Ofisi ya CHADEMA Mbeya yachomwa moto usiku wa kuamkia leo

Ofisi ya CHADEMA Mbeya yachomwa moto usiku wa kuamkia leo

CCM au Magufuli hahitaji kuchoma ofisi ya CHADEMA ili kushinda uchaguzi wowote, interesting part ni wanachoma wenyewe siku moja kabla Lissu hajafika huo mkoa, hii kiki wanategemea itampandisha Lissu, upuuzi mtupu.
Unaweza kuthibitiha we mbwiga? Vitisho, ikiwemo matukio kama hayo, hutumiwa sana na vyama tawala visivyojiamini kuelekea uchaguzi kwa lengo la kutisha wananchi!
 
Chalamila nae ni kirusi hapo Iringa ni baadhi ya watumishi waliopata fadhila za kuteuliwa na Rais ila wanachofanya sidhani kama watabaki salama wakati wakiondolewa madarakani maana Mahakama zitajaa kesi nyingi za viongozi waliopita
Apo Iringa ?? Bwa shee we ni wa nchi gani ???
 
Hao wanaochoma ofisi huwa wanalenga kuchoma jengo au nyaraka za chama?!
Au wanadhani kuna kura humo ofisini?!
 
Serikali ya CCM kupitia Jeshi la Polisi ambalo mara kibao limejinasibu kupata taarifa za kiintelijensia za fujo kwenye mikutano ya Cdm limeshindwa kupata taarifa ya Cdm kujichomea ofisi zao ili wapate kiki na kuwachukulia hatua za kisheria?
"Mna akili nyingi sana". Ni ninyi wale wale: Mbowe kavunja mguu kwa ulevi; ofisi za chadema zinachomwa na wanachadema; Lissu kajifyatulia risasi mwenyewe. Kweli mnatisha!
 
Wekeni cctv Watu waumbuke, la sivyo hujuma zitaendelea.
 
Habari hii ni kwa mujibu wa tweet ya kiongozi wa CHADEMA, Parick Ole Sosopi aliyoi-post dakika chache zilizopita asubuhi ya hii.

View attachment 1541770
This is getting serious, vyimbo vyetu vya ulinzi na usalama vinafanya nini

Hii haki inachochea chuki kuelekea uchaguzi mkuu, ni lazima hao wahuni wakamatwe wachukuliwe hatua kali
 
Wewe ------- hujui ulisemalo, Tayari vijiwe vyote washawatambua hao CCM waliopewa hela ya ubwabwa kuchoma ofisi Moto,halafu unakuja na dela lako kuongea utopolo wako hapa
Wanangoja nini kushikwa mkuu, maana si kuna kulipoti police mkiwa na zile tuhuma, na hizo tuhuma zinaanza KUFANYIWA KAZI?

Sasa vijiwe Vyote mpaka vimejuwa kuna watu wamepewa ubwabwa halafu eti bado unalalama badala ya kulifikisha mahali husika ili kukomesha huu upumbavu
 
CHADEMA MSICHOME MABLANKETI OFISINI MKASEMA OFISI IMECHOMWA

Tunapoelekea katika mchakato wa Uchaguzi mkuu 2020 kuna vitendo vingi vinajitokeza vya kuashiria uvunjifu wa amani. Katika hatua za mwanzo tu tunashuhudia CHADEMA kwa nyakati tofauti wakiwa wanaratibu vitendo vya kuchoma nyaraka za ofisi zao kwa kisingizio cha wanaofanya ni watu wasiojulikana.

Tumeshuhudia vitendo hivi vikianza kuota mapembe kama juhudi stahiki hazitachukuliwa na jeshi la polisi katika kuwabana na kuwahoji baadhi ya viongozi katika mikoa hiyo na kubaini vitendo ovu hivyo vinavyoashiria moja kwa moja vinafanywa na CHADEMA wenyewe kwa kisingizio kuwa watu wasiojulikana kuwa wanatenda vitendo hivyo.

