is impeded may he satisfy the obligation through another, i.e. his coadjutor, the auxiliary, or a suitable priest who resides in the diocese (c. 400 & sect. 2). Since auxiliary and other titular bishops are not the primary pastors of a particular church and have no quinquennial report to make, they are not held to the ad limina visit.

This visit has a sacred meaning, since "the bishops with religious veneration pay a visit to the tombs of Peter and Paul." It has a personal meaning, "because each individual bishop meets the successor of Peter and talks to him face to face," and it has a curial meaning, that is a "hallmark of community, because the bishops enter into conversation with the moderators of the dicasteries, councils, and offices of the Roman Curia" (Appendix 1, no. 6, of Pastor bonus ).

The purpose of the visit, for the bishops, is "the strengthening of their own responsibility as successors of the Apostles and of their hierarchical communion with the Successor of Peter" (Congregation for Bishops, "Directory for the 'ad limina' visit," in L'Osservatore Romano, July 11, 1988).

The ad limina visit has changed considerably under the pontificate of John Paul II from a canonical formality into a genuine exercise of the pope's care for all the Churches. As stated in the "Directory for the 'ad limina' visit," it is "an important moment in the exercise of the Holy Father's pastoral ministry," because he receives the bishops and discusses personally with them their questions concerning "their ecclesial mission."

Though there is no concrete date in which the visits started, "There are, however, numerous testimonies which speak of its existence from the 4th century" (Orti, Accompanying Historico-Juridical Notes to the "Directory for the ‘adlimina' visit
 
Back
Top Bottom