Ofisi ya CHADEMA Mbeya yachomwa moto usiku wa kuamkia leo

Ofisi ya CHADEMA Mbeya yachomwa moto usiku wa kuamkia leo

UVCCM mnapotea maboya sana. Dunia ya leo hamwezi kuwaondoa watu huko upinzani kwa vitisho . Pamoja na risasi lakini bado wapo !!.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Hakuna mtu anaweza kuchoma nyumba yake.

Acheni siasa za kijinga
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Haya ma thread ya kipuuzi mnayoleta kila mara ku justify upuuzi mnaoufanya nawaambia tena msijidanganye, msione watu wapo kimya, siku ya kilele ni pale mtapojaribu kuiba kura halafu muonekane, mtalia na kusaga meno, kama kugawana mbao hapo ndipo tutagawana.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Hii sasa janjajanja, watu watawazoea baadae. Balozi na atoe tena tamko, maana it's highly likely an orchestrated move.
Marehemu Tumaini (mke wa Nape), alikuwa anampiga makofi Nape wakati akikaa ukweni Changanyikeni.
 
Nani ametukanwa ?!. Ukiambiwa wewe ni mkarimu, mchoyo, mnafki, mbabe nk umetukanwa eh ?!
Hizo ni sifa za mtu mwenyewe
 
Hii kiki yao imebumu, CD ina scratch na kwa kuwa imebuma huu ujinga utakufa kifo asilia tu, baada ya muda hutasikia tena huu ujinga. Magu / CCM hahitaji kuchoma ofisi za CDM Mbeya wala Arusha ili kushinda
Kinachotakiwa akemee upuuzi huu hasa ndani ya nyumba
 
Asubuhi nilileta uzi unaofanana na huu mkuu, jamaa wanazingua sana kwakweli. CCM wachome office ili iweje? Ni mambo ya ajabu kweli. Ila kwa unafiki huu, Mungu anawaona
Chadema wanatafuta kiki za kijinga
 
Bipolar disorder ugonjwa mbaya sana , yaani mnajiona wajanja mlianza Lissu kapigwa Blankoo sio risasi , mbowe kaanguka kalewa , sasa mmekuja na dunderhead eti Chadema wanachoma ofisi , kuendesha nchi kwa uovu na propaganda hakutawasaidia kitu , Aboubakar Keita wa Mali huko tayari nguvu ya umma imemwondoa , jifunzeni malimbukeni wa kijani kibichi, Belarus is loading another dikteta Lukashenko will be overthrown soon kwa nguvu za umma.
Kwambinu ya kuchoma ofisi mtamtaoa nani siasa za huruma hizo
 
Hakuna mtu anaweza kuchoma nyumba yake.

Acheni siasa za kijinga
kwani ni yake au wamepanga. wanaondoa vile vitu vya muhimu wanachoma ili waweze kutupa lawama upande wa pili na kuongeza chuki ccm ionekane kuwa ni wabaya. Mazingira tuu ya kawaida ccm haiwez enda kuchopa nyumba ya mtu ili iweje. itasaidia nn tofaut na kumpa kiki yule unayemchomea
 
WAMECHOMA MAKARATASI, MAPAZIA HALAFU WANASEMA OFISI IMECHOMWA.

Tunapoelekea katika mchakato wa Uchaguzi mkuu 2020 kuna vitendo vingi vinajitokeza vya kuashiria uvunjifu wa amani. Katika hatua za mwanzo tu tunashuhudia CHADEMA kwa nyakati tofauti wakiwa wanaratibu vitendo vya kuchoma nyaraka za ofisi zao kwa kisingizio cha wanaofanya ni watu wasiojulikana.

Tumeshuhudia vitendo hivi vikianza kuota mapembe kama juhudi stahiki hazitachukuliwa na jeshi la polisi katika kuwabana na kuwahoji baadhi ya viongozi katika mikoa hiyo na kubaini vitendo ovu hivyo vinavyoashiria moja kwa moja vinafanywa na CHADEMA wenyewe kwa kisingizio kuwa watu wasiojulikana kuwa wanatenda vitendo hivyo.

Katika kukomesha vitendo hivyo Polisi inatakiwa kufanya DEEP INVESTIGATION ili kubaini vitendo hivyo. kwa kuanzia wanaweza kuanzia kuhusanisha kitendo kilichotokea Mbeya na kile cha Arusha vyote vinafanana kwa sababu zifuatazo:

1. Tukio la Arusha na Mbeya yote mawili yanafanana kwa sababu wachomaji wanachoma nyaraka tu. Mfano Mbeya wamechoma vitendea kazi vya ofisi makaratasi na pia hivyo hivyo na Arusha wamechoma vitendea kazi tena kwa kuchambua ambavyo si Muhimu.

2. Watoa taarifa wote Mbeya na Arusha wanatoa taarifa kuwa ofisi ya chadema imechomwa moto badala ya kusema nyaraka za ofisi zimechomwa moto. Unaweza kuona ni kauli ndogo lakini katika DEEP INVESTIGATION ni taarifa muhimu sana katika uchunguzi ndio maana tunasema haya matukio mawili yameratibiwa na mtu mmoja ambaye ni CHADEMA wenyewe.

