Ole Sabaya: Hai iliendeshwa kihuni sana, mimi nimekuwa mwarobaini

Ole Sabaya: Hai iliendeshwa kihuni sana, mimi nimekuwa mwarobaini

Kwa Mujibu wamaelezo yaliyotelewa leo na DC wa Hai, Sabaya, 360 Clouds, hakika eneo hilo uwajibikaji ulikuwa duni sana .

Takwimu zinaonyesha ujambazi ulikithiri, mihadarati, wananchi wanyonge kuporwa mashamba, makusanyo hafifu ya kodi, uhaba wa vituo vya afya, miundombinu chakavu na mengine mengi ya hovyo.

Kwa maelezo yake ni kama ilikuwa zone fulani ya gangstar.

Kwakua hili kalisema hadharani mchana kweupee kwenye media ambayo inatazamwa na kusikilizwa na watanzania wengi ,ajitokeze mtanzania hadharani apingane nae kwa takwimu, maana bila kukanushwa madai yake ni dhahiri aliyekuwa mbunge anawajibika kwa lawama na uhalibifu wote uliotokea kwa jamii na serikali kwa ujumla, sababu mbunge ni sauti ya wananchi.
Wakati mwingine kukaa kimya ni hekima. Mfano muone manywele a.k.a EDO. Wote waliomtukana hawapo lakini yeye bado anadunda tu. Na atadunda sana sana. Hata alivyorudi nyumbani sijui kama aliwatukanaCDM kama hao wengine wanavyofanya. Binafsi sijasikia. CDM wasijibu wakae kimya tu historia inajieleza vizuri sana. 2015 Mbowe hakupiga kampeni kabisa jimboni kwake, alizunguka na aliyerudi nyumbani lakini alichaguliwa tu. Hizo za Ole S. ni siasa za kitoto. Nasubiri Mbowe adai fidia ya kuvunjiwa greenhouse zake. Sijui kwa nini anachelewa kudai.
 
Ni shule kongwe tu ndizo zilipewa peas kwa ajili ya ukarabati. Machame sec school. Lyamungo sec school. Hakuna cha hospital wala zahanati kituo cha afya.
Usizungumze kwenye Jamhuri ya JF kudaganya watu, sisi ni wakazi wa Hai, iliyo sema Sabaya hajakosea. Naanza kuamini tatizo na haya majibizano ni Mbowe kukosa ubunge.
 
Anatafuta coverage ya uteuzi wa mama.maana anajua hayumo kabisa.ko huo ujumbe anamtumia mama.ana akili huyu jamaa!kinachowanyima usingizi zaidi ni pale mama aliposema atateua hata wapinzani madamu ni wachapa kazi.what if mbowe akapewa u RC kilimanjaro.ccm tunajambia pua kusikia atateua bila kujali itikadi
 
Huyu mkuu wa wilaya Ni muhuni Sana, alipaswa kuwa jela Sio kwenye ofisi za umma...
 
Kwa Mujibu wamaelezo yaliyotelewa leo na DC wa Hai, Sabaya, 360 Clouds, hakika eneo hilo uwajibikaji ulikuwa duni sana .

Takwimu zinaonyesha ujambazi ulikithiri, mihadarati, wananchi wanyonge kuporwa mashamba, makusanyo hafifu ya kodi, uhaba wa vituo vya afya, miundombinu chakavu na mengine mengi ya hovyo.

Kwa maelezo yake ni kama ilikuwa zone fulani ya gangstar.

Kwakua hili kalisema hadharani mchana kweupee kwenye media ambayo inatazamwa na kusikilizwa na watanzania wengi ,ajitokeze mtanzania hadharani apingane nae kwa takwimu, maana bila kukanushwa madai yake ni dhahiri aliyekuwa mbunge anawajibika kwa lawama na uhalibifu wote uliotokea kwa jamii na serikali kwa ujumla, sababu mbunge ni sauti ya wananchi.
Unaelewa maana ya TAKWIMU? Hivi vitu alivyotaja ni MEASURABLE kwa hiyo alipaswa kueleza kwa QUANTITY na QUALITY (Idadi na Ubora).

