Nyumba ya Oscar Kambona sasa ni Feza Primary. Nini kimetokea?

Nyumba ya Oscar Kambona sasa ni Feza Primary. Nini kimetokea?

Kama tu nchi ina wasomi wengi kwa sasa lakini UBEPARI unaitafuna nchi sijui miaka ile nyerere angekimbilia ubepari nchi ingekuwa na hali mbaya kiasi gani yani mali nyingi zingekuwa chini ya wazungu na mambo ya vita ya madini yanayoendelea CONGO yangekuwepo hadi leon tz maana wazungu wasingekubali kutolewa kiboya na kwa umaskini wa enzi zile tungeuzwaa aisee so NYERERE alitumia akili sana kuukataa ubepari ila kilichomuangusha ni UJAMAA kufail...!! NYERERE angkuwa na ubepari bhasi amini hakuna Rais wa afrika angemfikia utajiriii hata nusu ila ajabu mzee yule hakuacha hata hisa yoyote sio kwamba alishindwa ila alifanya alichokihubiri UJAMAA jambo waliloshindwa viongozi asilimi 98 wenye asili ya kiafrika.
Nakuunga Mkono. Zimbabwe, Afrika Kusini na Congo zilimbilia Ubapari, Sasa zina Amani??
 
Lakini Kambona kaonekana ndie aliyekuwa sahihi kuliko Mwalimu. Yafanyikayo sasa ni mawazo ya Kambona ya Nyerere yalishakufa kibudu
halafu kuna watu flani wana propose awe mtakatifu.Kama kwenye siasa kuna watakatifu anastahili lakini sio kwenye dini.
 
Lakini Kambona kaonekana ndie aliyekuwa sahihi kuliko Mwalimu. Yafanyikayo sasa ni mawazo ya Kambona ya Nyerere yalishakufa kibudu
na tupo wap ss baada ya kufuata sera za kambona ?
 
Mawazo ya Kambona kuhusu uchumi yanaishi hata sasa ya Mwalimu yamekufa
tumefikia wap ? mafisad ndo yanashamir , mtu anapata mpk mishahara 40 hlf kuna md anatafuta kaz , sera za nyerere hazikuwai kumuacha mtu mtaani , siasa hadi kwenye elimu , zero kbs
 
Nyerere alikuwa dikteta uchwara, hoja zake zote alizompinga nazo kambona zilikuja 'kuprove failure',kambona alikuwa anaona mbali kutokana na exposure na elimu, Nyerere alikuwa amemezwa na wachina,akaishia kufeli kwnye kila kitu,azamio la Arusha lilifeli,vijiji vya ujamaa vilifeli, ujamaa wenyewe ulifeli aliachia nchi kwa aibu watu wakiwa hawana chakula Wala mavazi!!
fikra za Kambona ndo zimetufikisha matajir wanapanga bei za bidhaa zipande linj , serikali haina nguvu , siasa hadi kweny elimu hlf baada ya kuhitimu chuo unaenda kuwa houseboy , ukituliza akili Nyerere was doing something amaizing , Mfumo wake ulilenga kumjenga mtu kwa jinsi alivyo sio kwa jins anavyotaka , huba uwezo shulen bas mapema unafelishwa ukalime au ukawe mpongo au mjeda , leo hii mkulima anafaulisha mpk chuo kea kozi ya IT then anamaliza anaenda kuwa secretary wa clinic fulani kwa mshahara wa laki 3 huki kodi elf 50 usafir 20k chakula laki 1 , huyu mtu anakuja kustuka amezeeka bado anapanga hana hata uwanja , Lazm tumpongez marehem , kuacha sera zake anangaloa tulipo kila mtu hatak kulima anakimbilia mjini hatuna chakula tunanunnua nje , aibu
 
Nyerere usimuamini sana, alikuwa akimuchukia atakuita majina yote mabaya, alisema Iddi Amin ni joka, sijui anakula nyama za watu, kumbe wapi
sw Nyerere ni mbaya , ila Kambona alijali mfuko wake ni mzur , Afrika haitakuja kuwa na kiongoz bora sabab vichwa vyetu vinawaza wizi so tuansifiana wez kwa wez , Nyerere aliweza kuifanya Tz kama Kenyetta alivyoifanya Kenya ila hakutaka , Nyerere aliweza kuibia nchi kama Mobutu alivyoiibia Zaire ila hakujali pesa , Nyerere aliweza kutembea na hazina ya nchi mfukoni kama Nguema wa Guinea ya Bissau ila hakuwaza , Nyerere aliweza kuwa mkali kama Iddi Amini ila hakutaka iwe hivyo , leo hii tunamkashif mzalendo ambae hakujali kuijengea familia yake nyumba ulaya bali akawazia kuijenga nchi , hakiwazia kuwaingizia familia yake kwenye mfumo bali aliwaza kutengeneza watu sahihi kwa taifa miaka ya baadae ila bado tuna mkashif , ili bara limelaaniwa , Enzi za Nyerere tulikuwa na influence kubwa sana ukanda wetu huu ila leo hii Rwanda iko mbali sana kiushawish , aibu hii ,ila yote haya sababu ya kushabikia wanafungua milango ya wiz wa hazina ya taifa , pray for Ngoro x 2 , pray for Kibiti , kitaya , Amboni , Richmond , Wafanyakaz hewa , Mirad fake , walipwa mishahara zaid ya 2 , all this done in this era
 
