Ofisi ya Kata wanashirikiana na baba yangu mzazi kuninyima haki yangu ya mali

Mzazi kumpatoa mtoto mali yake ni suala la hiyari na si lazima, hiyo haipo kisheria kwamba cha mzazi lazima kuwe na mgao wako. Tafuta zako, kama alivyotafuta zake. Hata ukishtaki unapoteza muda tu, ni hiyari ya mtu hiyo
ila naskia sheria inakataza kutokumpa mtoto maali
 
Soooon tutapata msiba wa mtu kuua baba kwa mwendo huu. Wazazi tukae makini na watoto wa aina hiii maaana huyu akipata Upenyo anammaliza mzeee haraka sana bila kujiuliza. Mzazi kapambana amekulea, amekusomesha hadi UDSM Halafu bado unamganda kiasi hicho???
Mzee akakupime DNA siyo bure wewe ni haramu kwa huyo baba
 
Na ikitokea tu mzazi wake amefariki kwa kifo chochote cha kutatanisha, huyu jamaa atakuwa suspect number 1...

Hajui kwamba anajitengenezea tu bomu hapa...
Kabisa...miaka 42 unataka mgawo

Wakati wenzie miaka ,18 tulistoaway kutafuta maishaa

Ova
 
Haya mafala haya ndo huwa yanaua wazazi haya, hutu jamaa anakoelekea atamuua baba yake, Mzee wa watu achukue RB, na utaozea jela mbweha wewe, mali ya mama yako inakuhusu nini zeee zima la miaka 42?
 
Wewe ni sikio la kufa husaidiki.

Ila, ningekuwa mm mzee wako ningetumia milioni 10 nikuanzishie biashara tena niwape serikali za mitaa wakukabidhi kwa maandishi.

Full duka la jumla la vyakula na kodi nalipa ya miezi mitatu.

Then nahamia mji ninaoutaka naenda kujenga room moja masta tu naishi humo.

Sasa hapo tuone utamudu kulipa hata kodi inayofuata?

Mnakaa tu mmesoma ila akili hamna
 
Angalia usimuue babako kisa hela ukaenda ozea jela bure, tafta vyako aisee huoni aibu wewe?
 
Unatia aibu kamanda... Kwani ndugu zako wengine walipewa uo mgao unao uitaji...
 
Unatia aibu kamanda... Kwani ndugu zako wengine walipewa uo mgao unao uitaji...
wao hawajapewa, nimeshauri wasipewe hawana elimu watachezea tu iyo pesa, mimi nimesoma mpaka chuo kikuu
 
Umefata ushauri wa hovyo

Baba yako mzazi amekaa nawewe mpaka umri huo unaishi kwake unashindwa vipi kuelewana nae akusaidie
Kujifanya msomi na mjuaji mbele ya mzazi haitokusaidia
Jenga uhusiano mzuri na mzee akusaidie kwa hiyari yake .
 
Mtafute jamaa mmoja humu anaitwa Deo Kisandu akili zenu zinaendana atakusaidia sana ushauri
Nahisi hii ni ID nyingine ya Don Nalimison, akili ile Ile!
Ubishi, king'ang'anizi Ka nabii Tito!
 
Ningekua mimi mzee wako mali zote ningeziandika urithi kwa mamako, kanisa na msikiti wa jirani...hupati hata mia, na ukinitanguliza pia hupati ht mia, babda mamaako akugaie yake, na km mama yako hayupo ndo usahau kitu urithi..
Yani ww badala ya kutafta mali zako unawaza za mzee wako...hizo ni za mzee wako yy ndo anaamua azifanyie nn kukupa ni utashi wake sio wajibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…