Pili kwani jukumu la hayo anayosema ni la nani kutekeleza? Mbunge, Diwani, RC, DC, Waziri, Serikali Kuu? Bajeti ikoje kwenye allocation?

Kwa maelezo yake anaona kazi ya kujenga hayo ni ya MBOWE! Kazi ya ulinzi na usalama ni ya MBOWE! What a waste!
 
Hapa haumkomoi Mh. Mbowe ni unaitusi serikali ya CCM hapo Hai

Alichofanya Mh. Sabaya ni sawa na kusema CCM ilishindwa kusimamia utekelezwaji wa ilani yake hapo Hai.

Tukirudi kuangalia Hansad za bunge akiongea Mh. Mbowe juu ya hayo mambo Mkuu utapoteana.

Tufichie ujinga basi japo kidogo
 
Kwa Mujibu wamaelezo yaliyotelewa leo na DC wa Hai, Sabaya, 360 Clouds, hakika eneo hilo uwajibikaji ulikuwa duni sana...
Hivi Clouds wamefikia kiwango cha kuuza kipindi kwa Sabaya ili afanye kampeni za kuteuliwa tena kuwa DC, hizo pesa anatoa wapi za kulipia kipindi ...na kutoka kituo chake cha kazi kuja kufanya hizo propaganda.

Anasema Hai iliendeshwa kihuni ...yeye ni mbunge au RC au DC ...hivyo kama inaonekana Hai ilikuwa inaendeshwa kihuni ; anawalaumu wakuu wa wilaya waliotangulia au mbunge.

Wabunge siku hizi wanfanya kazi za wakuu wa wilaya.
 
Hivi Clouds wamefikia kiwango cha kuuza kipindi kwa Sabaya ili afanye kampeni za kuteuliwa tena kuwa DC , hizo pesa anatoa wapi za kulipia kipindi ...na kutoka kituo chake cha kazi kuja kufanya hizo propaganda..
Endeleeni kumtetea kuu la majambanoka
 
Huyu kijana asisahau anaongea na watu walioenda shule na werevu ambao wanajua kuwa hakuna Mbunge anayepewa pesa za kujenga barabara ...hivyo wakadanganye kwenye maeneo ambayo bado hawajaelimika .....wananchi wanajua ni na nani anajenga barabara ...na mbunge ni mwakilishi tu ....wananchi wanajua kuwa Mgao wa keki ya taifa unagawanywa toka mfuko mkuu kupitia kwenye wizara husika na kigezo kikubwa moja wapo ni demographic information za sensa ya watu na makazi ....ndio maana maeneo yenye watu wengi hupata mgao zaidi ..na pia kuna factor kama Shughuli za kiuchumi na rasilimali za Taifa [ndio maana kuna maeneo hakuna watu wengi lakini barabara inaenda kufungua miradi ya kiuchumi ]