Kwa matawi yote ya Feza Tanzania hakuna hata tawi moja walilokodi yote ni ya kwao kwa kujenga au kununua.
hakuna cha kuilamu serikali hapo , ingekuwa serikali imefungua ofisi humo tungekuelewa ila Feza ni taasis binafs hatuez mnyooshea kidole yyt mpk tuthibitishe serikali ndo imewakodisha au kuwauzia Feza
 
Nyerere hakusimamia harusi ya Kambona....

Presidential historians tulishalisemea hili....


tanganyika-politician-oscar-kambona-marries-flora-moriyo-london-uk-picture-id878964884
hii picha inaonesha kbs jins alivyo kibaraka wa Mabeberu huyo jamaa , how comes unasimamia sera za unyonyaj wkt taifa ndo linaamka , bila sera za ujamaa tz ingekuwa km india ni taifa kubwa ila kuna large difference kati thos who hav and hav not
 
Jee, unamaanisha mshahara wake uendane na hadhi yake ya kuwa mtoto wa Kambona na si kulingana na kazi anayofanya na CV yake? Namfahamu mtoto wa Nyerere, Anna, anabangaiza tu. Pia nilisoma na Rehema, mtoto wa Kawawa. Naye ni mtu wa kawaida tu kama mimi. Sasa huyo mtoto wa Kambona apewe mshahara tofauti na wengine kwa kuwa tu baba yake ni Kambona?
dada yetu ana ni RIP
 
tumefikia wap ? mafisad ndo yanashamir , mtu anapata mpk mishahara 40 hlf kuna md anatafuta kaz , sera za nyerere hazikuwai kumuacha mtu mtaani , siasa hadi kwenye elimu , zero kbs
Ufisadi sio sera ya mfumo wowote duniani, fisadi anatakiwa auwawe si kwenye mfumo wa ujamaa wala ubepari,thus ulaya chezea mshahara wako na sio kodi ya wananchi au mwananchi usilipe kodi mtapotea.
Sisi ufisadi ni ushujaa pili ufungwi ni kwa sababu ya uozo wa mifumo hatuwezi kujisimamia, tunaishi kwa timing kama mbugani ukipata piga bahati haiji mara mbili at the end tunakuwa tumejiibia wenyewe, maana utapiga utakula na watoto wako then wajukuu zako wanakuja kupata maumivu ya uliyoyafanya. Mfano unapewa tenda ya mradi wa kusambaza maji unakula na afisa wa umma unaenda kununua mabus au malori huku Jamii ikiendelea na shida ya maji.
 
na tupo wap ss baada ya kufuata sera za kambona ?
Tofautisha sera na uozo,mfumo sasa umeooza tunajiendea tupo kwenye autopilot hatuna mfumo wowote tunaoufuata kwa sasa,zaidi KILA mtu apambane na hali yake KILA mtu anawaza kukimbiza mkate.Hatuna dora kama taifa tunajiendea tu bora hata ya wakoloni walikuwa na dira nasi.
 
Ulitaka alipwe shingapi?

Unataka watu waanze kulipwa mamilioni just cos ni watoto wa fulani? Kina Ridh, Pinda, Sokoine, Makongoro nk ni wabunge na nafasi zingine kadha wa kadha na yeye apambane ashike wadhifa hakuna free lunch.
Kambona alikuwa na watoto wa wiwili tu Amos na neema, Amos alipigwa risasi uingereza miaka ya 90 na neema bado yupo huko UK ni mtu mzm sasa, huyo witness sidhani. Kambona alioa mwanamke kutoka kilimanjaro ambaye pia aliwahi kuwa miss tanganyika miss Flora moriyo, harusi ilifanyika St Paul cathedral Church ilikuwa ndio harusi ya kwanza ya watu weusi ilikuwa ni 19.11.1960 na nyerere alikuwa kama mpambe wa kambona kwenye harusi hiyo, jamaa alikuwa kichwa sana ila shida yake aliwakumbatia sn mabeberu kiasi cha kumchafua rafiki yake mpendwa waliyekutana huko tabora kwa mara ya kwanza. Mambo ni mengi muda mchache
WhatsApp%2BImage%2B2019-01-27%2Bat%2B19.28.11%25281%2529.jpg
 
Back
Top Bottom