Katika kukomesha vitendo hivyo Polisi inatakiwa kufanya DEEP INVESTIGATION ili kubaini vitendo hivyo. kwa kuanzia wanaweza kuanzia kuhusanisha kitendo kilichotokea Mbeya na kile cha Arusha vyote vinafanana kwa sababu zifuatazo:

1. Tukio la Arusha na Mbeya yote mawili yanafanana kwa sababu wachomaji wanachoma nyaraka tu. Mfano Mbeya wamechoma vitendea kazi vya ofisi makaratasi na pia hivyo hivyo na Arusha wamechoma vitendea kazi tena kwa kuchambua ambavyo si Muhimu.

2. Watoa taarifa wote Mbeya na Arusha wanatoa taarifa kuwa ofisi ya chadema imechomwa moto badala ya kusema nyaraka za ofisi zimechomwa moto. Unaweza kuona ni kauli ndogo lakini katika DEEP INVESTIGATION ni taarifa muhimu sana katika uchunguzi ndio maana tunasema haya matukio mawili yameratibiwa na mtu mmoja ambaye ni CHADEMA wenyewe.

3. Ofisi hizi za Mbeya na Arusha si mali ya CHADEMA na mikataba yao inaelekea ukingoni ndio maana wameamua kuchoma. Hapa mchomaji alichagua aina za ofisi za kuchoma moto kwanza si mali za chadema wao ni wapangaji hawana Hasara yoyote juu ya uchomaji huu wa ofisi maana sio mali za chama.

4. Tujiulize walinzi wote wawili wa Mbeya na Arusha wanatekwa na watekaji arafu baada ya muda wanarudi eneo la tukio. Hapa pia kuna uwezekano mkubwa mtekaji huwa anapiga stori na walinzi wanasaidiana kutoa baadhi ya vitu ili wasije wakapata asara kupwa katika kutekeleza mpango wao

5. Pindi taarifa zinapotolewa na Makatibu wa wilaya ya Mbeya na Arusha viongozi wote waandamizi kwa wakati mmoja wanaanza kutoa taarifa kupitia PAGE ZAO za mitandao ya kijamii huku taarifa zao ukizisoma vizuri kwa kutumia DEEP INVESTIGATION utagundua mtuma taarifa alisambaza taaifa moja kwa watu waliokuwa wamejiandaa kuripoti hizi taarifa kwa namna hiyo inadhihilisha kuwa mpanga mpango ni CHADEMA MWENYEWE.

6. Kwa nini wamechagua Mbeya na Arusha na si SIngida wala Tanga au Morogoro ukiangalia mpanga mpango amechagua maeneo ambayo wabunge wa maeneo hayo wamejibapambanua kuwa wao ni wabunge wa siasa za CHUKI ndio maana mipango imetekelezwa maeneo hayo na si maeneo mengine. Hapa ni hofu ya kupoteza majimbo hayo katika uchaguzi huu

7. Kwa nini mtekeleza mpango wa Arusha na Mbeya amesubiri siku wakati Tundu Lisu anakwenda maeneo hayo tu ndio achome hizo nyaraka si wakati anatoka ubelgiji na si wakati yupo kwao Singida na si wakati yupo Tanga au Morogoro hapa ndio patamu maana watekeleza mpango huu hawatumii REASONABLE INVESTIGATION FEEDBACK wakati wanatekeleza mpango huu kuwa watanzania watahoji kwa nini iwe siku ambayo Tundu Lisu anakwenda maeneo hayo ndio ofisi zichomwe moto.

Mwisho kwa masikitiko makubwa nawahasa CHADEMA kumbukeni hizo ofisi ni mali za watanzania waliotafuta fedha za kujenga kwa kujinyima kwa muda mrefu lakini mnakuja kufanya ujinga wa kuchoma mali ambazo si zenu kwa kulipa pango la laki tatu kwa miezi sita. Hapa mnawakosea watanzania kwa kiasi kikubwa kweli

==========ACHENI HUO UHUNI WENU CHADEMA========
 
Vurugu katika mataifa tunayoyaona huwa zinaanza hivi hivi. Tumuombe mungu atunusuru.
 
Back
Top Bottom