Ole Sabaya asomewa Mashtaka Sita (6) kwa Uovu aliotenda Hai. Aenda Rumande hadi Juni 18

Ole Sabaya asomewa Mashtaka Sita (6) kwa Uovu aliotenda Hai. Aenda Rumande hadi Juni 18

Aisee! Naomba uende x2 uende ukamweleze baba yangu,uende ukamweleze mama.....malizia mwenyewe nyimbo ya wajelajela original
Nalog off
 
Mwendazake aliwapa Sana Vijana nafasi ya Uongozi, bahati mbaya walikosa Mentor mzuri kuwafunza ethics za Utumishi na Uongozi wa Umma kwa ujumla labda kwa kuwa aliyewateua hakujali rule of law.

Hili liwe funzo kwa Vijana wote watakaoaminiwa na kupewa nafasi za uongozi, wawe wanatenda kwa kufata sheria na taratibu za Nchi.

Wao kama ni gali, linasoma Zero kilomita, hivyo wanasafari ndefu kulitumikia Taifa.

Wanaowateua Wamejiwekea Kinga ya Kutoshtakiwa, wao hawana.

Tafadhali Makinikeni
shida ya Mwendazake alipenda kuwatesa wale waliokuwa na mtizamo tofauti na yeye na alitesa kwa kutumia hao aliowapa vyeo sasa wengine walijiongeza wakajua kuna kesho, wengine walijisahau wakatumia ubaya wa magu kujipatia vinono kwa kujipendekeza kwake kwa kuwatesa wabaya wake wakajua magu ni ka Mungu haondoki leo wala kesho na hata akiondoka wao wana kinga sasa Mungu alipofanya yake leo ndo wanaumbuka. Ni vizuri sana next time ccm wakaleta rais ambaye anavumilia kukosolewa kupingwa na mwenye utu pia maana kiongozi inabidi awe na ngozi ngumu. Kama wapo wanaompinga Munga na bado Mungu anawapa uhai na mali sembuse binadamu ndo atese, aue wakosoaji wake hapana ni machukizo mbele za Mungu.
 
Back
Top Bottom