Uchaguzi 2020 Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa: Vyama vya Siasa vinavyotaka kushirikiana Uchaguzi Mkuu vimeshachelewa kwa mujibu wa Sheria

Uchaguzi 2020 Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa: Vyama vya Siasa vinavyotaka kushirikiana Uchaguzi Mkuu vimeshachelewa kwa mujibu wa Sheria

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Naibu wa msajili wa vyama vya siasa Dkt. Nyahoza amesema vyama vya siasa vinavyojipanga kushirikiana vimeshachelewa.

Nyahoza amesema muda uliowekwa kisheria kwa vyama vyenye nia ya kushirikiana kuingia mkataba wa kisheria umeshapita hivyo hakuna ushirikiano utakaoruhusiwa kwa sasa.

======

MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA: VYAMA VINAVYOTAKA KUUNGANA, VIMESHACHEWA

Vyama vya Siasa ambavyo vinatarajia kushirikiana wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu bila kufuata Sheria ya Vyama vya Siasa kama ilivyoainishwa kwenye Kifungu Na.11 (a) cha Sheria hiyo vitakuwa vimevunja sheria.

Onyo hilo limetolewa jijini Dodoma na Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, wakati alipofanya mahojiano kuhusu msimamo wa ofisi yake kwenye suala la ushirikiano wa vyama vya siasa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Nyahoza amesema kuwa ushirikiano wa vyama hivyo umeratibiwa vizuri kisheria ambapo vyama vinapohitaji kushirikiana vinapaswa kutumia vikao halali vya chama badala ya utashi wa mtu binafsi. Msajili Msaidizi Nyahoza ameongeza kuwa baada ya vikao halali kupitisha azimio la kufanya ushirikiano vyama husika vinapaswa kuwasilisha mkataba wa ushirikiano Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa miezi mitatu kabla ya mchakato wa uchaguzi kuanza.

“Vyama havijakatazwa kushirikiana bali vimewekewa utaratibu ili Tume ya Uchaguzi pamoja na taasisi zote zinazohusika na uchaguzi ziweze kujiandaa vizuri na kuimarisha ulinzi hasa wakati wa kampeni pamoja na kuvisaidia vyama vingine kuelewa wanashindana na vyama vya aina gani” alisema Nyahoza.

Kuhusu ushirikiano wa vyama vya siasa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2020 Msajili Msaidizi Nyahoza ameelezea kuwa mpaka sasa ofisi yake haijapokea mkataba wa makubaliano ya ushirikiano kutoka kwa chama chochote cha siasa hivyo kwa mujibu wa sheria vyama ambavyo vina nia ya kushirikiana vimeshachelewa.

Aidha, Msajili Msaidizi Nyahoza amesema hadi sasa vyama vyenye usajili wa kudumu ni 19 na chama kimoja kina usajili wa muda na maombi ya vyama 16 bado yanafanyiwa upembuzi.

1600846787994.png

Maendeleo hayana vyama!
 
Naibu wa msajili wa vyama vya siasa Dr Nyahoza amesema vyama vya siasa vinavyojipanga kushirikiana vimeshachelewa.

Nyahoza amesema muda uliowekwa kisheria kwa vyama vyenye nia ya kushirikiana kuingia mkataba wa kisheria umeshapita hivyo hakuna ushirikiano utakaoruhusiwa kwa sasa...

..mbona hajazuia ushirikiano wa TLP na CCM.

..tena Nyahoza alikuwepo siku Mzee Mrema alipotangaza chama chake kushirikiana na CCM.
 
Naibu wa msajili wa vyama vya siasa Dkt. Nyahoza amesema vyama vya siasa vinavyojipanga kushirikiana vimeshachelewa...
Mbona hii simple sana

Mfano Mimi SYOLOSU kama mgombea wa CCK kwenye kampeni zangu nikiwa nawambia wananchi kurazangu wampe TAL
 
Mimi nilimsikikiza Benard Membe vizuri kabisa kwamba wamefata sheria zote ila watashirikiana kirafiki maana ukija kwenye sheria kila mgombea yupo kwenye karatasi ila wanachama watapewa uamuzi wa kuchagua mgombea mmoja mwenye nguvu na sheria inahusu document siyo maneno cause kila mtu anachama chake na kafata stage zote za kugombea.
 
Kungekuwa na somo la SIASA ningekuwa nakuwa wa mwisho kila mhula!
 
Ilikuwa ndani ya muda wa kisheria!
Sheria inatamka vyama vinapaswa kufanya hivyo at least mwaka mmoja kabla ya uchaguzi. Sasa Augustino Mrema (TLP) alifanya hayo lini? Maana Mrema alitangaza hayo mwezi May mwaka huu.

Na ushirikiano huo unapaswa uridhiwe na CCM pia kwa vikao. CCM waliliridhia hilo lini? Yaani CCM walidhie hilo halafu Pole Pole na Bashiru wakae kimya! Thubutu.

Mwisho kabisa maridhiano hayo yanapaswa kupelekwa kwa msajili ili yaidhinishwe. Na msajili amesema wazi kabisa kuwa Hakuna vyama vilivyofanya mpaka leo hii.

Yote kwa yote, ushirikiano ni dhamira, na huwezi kuilazimisha sheria ipime dhamira.
 
Back
Top Bottom