3. Ofisi hizi za Mbeya na Arusha si mali ya CHADEMA na mikataba yao inaelekea ukingoni ndio maana wameamua kuchoma. Hapa mchomaji alichagua aina za ofisi za kuchoma moto kwanza si mali za chadema wao ni wapangaji hawana Hasara yoyote juu ya uchomaji huu wa ofisi maana sio mali za chama.

4. Tujiulize walinzi wote wawili wa Mbeya na Arusha wanatekwa na watekaji arafu baada ya muda wanarudi eneo la tukio. Hapa pia kuna uwezekano mkubwa mtekaji huwa anapiga stori na walinzi wanasaidiana kutoa baadhi ya vitu ili wasije wakapata asara kupwa katika kutekeleza mpango wao

5. Pindi taarifa zinapotolewa na Makatibu wa wilaya ya Mbeya na Arusha viongozi wote waandamizi kwa wakati mmoja wanaanza kutoa taarifa kupitia PAGE ZAO za mitandao ya kijamii huku taarifa zao ukizisoma vizuri kwa kutumia DEEP INVESTIGATION utagundua mtuma taarifa alisambaza taaifa moja kwa watu waliokuwa wamejiandaa kuripoti hizi taarifa kwa namna hiyo inadhihilisha kuwa mpanga mpango ni CHADEMA MWENYEWE.

6. Kwa nini wamechagua Mbeya na Arusha na si SIngida wala Tanga au Morogoro ukiangalia mpanga mpango amechagua maeneo ambayo wabunge wa maeneo hayo wamejibapambanua kuwa wao ni wabunge wa siasa za CHUKI ndio maana mipango imetekelezwa maeneo hayo na si maeneo mengine. Hapa ni hofu ya kupoteza majimbo hayo katika uchaguzi huu

7. Kwa nini mtekeleza mpango wa Arusha na Mbeya amesubiri siku wakati Tundu Lisu anakwenda maeneo hayo tu ndio achome hizo nyaraka si wakati anatoka ubelgiji na si wakati yupo kwao Singida na si wakati yupo Tanga au Morogoro hapa ndio patamu maana watekeleza mpango huu hawatumii REASONABLE INVESTIGATION FEEDBACK wakati wanatekeleza mpango huu kuwa watanzania watahoji kwa nini iwe siku ambayo Tundu Lisu anakwenda maeneo hayo ndio ofisi zichomwe moto.

Mwisho kwa masikitiko makubwa nawahasa CHADEMA kumbukeni hizo ofisi ni mali za watanzania waliotafuta fedha za kujenga kwa kujinyima kwa muda mrefu lakini mnakuja kufanya ujinga wa kuchoma mali ambazo si zenu kwa kulipa pango la laki tatu kwa miezi sita. Hapa mnawakosea watanzania kwa kiasi kikubwa kweli

==========ACHENI HUO UHUNI WENU CHADEMA========
IMG-20200819-WA0201.jpg
 
CHADEMA ni wahuni, ushahidi ni wale waliojitoa CHADEMA kueleza wazi na kwa kina.

Lakini kinachotia kinyaa ni kukubali kutumika na mabeberu. Wameona kwa uchaguzi wa kawaida hakuna namna watapata hata wabunge 5, mbinu mbadala ni kutumika kuleta vurugu kisha mbinyo wa kiuchumi ili mataifa ya magharibi yalazimishe angalau serikali ya umoja Kama si ku engineer vurugu za kuitoa serikali halali itakayoundwa na Mh Rais atakayeshinda.

Ukitaka kujua move yao angalia Tundu Lissu alivyokuja kwa vurugu, matusi na uchokozi wa wazi kabisa. Tunaelewa anatafuta nini. Na ukichunguza kuna ushirikiano wa kampaign zinazoendana na lengo hili na vyombo vya habari hasa vya kimataifa na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGO's). Wachunguzi wa mambo wanaelewa namna ambavyo vyombo vya kimagharibi Kama CIA zinavyo tumia "covert actions" kwa vyombo hivi ili "ku justify" malengo yao yaliyojificha ya kujaribu kuondoa utawala ambao hauungi mkono maslahi yao na kuweka vibaraka.

Uzuri serikali haiishii kuangalia uhuni wa karibu Kama kuchoma ofisi, bali kwenye move zao za mbali zilizojicha kama kampeni chafu ya habari za uongo za vyombo vya habari na taasisi zisizokuwa za serikali, ambazo ndiyo mara nyingi zinabeba agenda za moja kwa moja za mabeberu kupitia ufadhili wa "projects na programs" mbalimbali.

Hatua ya hivi karibuni ya serikali dhidi ya habari ya BBC na kituo cha haki za binadamu inapeleka salaam kwamba serikali inajua mbinu, malengo na mikakati yote wanayoifanya sasa hivi.

Viva Tanzania, viva JPM!
Chadema wako majimboni wanajidhatiti myie maccm bado mnapigana hadharani
 
Ikichomwa ofisi ya CCM wamechoma chadema, ikichomwa ofisi ya chadema wamechoma chadema , lord have mercy
 
Back
Top Bottom