Ole Sabaya asomewa Mashtaka Sita (6) kwa Uovu aliotenda Hai. Aenda Rumande hadi Juni 18

Ole Sabaya asomewa Mashtaka Sita (6) kwa Uovu aliotenda Hai. Aenda Rumande hadi Juni 18

Haya halafu mseme Magufuri alikuwa mzalendo,tuliibiwa sana kipindi cha Magufuri,Tulidhulumiwa sana kipindi chake na kunyanyaswa sana utafikiri Tanzania siyo nchi yetu kwa kukumbatia vibaka kama Ole Sabaya na Makonda.
... jambazi lililokuwa limepewa cheo na kulindwa kwa kila hali na mamlaka ya uteuzi! Shame on them all!
Wapumbav tu ndio wanasema jiwe alikuwa mtu
 
Mwigulu Nchemba na Kinana wana semaje?
Maana ndio walimpigia kifua kwa mwenda zake hadi akaupata uDc wa ujambazi na kufutiwa kesi ya kugushi kitambulisho cha Tiss?
Ati ni hongera kwa kazi maalum aliyo fanya kuisambaratisha CHADEMA. Mungu ni Mwema sana.
Aibu kwao.
 
Mwendazake aliwapa Sana Vijana nafasi ya Uongozi, bahati mbaya walikosa Mentor mzuri kuwafunza ethics za Utumishi na Uongozi wa Umma kwa ujumla labda kwa kuwa aliyewateua hakujali rule of law.

Hili liwe funzo kwa Vijana wote watakaoaminiwa na kupewa nafasi za uongozi, wawe wanatenda kwa kufata sheria na taratibu za Nchi.

Wao kama ni gali, linasoma Zero kilomita, hivyo wanasafari ndefu kulitumikia Taifa.

Wanaowateua Wamejiwekea Kinga ya Kutoshtakiwa, wao hawana.

Tafadhali Makinikeni
Bojana wazuri, wenye maadili na busara wapo lakini bahati mbaya marehemu alipendelea zaidi kuwateua waovu kama yeye kuliko kuwateua watu wema.

"Wewe nimekuteua kwa sababu ni kichaa kama mimi" - Hayati Magufuli.
 
Dogo mimi ni mtu mwenye msimamo. Unaposema mimi bingwa wa kusifia madhalilu unakosea
Ukiambiwa uthibishe kwa ushahidi kihusu dhalimu utaweza?

Kama Sabaya ana makosa nini kulemba? Kwa nini msianze kusikiliza kesi?
Hebu tulia ww.
 
Duuh kwa makosa hayo sabaya hachomoki aisee. Kikubwa aombe Mungu adhabu ipunguzwe kutoka kunyongwa hadi kufa mpaka kifungo cha maisha.

Amna kitu huwa nagwaya kama makosa ya ivo ukishtakiwa na jamhuri aisee kuchomoka huwa ni ngumu labda mkulu atie neno. Hapo bado yale ya kubaka na zaidi kina mama 40 ni mashahidi daah uyu jamaa sijui...
 
Kwa kuwa makosa hayo hayana dhamana watuhumiwa hao walipelekwa mahabusu Gereza Kuu la Kisongo na kesi hiyo kuahirishwa hadi Juni 18, 2021.

June 18 mbona karibu sana? Huyu ni Jambazi hakuna plea-bargain na DPP.....Makosa ya kuendesha genge la uhalifu,ujambazi,ubakaji hauwezi kukaa mezani na DPP,

Bado Bashite.
 
Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai Ole ngai Sabaya leo tar. 04.05 2021 amefikishwa mahakani akiwa na wenzake watano.

Sabaya peke yake amesomewa mashitaka sita likiwemo la Uhujumu uchumi na utakatishaji fedha pamoja na unyang'anyi kwa kutumia silaha.

Kesi imeahirishwa mpaka June 18 2021 na watuhumiwa wote wamerudishwa rumande kwani makosa hayo hayana dhamana.

