Ole Sabaya afikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi na kufunguliwa kesi mpya. Amkataa Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU

kijana bado anabananishwa tu, aisee !!
 
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kufunguliwa mashitaka mengine yanayomkabili, leo Jumatano Juni Mosi, 2022

Sabaya amefikishwa Mahakamani hapo Sa 11:40 Asubuhi.

===========================

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya amemkataa Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Tumaniel Kweka kwa kuwa anatokea Wilaya ya Hai.

Aliwasilisha hoja hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Salome Mshasha, Sabaya alisema hana imani na mwendesha mashitaka huyo kwa kuwa anatokea katika wilaya hiyo na kwamba ni mtu aliyedai ni wa visasi na anatumika kisiasa.

Sabaya na washtakiwa wenzake wanne wanaokabiliwa na mashitaka saba ambapo alienda mbali na kumuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati kesi hiyo.

Mbali na hoja hiyo lakini kulijitokeza hoja nyingine kupitia kwa wakili Hellen Mahuna, aliyedai washitakiwa hao hawakupelekwa mahakamani hapo kwa kufuata taratibu za kisheria na kwamba mawakili wao hawakupewa taarifa.

Kutokana na malumbano hayo, Hakimu Mshasha ameahirisha kesi hiyo kwa muda wa dakika 10 hadi 15 ili kupitia hoja hizo ili kutoa uamuzi mdogo.

--UPDATES--
Watamfungulia kesi huyu Sabaya nyingi tu na kila sehemu. Tungoje na yule aliyeko Canada naye amfungulie kesi Sabaya kabla na wale wa Ubelgiji na Marekani hawajamfungulia kesi, ukiachilia mbali hawa wa hapa DAR-ES-SALAAM! Aaaaaah!
 
Kwa kweli ile kesi ya kwanza Sabaya hakutakiwa kuachwa huru.
 
jamani hii serikali ya samia imu achie huyo kijana
 
Mh.aingilie kati kumnusuru huyu kijana kwenye hili sakata kuna mkono wa mtu hapa sio bure na bila shaka ni yule aliyetoka majuzi.
Kila mtu ata lipwa kwa mujibu wa ujira wake. Huyu alidhani dunia ni yake. Ati hamtaki mwendesha mashtaka kwa vile ana toka Hai.. Vichekesho hivyo... Yaani huyu ndie mzuri kwa vile alikuwa na wilaya moja. Anajua upumbavu wooote alio tenda.
 
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kufunguliwa mashitaka mengine yanayomkabili, leo Jumatano Juni Mosi, 2022

Sabaya amefikishwa Mahakamani hapo Sa 11:40 Asubuhi.

===========================

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya amemkataa Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Tumaniel Kweka kwa kuwa anatokea Wilaya ya Hai.

Aliwasilisha hoja hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Salome Mshasha, Sabaya alisema hana imani na mwendesha mashitaka huyo kwa kuwa anatokea katika wilaya hiyo na kwamba ni mtu aliyedai ni wa visasi na anatumika kisiasa.

Sabaya na washtakiwa wenzake wanne wanaokabiliwa na mashitaka saba ambapo alienda mbali na kumuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati kesi hiyo.

Mbali na hoja hiyo lakini kulijitokeza hoja nyingine kupitia kwa wakili Hellen Mahuna, aliyedai washitakiwa hao hawakupelekwa mahakamani hapo kwa kufuata taratibu za kisheria na kwamba mawakili wao hawakupewa taarifa.

Kutokana na malumbano hayo, Hakimu Mshasha ameahirisha kesi hiyo kwa muda wa dakika 10 hadi 15 ili kupitia hoja hizo ili kutoa uamuzi mdogo.

--UPDATES--
Huyu Sabaya anatakiwa akutane na yule mwamba wa Mwanza, Saidi Oswaya
 
Yeye kama hamtaki mwendesha mashtaka wa Jamhuri, afanye mgomo wa kwenda mahakamani kusikiliza kesi dhidi yake. Akae nyumbani anywe bia halafu alale. Ngoma ipigwe upande mmoja "EX PARTE".

Ndio atajua kwanini dunia ya mviringo!
Hivi kisheria mwendesha mashtaka anaweza kukataliwa na mtuhumiwa?
 
Kadri wanavyomuandama na ndivyo wanavyompaisha kwa siku zijazo!
Acha kujipa matumaini ya kijinga,hakuna anayemwandama zaidi ya kulipa maovu aliyoyafanya,na apaishwe ili aende wapi??[emoji2][emoji2]huyu hata akisamehewa leo atakuwa hana jipya lolote mtaani
 
Back
Top Bottom