Ofisa wa TRC aliyefukuzwa kazi kwa kukosoa tozo akamatwa na Jeshi la Polisi akiwa nyumbani kwake

Ofisa wa TRC aliyefukuzwa kazi kwa kukosoa tozo akamatwa na Jeshi la Polisi akiwa nyumbani kwake

Asante mkuu usiombe hio situation ikukute. I was overstressed!
Kwa kweli huwa siombei maana unakuwa huna amani, furaha yote inatoweka hakuna kitu kizuri kitapita au ukione halafu ukipende, mwanzo mwisho ni mawazo tu.Mungu amsaidie mshikaji asolve hili jambo liishe awe huru basi mambo mengine yatajisort baadaye.
 
Ni vyema kusoma bila kutoa maoni kwani lazima kula mihogo na chachandu mambo yarndelee
 
Wameanza kumtisha ili asitafute haki yake, hili taifa tunahitaji ukombozi wa mara ya pili.

Hatakiwi kukata tamaa, apambane atashinda, hayo ni mapito tu ya nchi yetu.

Mnaosema apambane mpo kwenu mmeweka miguu juu. Mnamuunga mikono behind the keyboard tu.

Jamaa kavamia mtumbwi wa vibwengo ameyakanyaga, atapoteza box na sisi keyboardd warriors kama kawaida yetu tutaishia kumpa moyo tu ila cha moto atakiona peke yake.
 
Hebu tuwe na subira basi. Maana kila mtu ataanza kuongea lake. Ninachoamini Polisi Tanzania ni sehemu salama. Kama kweli yupo au hayupo tutaelezwa.🙏🙏🙏
Mkuu unaamini vibaya, polisi sio sehemu salama
 
Kwa serikali hii ya chawasynthesis lazma muhuni atakomeshwa! Kwanza kavujisha barua aliotwangwa na boss.

Hio situation ya hivyo ilinikutaga staki kukumbuka nilipigwa disclipinary comittee round 2 nikapangua accusations ila mwisho walitumia ubabe tu sababu VC alitaka nikomeshwe.
Hapo ni ubabe utatumika aisee, maana kama suala la barua kuvuja hata Masanja Kadogosa anaweza kuwa ndio mvujishaji maana nae ana nakala.

Vivyo hivyo, jamaa kuanzia tarehe ya barua ile sio mtumishi wa umma, habanwi na sheria za utumishi wa umma.

Pia, kama kungekuwa na malalamiko, Afumisye ndio angepaswa kulalamika kwa taarifa zake kuwekwa hadharani, ila kama yeye ndio ameziweka, Kadogosa atachekesha sana akilalamika mtu kujiwekea hadharani taarifa zake binafsi😀

Tumwombee na tupaze kelele mwana asipotee huko korokoroni
 
Taarifa iliyotufikia hivi punde inasema kwamba Jonas Afumwisye meneja wa TRC aliyesimamishwa kazi kwa kupinga Tozo, AMEKAMATWA NA POLISI.

Wakili wa Meneja huyo Peter Kibatala, amedai kupigiwa simu na Mteja wake Ndugu Afumwisye na kuelezwa kwamba amefuatwa na Polisi nyumbani kwake ambao wametumwa kumkamata.

View attachment 2335762

Chanzo : MwanaHalisi
Wale waliyojidai eti mama anaupiga mwingi oneni sasa. Wahuni wake kina nape mnauye wanaanza kukosa uvumilivu hadi kumkamata mwananchi kwa kutoa mawazo yake. Kazi wamemsimamisha kinyume na sheria ya ajira ya nchi haikutosha sasa wanamkamata.
Walaaniwe wahuni wote.
 
Back
Top Bottom