Chanzo cha habari: Azam
View attachment 1808137
Karma is a bitch let it f. U. C. K him
 
JPM kwa kuyajua yote hayo, akaamua kuwakomesha wachaga kwa kuwapelekea jambazi!!!!!! kweli jamaa aliwachukia sana.
Naam, Sabaya alipata uteuzi akiwa na kesi ya jinai mahakamani! Hivyo aliteuliwa kwenda kufanya kazi maalum chafu ambayo ni mtu wa aina yake pekee anaweza kufanya. Tuhuma za unyang'anyi zilitolewa hadharani mbele ya camera lakini Sabaya hakuguswa!
 
Karibia yote 6 ni mazito
Mkuu sio karibia ni yote ni mazito aisee. Rushwa, utakatishaji fedha, kuongoza genge la uharifu, duuh kuna makosa mengine ukisingiziwa tu kuchomoka ni kwa mbinde sasa huyu ndgu kafanya kabisaa 😂😂
 
Akae ndani miaka 6 hadi ushahidi kukamilika kama walivyowatendea wenzao
 
Aliyekuwa mkuu DC wa Hai amesomea mashaka yake sita UHUJUMU UCHUMI UJAMBAZI KWA SILAHA KUTAKATISHA FEDHA NK AMEKWENDA RUMANDE MPAKA TAREHE 18/6/2021

View attachment 1808139
View attachment 1808140
View attachment 1808141

=======

Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya (34) na walinzi wake watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha wakikabiliwa na makosa mbalimbali likiwemo la uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na kupokea rushwa.

Sabaya ambaye alisimamishwa na Rais Samia Suluhu Hassan Mei 13, 2021 kupisha uchunguzi alifikishwa mahakamani hapo akiwa amefungwa pingu na baada ya wote kushuka kwenye magari ya polisi, walitakiwa kuchuchumaa na kisha kupelekwa katika chumba maalum na baadaye kuingizwa mahakamani.

Waendesha mashtaka wa Serikali, Tumaini Kweka, Abdallah Chaula na Tresla Garvas mbele ya Hakimu Mfawidhi, Martha Mahumbuga na Hakimu Mkazi Mkuu, Salome Mshasha wamesema Sabaya na wenzake walitenda makosa hayo Januari 20 na Februari 9, 2021.

Kweka amesema Sabaya na wenzake watano anatuhumiwa kwa makosa ya kuunda genge la uhalifu, uhujumu uchumi, kujipatia fedha kwa njia ya rushwa na utakatishaji fedha ambapo Sabaya alijipatia Sh90 milioni kutoka kwa mfanyabiashara, Francis Mroso mkazi wa kwa Mromboo ambaye alikuwa anatuhumiwa kwa makosa ya ukwepaji kodi ili amsaidie jambo ambalo ni makosa.

Pia, Sabaya na walinzi wake wawili, Sylivester Nyengu (26) maarufu kicheche na Daniel Mbura (38) wanakabiliwa na makosa mawili ya ujambazi wa kutumia silaha wakidaiwa kuyatenda Februari 9, 2021.

Wanadaiwa walimfunga pingu na kumpiga Bakari Msangi ambaye ni diwani wa CCM kata ya Sombetin na kumuibia Sh390,000 na pia katika eneo la Bondeni jijini Arusha wakitumia silaha, Sabaya na walinzi hao wanatuhumiwa kumpiga, kumtishia silaha na kumpora Ramadhani Ayoub simu na Sh35,000.

Kwa kuwa makosa hayo hayana dhamana watuhumiwa hao walipelekwa mahabusu Gereza Kuu la Kisongo na kesi hiyo kuahirishwa hadi Juni 18, 2021.
Thanks serikali ,Takukuru, na washirika wote katika zoezi zima, KWA kulikamata jambazi sugu,
Sasa MACKONDA NA WENGINE WAFYATULIWE
 
Back
Top Bottom