KInachotokea ni kuwa kutokana na sera za kibaguzi za magufuli ....migawo ya pesa za Maji ., Barabara [tarura na baadhi Tanroad] , elimu na afya kwenye maeneo yanayokaliwa na wapinzani hasa kipengele cha bajeti ya maendeleo ilikuwa aidha hazipelekwi pesa zaidi ya mishahara, au pesa zinapelekwa kujenga maeneo mengine anayotaka au pesa hivo zilichukuliwa makusudi [hewa] ili tu kuwakomoa wananchi miradi isitekelezwe .......
Pamoja na maeneo yaliyopigia kura upinzani kunyimwa maendeleo makusudi ...bado haijasadia sana kwani kuna maeneo mengi tu nchini toka uhuru yamekua yakipigia kura ccm lakini nako pesa za maendeleo zimekua zikifujwa ...na hakuna kilichofanyika .....Wakati wa Kikwete ambako alikuwa akiacha pesa ziende kwa haki ...maeneo yaliyochagua upinzani kama Karatu na Kigoma yalipata maendeleo kwakua tu walihakikisha wanasimamia vizuri pesa hata kama ni kidogo na hii sana sana ilichangiwa na ubora wa madiwani asilimia kubwa ya upinzani kuwa na elimu wengi tu wakiwa na diploma ,shahada au wastaafu wasomi tofauti na kiwango cha elimu ya madiwani baadhi ya maeneo nchini ..mfano iliwahi kutokea madiwani wa Bagamoyo kupitisha nyaraka bila kujua ndani kuna ujenzi wa matundu ya vyoo kwa bei ya milioni 70 kwa tundu [ Bilioni 7 zilipotea ] ,Kishapu madiwani waliwahi kupitisha taarifa inayoonyesha wamejengewa barabara na ofisi za utawala kwa gharama ya bilioni 3 wakati hakuna kilichojengwa na pesa zote ziliingia na kutolewa na mkurugenzi wa wilaya huku viongozi wote waandamizi na kamati ya ulinzi na usalama akiwamo mbunge wakijua [japo ushahidi uliwatia hatiani mkurugenzi na meneja wa tawi la NMB ]...........Kiwango duni cha madiwani kimezorotesha sana usimamizi wa miradi huku chini .......
Ukitazama utagundua halmshauri nyingi zenye madiwani wasomi...inakuwa ngumu sana kwa watendaji kuwatapeli ....kama mikataba ya chief mangungo , kwa kutumia posho nono siku wakitaka kupitisha mabomu, chakula kizuiri na kufuatiwa na miadi ya kunywa pombe baada ya kikao ...huku wakiwa wamepewa makabrasha yanayowazidi uzito na kuwatia uvivu wa kusoma .....
 
Ulichokiandika wewe na alichokiongea sabaya ni kuonyesha tu ni jinsi gani taifa limetamalaki siasa zakishamba.Sana sana mnaidhalilisha tu serikali ya ccm iliyoongoza nchi toka uhuru.Huyo sabaya angekutana na waandishi wa habari wanaojielewa angepigwa maswali ya maana mawili tu angeweweseka sema ndo hivyo lengo lake lilikua kumchafua mbowe, akajisahau kua mbowe alikua mbunge tu na Hai ni sehemu ya jamhuri ya muungano wa Tanzania nchi ambayo iko chini ya chama cha mapinduzi,chama ambacho sabaya ni mwanachama na kiongozi ndani ya hiyo serikali.Kwahiyo mapungufu au umasikini wa Hai wakwanza kuwajibika ni serikali.Kauli kama zile zilitakiwa zitolewe na mtu anayetaka kugombea ubunge dhidi ya mbowe na sio kiongozi mtendaji anayeiwakilisha serikali.Kwa wenye akili tunawaona mbulula tu.
 
Nimemsikiliza katoa facts tupu tena kwa data ,hili limewakera sana wafuasi wa Mbowe,

Inatakiwa serikali ilinde hivi vipaji kwa nguvu nyingi sana
Mkuu wa wilaya, mkurugenzi, das waliokuwepo kabla watakuwa walikuwa wa ovyo Sana... Bila kumsahau mbunge wa sasa... Naye ni wa ovyo.. HONGERA SANA KAKA JAMBAWAZ SABAYA...
 
Kwa Mujibu wamaelezo yaliyotelewa leo na DC wa Hai, Sabaya, 360 Clouds, hakika eneo hilo uwajibikaji ulikuwa duni sana .

Takwimu zinaonyesha ujambazi ulikithiri, mihadarati, wananchi wanyonge kuporwa mashamba, makusanyo hafifu ya kodi, uhaba wa vituo vya afya, miundombinu chakavu na mengine mengi ya hovyo.

Kwa maelezo yake ni kama ilikuwa zone fulani ya gangstar.

