Ofisi ya Rais – TAMISEMI Special Thread: Karibu tukuhudumie, tupe Maoni, Maswali, Mapendekezo na Malalamiko

Nataka kukutana ana kwa ana na katibu mkuu ama kiongozi anayepokea malalamiko ya wananchi, nafanyaje?
 
Hivi mnafahamu kuwa mishahara ya walimu wa wilaya ya chamwino inachezewa na watu wanavyotaka kuna walimu wanafanyakazi bila mishahara muda mrefu sana wapo wa miezi 10,7 ,1 pia wapo wanao zuwia mala umerudi ila hazina inasoma mshahara umetoka kuna uwizi na uonevu wa kiwango cha juu kabisa sasa fanyeni uchunguzi Kwa kufanya vikao na walimu bila viongozi au tafuteni njia watoe maoni yao kwenye sanduku la siri wapo wengi kuna viongozi chamwino wanakula mishahara ya wenzao tena wanagawana sasa tataona na hili kama mutafatilia
 
Mkuu mimi nimewahi kufanya kazi wilaya ya chamwino ila nilikuwa upande wa upande tofauti tatizo laa walimu wa chamwino hasa wa shule ya msingi ni mkuu wao wa idara ya elimu msingi anaitwa zainabu kishegwe huyu ni mke wa meya wa Jiji la Dodoma kwahiyo hao unaowapa maoni yako hawatawasaidia lolote hao walimu labda wafundishe ndumba wamloge huyo afisa elimu awe kichaa au afe na zaidi ameungana na tume ya TSC chamwino hivyo walimu watasagika sana niamin nasisitiza kishegwe ni mke wa meya wajiji kupia CCM elewa neno CCM
 
Mkuu kufa c mwiko mimi mwenyewe nipo upande wa upande najua kila kitu ndiyo maana nimewalengesha na subili wasifanyie kazi maoni yangu maana mtandao wao nu mrefu hadi wizarani msalimie barafu
 
Pole sana kwa changamoto hii tafadhali naomba utume raarifa za kutosha ili tuweze kufuatilia suala hili
Nashukuru sana kwa majibu yenu, naomba msaada kuhusu Uhamisho...

Mtumishi amefuata taratibu zote za uhamisho na akahamia katika kituo kipya cha kazi lakini hajahamishwa katika mfumo (Mshahara haujahama na inasoma vote ya kule alikotoka) ila kwa wengine umehama vizuri...naomba unisaidie katika hili

Nawasilisha.
 
Issue ya Ngorongoro

Mlifanga tadhimini vizri

Au mlikurukupa

Pili kama nyinyi mlitoa tangazo lenu

Mna mmamlaka gani ya kisheria la kufuta vijiji

Mbona kama mnajitekenya na hamna

Muondoe ninyi mrudishe ninyi.

Kwanini waziri na secretariat ya wizara isijiuzulu kwa kugombanisha serikani na wananch

Majibu tafadhali.
 
Natoaje malalamiko kwenu ikiwa Mkurugenzi wangu na subordinates wake hawanisikilizi na wapekula stahiki zangu?
 
Mkoa wa Morogoro ni mkubwa sana mnaonaje mkafanya mchakato wa wakuugawa huu mkoa kwa haraka zaidi ili kuwasogezea huduma za kijamii wananchi wa maeneo hayo kwa wepesi.
 
Jamaa anajibu wanapojisikia
Hebu wadau humu achaneni naye ana waenjoy tu 😄

Ova
 
Ninyi TAMISEMI ni Kwanini Watu wakiwatumia Message kwa PM hamjibu?
 
Mbona tovuti za Halmashauri nyingi ni dormant Hazina Taarifa current?

Pili mbona Halmashauri zingine zinatoa mwenendo wa makusanyo Yao ila zingine hakuna hata kidogo?

Je taarifa hizo ni za watu wa Halmashauri au Public?👇👇

View: https://www.instagram.com/p/DABtOcotNP-/?igsh=MTVnMHdyYmptZnA2Mg==
 
Ukiwasikiliza kina Mchengerwa wanavyojisemesha kuhusu Tamisemi unaweza dhani Kila kitu kiko.sawa wakati kiuhalisia hakuna response yeyote wanatoa
 
Watumishi tulioomba uhamisho kwa njia ya mfumo na status inasoma TAMISEMI Nini kinaendelea miezi minne hakuna kinachoendelea naomba mtujuze,uhamisho mtatoa lini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…