Nyumba ya Oscar Kambona sasa ni Feza Primary. Nini kimetokea?

Nyumba ya Oscar Kambona sasa ni Feza Primary. Nini kimetokea?

Kuwa na jumba lile kwa miaka ile maeneo ya Mikocheni sio hohehahe labda useme alipokuwa huko London
Hiyo nyumba ilikuwa kubwa lakini siyo kwa mfanyakazi wa serikali ambaye alikuwa anaruhusiwa kuchukuwa mkopo benki (enzi zile kulikuwa na building society, housing bank n.k). Hata Nyerere mwenyewe alichukuwa mkopo na kujenga nyumba yake ya Msasani.

Na hayo mapesa aliyoyaficha Ulaya sijui yaliishia wapi maana asingeishi maisha ya kawaida sana kama alikuwa nayo.
 
Daaa achana tuu na hayo yote mnayojadili,
Imebidi nisome historia ya kambona n.k...

Yaaani vijana wa zamani walikua wanaenda mbele kama wanaenda magomeni mapipa, na sio tuu kwenda mbele wakifika huko wanatengeneza attention,

Katika kusoma historia ya Kambona, nikapita kwenye hio wedding yake 1967, kwanza ndio alikua mwafrika wa kwanza kufunga pingu za maisha katika kanisa la St Paul's Cathedral, maana walikua hata wazungu wenyewe wa maisha ya kati hawaligusi, Lakini pia Ilifuatiliwa na vyombo vikubwa vya habari Duniai enzi hizo, Alipokea ulinzi wa serikali, kitu ambacho wenyeww walikua hawapati, Alipata wangeni 400, roho tatu wakiwa wazungu na wengi wao ni wenye nyadhifa kubwa, Mwisho iliyengeneza International attention.

Daaa, yaa leo hii baada ya miaka 55, bado kufunga ndoa mpaka watu wapitishe bakuli..
Mgeni mkubwa ni balozi wa nyumba kumi.
 
Nyerere hakusimamia harusi ya Kambona....

Presidential historians tulishalisemea hili....


tanganyika-politician-oscar-kambona-marries-flora-moriyo-london-uk-picture-id878964884
Huyo best man Mwafrika aliyevaa koti jeusi nyuma ya Kambona ni nani?
 
Oscar Kambona ana mtoto wa kike ni Askari Magereza gereza la Karanga Moshi. Kama sikosei anaitwa Witness.
Huwezi amini mtoto wa kambona analipwa mshahara usiozidi TSH laki tano.
Kama ndio mshahara wa kazi yake ulitaka akaibe?
 
Wazoefu wa mitaa ya Mikocheni, kwa Nyerere, kwa Mwinyi, kwa Warioba haya ni majina ya vituo vya daladala. Lakini pia Kuna nyumba ya Oscar Kambona mitaa hiyo ila kwa sasa naona imekuwa shule ya msingi Feza.

Nini kilitokea? Iliuzwa? Je Kambona hakuacha familia? Mke na watoto wake wako wapi? Baba akiwa muasi hadi familia yake inachukuliwa kama waasi?

Je, ilikuwa ni nyumba ya serikali au alijenga mwenyewe Oscar?

We nawe alokwambia pale ni Feza primary ni nani? Feza primary iko Kawe ..
Ile shule inaitwa dar es salaam international school DIS mkewe alipangisha kiwanja kile kwa mkataba wa miaka 40 Kama sikosei baadae tamaa ikamuingia akataka kubadili lakini wp mana mwenye shule ni mzungu yuko makini mkewe kambona akashindwa kesi bs tena Ndio mpaka leo bd wamepanga hapo iyo shule imebaki miaka mingapi sijui mkataba kuisha
 
Hii nyumba Kambona wakt amekwenda Uingereza alimuachia Swaiba wake Abdallah Kassim Hanga baada Hanga kukamatwa kupelekwa mashinjioni Zanzibar chini ya Mzee Abeid Karume nyumbani ile baadae alikuja kuishi Obote alivyopinduliwa na Idd Amin Sina hakika km alipewa tena Kambona au...
 
Nadhani nyumba mikocheni inayojulikana Mama Kambona ameishi muda mrefu na kuimiliki ni ilipo Dsm International School (DIS).

Mwanae anayejulikana ni Neema aliyekuwa anafanya kazi British Council na baada ya kumaliza ndoa yake na Mchaga Masika akaamua kurudi Uingereza. Sidhani kama Kambona ana mtoto mwingine. Nadhani Kambona ana asili ya ugenious maana hata huyo neema ni kama akili zimezidi na kuwa fyatu kidogo in a good way.
 
Mtoto mmoja aliuwawa huko uk na majasusi wa tz
fafanua mkuu,

majasusi wa kitz walimua mtoto wa kambona kwa kosa lipi?. aliwakosea nini?.

alikula chakula chenye sumu alichotegeshewa baba yake?.

alipigwa risasi kwa bahati mbaya baada ya kukosa target ambaye ni baba yake?.
 
Back
Top Bottom