Nyumba iliyojengwa na Bushiri Ali Harthi bado iko Pangani mkoa wa Tanga

Nyumba iliyojengwa na Bushiri Ali Harthi bado iko Pangani mkoa wa Tanga

Nyumba ya Bushiri Ali Harthi, iliyojengwa kwa Matumbawe na udongo, bado ina nguvu kama ilivyo, inayopatikana Pangani, mkoani Tanga. Nyumba ina basement, ambapo mazungumzo ya watumwa yamefichwa.

Bushiri alipigana vita na Wajerumani (Bushiri Revolt 1888 - 1889) na kushindwa sana, kukamatwa na kuhukumiwa hukumu ya kifo, kunyongwa tarehe 15 Dec 1889 huko Pangani.

_________

Bushiri Ali Harthi's House, built from Coral and clay, still strong as it is, found in Pangani, Tanga region. The house has basement, where a chattel of slaves hidden.

Bushiri fought a war with Germans (Bushiri Revolt 1888 - 1889) and desperately defeated, apprehended and sentenced to a death sentence, hanged on 15th Dec 1889 in Pangani.
Bushir na bwana heri
 
Biashara ya utumwa iliendelezwa na Ottomans, soko kubwa la awali lilikua Misri mpaka Arabuni. Wazungu walianza kununu watumwa baada ya kupata makoloni na kuanza kulima kuanzia Brazil, Mexico, Jamaica mpaka North America.
Kwa uhakika biashara ya utumwa ilikuwepo tengu enzi za awali hata kabla ya hiyo Ottoman Empire.

Wakati wa Roman Empire 2000 BC tayari walikuwepo watumwa, sema enzi hizo walikuwa watumwa wazungu wenzano wa kutoka 'porini' au walioshindwa vita walivyokuwa wakipigana.
 
Waizrael walikaa utmwani Misri kwa miaka 40.
 
Mzee Mohamed Said naomba tukubaliane kitu kimoja. Kwenye biashara ya utumwa pande zote zinastahili lawama tofauti na tulivyosomeshwa zamani.
Wazungu walifanya biashara ya utumwa, hali kadhalika waarabu na watemi wa jamii zetu waliwauza weusi wenzao kwa waarabu, na wazungu kwa jamii za Afrika Magharibi. Sisi tuli supply wao wakanunua. Wote wananuka jinai hii dhalimu.
 
Waarabu wote walikua wanafanya biashara ya watumwa kama si kuuza walikua wananunua na wengine walikua wanakusanya watumwa. Kwahiyo hamna mwarabu hapa tanzania ambaye babu yake hakuhusika kwenye biashara ya utumwa
Anza kusoma na kupata elimu angalau kidogo, tafadhali!
Idadi ya Waarabu, hasa kutoka Hadramaut (Yemen), walifika visiwani baada ya kufungwa kwa soko la watumwa. Kazi yao mwanzoni ilikuwa kubeba mizigo kwenye bandari na kazi nyingine duni. Mababu wa Abdulrazak Gurnah walikuwa Waarabu maskini vile waliofika baada ya mwisho wa biashara ya watumwa.
Hakuna kupinga hapa kwamba Waarabu waliendesha biashara ya watumwa katika Afrika ya Mashariki (kwa kushirikiana na watawala wa Kiafrika...) . Lakini kujumlisha kundi jinsi unavyofanya ni mbali na ukweli wowote.
AU - unatambuaje leo hao Waafrika ambao mababu wao waliuza watumwa? Je hao wa leo wana kosa?
 
Wazungu ndio walifanya biashara ya watumwa wala hatukatai ila hapa kwetu tanzania waarabu ndip walikua vinara wa biashara ya utumwa na wareno mzee acha kutetea warabau kwasababu ya dini
usisahau Waafrika waliofanya biashara hiyo pia pande zote mbili, magharibi na mashariki
 
Anza kusoma na kupata elimu angalau kidogo, tafadhali!
Idadi ya Waarabu, hasa kutoka Hadramaut (Yemen), walifika visiwani baada ya kufungwa kwa soko la watumwa. Kazi yao mwanzoni ilikuwa kubeba mizigo kwenye bandari na kazi nyingine duni. Mababu wa Abdulrazak Gurnah walikuwa Waarabu maskini vile waliofika baada ya mwisho wa biashara ya watumwa.
Hakuna kupinga hapa kwamba Waarabu waliendesha biashara ya watumwa katika Afrika ya Mashariki (kwa kushirikiana na watawala wa Kiafrika...) . Lakini kujumlisha kundi jinsi unavyofanya ni mbali na ukweli wowote.
AU - unatambuaje leo hao Waafrika ambao mababu wao waliuza watumwa? Je hao wa leo wana kosa?
Hawa wana fikra kuwa waarabu wote walikuwa matajiri wenye kufanya biashara ya utumwa. Wengi walikuja kujitafutia riziki tu kama waafrika walioondoka hapa kwenda ulaya. Wao na wahindi wengi waliokuja mwanzo wa karne ya ishirini walikuwa ni masikini na wakitembea hata bila kuvaa viatu.
 
usisahau Waafrika waliofanya biashara hiyo pia pande zote mbili, magharibi na mashariki
Nitajie hao waafrika huku tanzania walikua waarabu au machotara wa kiarabu. Huku sisi hatujawahi uzana ni baada ya ukoloni ndio tumekuwa mazipe zipe tunauza nchi yetu
 
Ndugu zanguni,
Ikiwa mnataka historia ya utumwa ni vizuri sana mkasogea mbele na kusoma The Across Atlantic Slave Trade na Belgian Congo Slave Trade.
Vipi kuhusu Slave Trade Across the Indian Ocean?
Mzee wetu siku utakapoamua kuwa objective kwenye thinking yako wengi sana tutakuamini.
Ila hii religious inclination yako inakufanya uonekane kuwa very irrelevant.
Why bother yourself to defend Arabs. Kweli kabisa hakuna kitu kibaya kwenye maisha kuwa mentally enslaved
 
Back
Top Bottom