Ila Watumishi wengi wa Umma Nchi hii hawana Ushirikiano kabisa, kazi Yao ni kuimba Solidarity Siku ya Mei Mosi pasi kuionesha Kwa vitendo.
Suala la huyu Meneja wa TRC kuhusu Tozo za makato ya Benki halimuathiri yeye peke yake isipokuwa Watumishi wote kwani Mishahara Yao inapita huko Benki na makato lazima yahusike.
Kutokuwa na Solidarity baina ya Watumishi wa Umma ilifanya hata Hayati JPM hadi anafariki asiweze kuwaongezea hata shilingi 1 kwenye Mishahara yao huku wao wakikaa Kimya tu.
Mama naye amewaongezea shilingi 63,000 Kwa kima Cha Chini na wengine shilingi 20,000 huku Yeye akiishia kuichukua hiyo ongezeko Kwa Mlango wa nyuma Kwa Kuimpose Tozo za Miamala ya Simu, Tozo za Kutoa Hela Benki n.k
So kama Watumishi wataendelea kutokuwa na Umoja baina Yao wataendelea Kuumia hadi Siku Wanastaafu Utumishi wao na kuishia kujenga Makazi Yao Kwa Hela ya Pension tena nyumba ya Vyumba Mbili kwani Kujenga nyumba kubwa watashindwa, Kwani Pension yao ya Mkupuo imeshuka kutoka 100% zamani hadi kuwa 33% Kwa Awamu [emoji119]