Oktoba 29 imetuonyesha namna Uraia pacha unavyohitaji mjadala zaidi

Oktoba 29 imetuonyesha namna Uraia pacha unavyohitaji mjadala zaidi

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,154
Reaction score
17,491
Kuna watanzania wenzetu wakifanikiwa kwenda kuishi ulaya na marekani wanajifanya kuusahau utanzania wao. Wanawaona watanzania walioko Tanzania kama washamba, wajinga, wasiojua kutukana na kubeza viongozi kama wazungu wanavyofanya. Ghafla wanatamani Tanzania iwe na utamaduni, siasa na uhuru kama wa wazungu.

Baadhi ya diaspora wanawachochea vijana watukane, wachome, waharibu na kupindua serikali. Wanafadhili vurugu na uvunjifu wa amani na utulivu nchini. Wanafadhili uchafuzi wa nchi yao kwenye vyombo vya habari vya Magharibi kama CNN, BBC, DW na vingine kwakuwa wana uwezo wa kuchangishana na kulipia uchafuzi huo.

Walifanya kila kitu ili nchi ikose misaada na mikopo, huku wakijua baadhi ya chanjo za watoto na dawa zinapatikana nchini kwa misaada.

Wanawapa matumaini hewa vijana wasiojua kuwa ulaya na marekani hakuna shida na kero hata moja, ni amani tu, asali, tende na maziwa.

Sijawasikia diaspora wakilaani vurugu za oct29 zilizowakata vidole watanzania na kuchoma miundombinu ya umma na watu binafsi.

Je, Tanzania tunahitaji uraia pacha?
 
Ni Diaspora yupi aliye wachochea vijana wachome na kupindua nchi.Tupe mfano hair na source yako.
Mwana Diaspora gani aliyesema Ulaya na Marekani hakuna shida wala kero.
Tupe mifano michache na rejea nasi tukaone.
Bet huwezi unaandika hekaya za Abunuwasi tuu tunachojua walikuwa wanawaambia watu wadai katiba mpya na chaguzi za huru na haki.
Wanapinga mauaji na utekaji ya yanayotekelezwa na watu wanaoitwa wasiojulikana.
Hayo ya kupindua nchi ni yako na Chande.
 
Ni Diaspora yupi aliye wachochea vijana wachome na kupindua nchi.Tupe mfano hair na source yako.
1791915222535.png


dayaspora kutoka kenya, alikua anamaanisha nini?
 
Umeukana utanzania unataka nini tena? Endelea kuwa mzungu mweusi, kula mema ya wazungu tuache tuendeleze nchi yetu kivyetu vyetu.
 
Are you sure?
This is exactly the kind of language and attitude I am talking about diaspora. Most of them are stupid.
Don't project your uchawa onto the diaspora. The irony of a real-life chawa calling them stupid when they actually work for their own money, while you're busy sucking up to people and begging for leftovers just to survive.
 
Wakenya hao sio ?
Hadi mmoja wao akaamua kuingia na Bomu la M13 multiple Bang.

Kamsikilize Mzee Mohamed Said anakwambia miaka yote mmeajwa na Hila hamjawahi kushinda kwa haki.
Mzee Mohamed Said hampendi rasi kwasababu rais ni muislamu na katoka Zanzibar hana tofauti na Kitima 😆😆😆😆
 
Waliofanya vurugu walikuwa Dayaspora kulingana na kauli zenu za kugeuka geuka.
DIaspora walichangia pesa za kulipia uhalifu, kuichafua nchi kwenye vyombo vya habari vya Magharibi na kwenye jumuiya za kimataifa. They had access to them.
 
Mzee Mohamed Said hampendi rasi kwasababu rais ni muislamu na katoka Zanzibar hana tofauti na Kitima 😆😆😆😆
Ina maana hata alipoongelea kuhusu chaguzi huko visiwani napo alikuwa hampendi nani ?

Mzee wetu ndugu katika imani huwa hamtengi bhana

Je alichukia awamu zote ?
 
Mzee Mohamed Said hampendi rasi kwasababu rais ni muislamu na katoka Zanzibar hana tofauti na Kitima 😆😆😆😆
Ina maana hata alipoongelea kuhusu chaguzi huko visiwani napo alikuwa hampendi nani ?

Mzee wetu ndugu katika imani huwa hamtengi bhana

Je alichukia wa awamu zote ?
 
Back
Top Bottom