Ole Sabaya asomewa Mashtaka Sita (6) kwa Uovu aliotenda Hai. Aenda Rumande hadi Juni 18

Kwakuwa kituo ninachofuata ni kwako ama kwa sababu gani.
nilikuwa nasikiliza wimbo wa zamani sana wa 2Pac "changes"
anasema;

"let's change the way we eat, let's change the way we live, and let's change the way we treat each other".....................things 'll never be the same"

somo;
tujifunze pia kusamehana ili kuondoa chuki na visasi kuendelea.
 
Yaani mitandao ni hatari sana. Hasa hii ambayo tunatumia majina bandia, mambo mengi ni fake na ya kufikirika...ogopa sana. Usishangae jamaa akatoka akiwa ameoshwa safi.
Kuna wanaotamani atoke akiwa safi, siwacheki! Hata Mimi nilitamani Simba iwapige Amakhosi 5, zikaishia 3 tu!
 
Dah,kwakweli dunia duara yaani sabaya ambaye alikuwa anagegeda kila siku tena pisi kali(yaani akikutamani ndo hivo tena) leo hiii anaweza kaaa miezi hajagegeda(hapa akizengua yeye ndo atagegedwa)inauma sanaa
 
Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai Ole ngai Sabaya leo tar. 04.06 2021 amefikishwa mahakani akiwa na wenzake watano.

Sabaya peke yake amesomewa mashitaka sita likiwemo la Uhujumu uchumi na utakatishaji fedha pamoja na unyang'anyi kwa kutumia silaha.

Kesi imeahirishwa mpaka June 18 2021 na watuhumiwa wote wamerudishwa rumande kwani makosa hayo hayana dhamana.

Chanzo cha habari: Azam
View attachment 1808137
Ikiwapendeza wale aolewe usiku huu huu wa leo na wale watemi wa selo!!
 
Aliyekuwa mkuu DC wa Hai amesomea mashaka yake sita UHUJUMU UCHUMI UJAMBAZI KWA SILAHA KUTAKATISHA FEDHA NK AMEKWENDA RUMANDE MPAKA TAREHE 18/6/2021

View attachment 1808139
View attachment 1808140
View attachment 1808141

=======

Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya (34) na walinzi wake watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha wakikabiliwa na makosa mbalimbali likiwemo la uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na kupokea rushwa.

Sabaya ambaye alisimamishwa na Rais Samia Suluhu Hassan Mei 13, 2021 kupisha uchunguzi alifikishwa mahakamani hapo akiwa amefungwa pingu na baada ya wote kushuka kwenye magari ya polisi, walitakiwa kuchuchumaa na kisha kupelekwa katika chumba maalum na baadaye kuingizwa mahakamani.

Waendesha mashtaka wa Serikali, Tumaini Kweka, Abdallah Chaula na Tresla Garvas mbele ya Hakimu Mfawidhi, Martha Mahumbuga na Hakimu Mkazi Mkuu, Salome Mshasha wamesema Sabaya na wenzake walitenda makosa hayo Januari 20 na Februari 9, 2021.

Kweka amesema Sabaya na wenzake watano anatuhumiwa kwa makosa ya kuunda genge la uhalifu, uhujumu uchumi, kujipatia fedha kwa njia ya rushwa na utakatishaji fedha ambapo Sabaya alijipatia Sh90 milioni kutoka kwa mfanyabiashara, Francis Mroso mkazi wa kwa Mromboo ambaye alikuwa anatuhumiwa kwa makosa ya ukwepaji kodi ili amsaidie jambo ambalo ni makosa.

Pia, Sabaya na walinzi wake wawili, Sylivester Nyengu (26) maarufu kicheche na Daniel Mbura (38) wanakabiliwa na makosa mawili ya ujambazi wa kutumia silaha wakidaiwa kuyatenda Februari 9, 2021.

Wanadaiwa walimfunga pingu na kumpiga Bakari Msangi ambaye ni diwani wa CCM kata ya Sombetin na kumuibia Sh390,000 na pia katika eneo la Bondeni jijini Arusha wakitumia silaha, Sabaya na walinzi hao wanatuhumiwa kumpiga, kumtishia silaha na kumpora Ramadhani Ayoub simu na Sh35,000.

Kwa kuwa makosa hayo hayana dhamana watuhumiwa hao walipelekwa mahabusu Gereza Kuu la Kisongo na kesi hiyo kuahirishwa hadi Juni 18, 2021.
Kweli mkuu wa Wilaya anaweza kumpora mtu shilingi 35,000/= tena kwa kutumia silaha? Huu ni udhalilishaji tu Sabaya anafanyiwa. Mama Samia awe makini na huu ushabiki wa kipumbavu
 
Hayo mashitaka yameandikwa kwa lugha ya kifaransa kwani bado lugha yetu ya kiswahili haitumiki?
au ndio kiswahili kimeshapuuzwa?
kwa nini Lugha ya kiswahili inadharauliwa na waswahili wwnyewe?
hivi kweli viongozi wetu wa sasa wanayo nia ya kukitumia kiswahili au ndio tuendelee na kifaransa tu kama zamani?
maaana sielewi kabisa kilicho andikwa.
 
Bojana wazuri, wenye maadili na busara wapo lakini bahati mbaya marehemu alipendelea zaidi kuwateua waovu kama yeye kuliko kuwateua watu wema.

"Wewe nimekuteua kwa sababu ni kichaa kama mimi" - Hayati Magufuli.
Wameingizwa kwenye mtego nao wameingia kichwa kichwa, wenzao wanakinga ili hali wao hawana.

Mbona mwenzao Anthony Mtaka ameonekana kufata sheria, nadhani akina Ally Happi wanacha kujifunza.
 
Hayo mashitaka yameandikwa kwa lugha ya kifaransa kwani bado lugha yetu ya kiswahili haitumiki?
au ndio kiswahili kimeshapuuzwa?
kwa nini Lugha ya kiswahili inadharauliwa na waswahili wwnyewe?
hivi kweli viongozi wetu wa sasa wanayo nia ya kukitumia kiswahili au ndio tuendelee na kifaransa tu kama zamani?
maaana sielewi kabisa kilicho andikwa.
Wakati wengine wanaangalia uhalifu wa sabaya wewe unaangalia matumizi ya kiswahili.[emoji17]
images%20(20).jpg
 
Huyu dwanzi amenyanyasa sana raia
 
Hizi comment zinajieleza namna watanzania walivyo magay japo wanajifanya kuukataa ugay
 
Back
Top Bottom