Mkuu wa ulinzi na usalama wa wilaya akamate siraha na kufanya uvamizi usiku ni tuhuma kubwa sana. Hivyo mpaka anamfikisha mahakamani basi ushahidi umekamilika.
Achana na unyag'anyi wa kutumia siraha, uhujumu uchumi au kutesa na kupiga watu na utakatishaji pesa ni mashitaka ambayo hayana dhamana.
Lakini kwa kiongozi ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama kufanya makosa makubwa kama haya basi lazima Ocd, Oc-Cid, Dso afahamu anafanya uhalifu. Kama hawafahamu basi ni uzembe. Lakini kama walifahamu kwa miaka mitatu walikuwa wapi kumkamatisha? Watu watasema alilindwa!
Ok, ni mhalifu na anahatia, upelelezi umekamilika. Kwa nini akae rumande? Ilitakiwa Jumatatu asomewe maelezo ya awali, kesi ianze kusikilizwa na apate haki yake.