Labda kosa la Mwalimu lilikuwa kuamini Waswahili tunaweza kuijenga nchi yetu wenyewe, Kambona hakuamini.
Sasa mnasafiri vipi na Mtu anayeamini kingine kama sio kuishi kupinduana.
Congo alikuwepo Shombe na Tanzania Kambona...Kambona aliamini na kuukumbatia sana Uzungu, utaona hata mtindo wake wa maisha ni wa kuiga Uzungu...aliamini bila Wazungu sisi hatuwezi.
Kufaulu au kushindwa kwa muelekeo fulani ni matokeo, na huwezi kufaulu au kushindwa bila kwanza kufanya...na sijui mnavyodhani siasa ilifeli mnatumia mlengo upi, maana sio lazima wote tuwe na mtazamo huo huo...na kama Mwalimu alifeli Congo ndio walifaulu?.
Naona Vijana humu kila mmoja anaandika tu anachokidhania.