Kwakuwa hili kalisema hadharani mchana kweupee kwenye media ambayo inatazamwa na kusikilizwa na Watanzania wengi ,ajitokeze Mtanzania hadharani apingane nae kwa takwimu, maana bila kukanushwa madai yake ni dhahiri aliyekuwa mbunge anawajibika kwa lawama na uhalibifu wote uliotokea kwa jamii na serikali kwa ujumla, sababu mbunge ni sauti ya wananchi.
Mpuuzi wewe, maanake Mbunge ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya?
 
Ulichokiandika wewe na alichokiongea sabaya ni kuonyesha tu ni jinsi gani taifa limetamalaki siasa zakishamba.Sana sana mnaidhalilisha tu serikali ya ccm iliyoongoza nchi toka uhuru.Huyo sabaya angekutana na waandishi wa habari wanaojielewa angepigwa maswali ya maana mawili tu angeweweseka sema ndo hivyo lengo lake lilikua kumchafua mbowe, akajisahau kua mbowe alikua mbunge tu na Hai ni sehemu ya jamhuri ya muungano wa Tanzania nchi ambayo iko chini ya chama cha mapinduzi,chama ambacho sabaya ni mwanachama na kiongozi ndani ya hiyo serikali.Kwahiyo mapungufu au umasikini wa Hai wakwanza kuwajibika ni serikali.Kauli kama zile zilitakiwa zitolewe na mtu anayetaka kugombea ubunge dhidi ya mbowe na sio kiongozi mtendaji anayeiwakilisha serikali.Kwa wenye akili tunawaona mbulula tu.
Right
 
Hivi mbunge ninserikali? Kwa ufinyu wako wa mawazo hata kazi za mbunge huzijui. Akili yako ni sawa na ya Sabaya.

Mbunge ana husikajena ujambazi, uvuta bangi, kuuza mihadharati?

Hii ni kuonyesha mnavyo idharaulisha serikali yenu na vyombo vya ulinzi na usalama.

Mbona hakiongelea kwenda kuvamia hoteli za watu usiku kutafuta wanawake?

Mbona haja zungumzia kuingia mabaa na kurusha huduma anazo tumia? Mbona haja zungumzia kufanya fujo disco na kupiga watu risasi?
Niwaambie kitu.

Mnazidi kuharibu. Acheni kujaribu kumpa kick Sabaya.
Mkuu wanajua wanachokifanya, ni mkakati maalum..wanajua kuna panga pangua ya wakuu wa wilaya inakuja... Bila kujiandaa Mapema inakula kwao..
 
Kwa Mujibu wamaelezo yaliyotelewa leo na DC wa Hai, Sabaya, 360 Clouds, hakika eneo hilo uwajibikaji ulikuwa duni sana .

Takwimu zinaonyesha ujambazi ulikithiri, mihadarati, wananchi wanyonge kuporwa mashamba, makusanyo hafifu ya kodi, uhaba wa vituo vya afya, miundombinu chakavu na mengine mengi ya hovyo.

Kwa maelezo yake ni kama ilikuwa zone fulani ya gangstar.

Kwakuwa hili kalisema hadharani mchana kweupee kwenye media ambayo inatazamwa na kusikilizwa na Watanzania wengi ,ajitokeze Mtanzania hadharani apingane nae kwa takwimu, maana bila kukanushwa madai yake ni dhahiri aliyekuwa mbunge anawajibika kwa lawama na uhalibifu wote uliotokea kwa jamii na serikali kwa ujumla, sababu mbunge ni sauti ya wananchi.
Maana yake ni kuwa wakuu wa wilaya waliomtangulia (Byakanwa, Antony Mtaka, novatus makunga na wengineo) walikuwa wahuni/wanaendesha wilaya kihuni? walikuwa wanapora mashamba ya wanyonge, wanauza mihadarati, walikuwa wanafadhili ujambazi na hawakuwa wanakusanya kodi?
 
Back
Top Bottom