Ombi kwa Rais Samia: Sheria Mpya ya Uchaguzi Bado ina Ubatili. Haki ya Kuchagua na Kuchaguliwa imeporwa! Irejeshwe kwa Mujibu wa Katiba!

Shida nchi imetekwa nyara na CCM wakisaidiwa na JWTZ, Polisi na TISS. As long as hao watu wanaona CCM haina shida hakuna mabadiliko yoyote.
Katika mazingira haya ni wendawazimu kuendelea kushiriki chaguzi za nchi hii. Inatakiwa wananchi wengi wapuuze kupiga kura, hapo tutakuwa na nguvu ya kudai chaguzi za haki. Kinyume na hapo kuendelea kushiriki chaguzi hizi ni kuzipa uhalali usiostahili.
 
Kama ni ombi kwani kuna ulazima kulikubali? Tukisema tudai Katiba MPYA yenye misingi mizuri hamtuelewi, Sasa haya maombi mpaka lini? Kila kitu Rais tunaomba, Rais tunaomba, Hivi Watanganyika tutaamka lini kwenye huu usingizi wa pono? Nchi imeachwa mikononi mwa mtu mmoja anatufanya avyotaka halafu tupo tu kama mazezeta. 🚮🚮🚮
 
Tatizo sheria nyingi zinazohusu siasa, chama Tawala lazma ziwe na manufaa kwa CCM
Uhuru wa kuchagua au kuchagulia lazima suala la mgombea binafsi lizingatiwe. Maana ni haki na uhuru wa mtu (awe mpiga kura au mgombea)
Nakumbuka comredi Mtikila alivyopambambania hili jambo
 

Maamuzi hayo ndio mtaji wa CCM, maana wale wanao susia kupiga kura kisasa madudu ya CCM wanapunguza idadi ya kura kwa wapinzani, sababu CCM wataenda na wataongeza idadi ya kura zao

cha msingi kuwepo na tume huru ya uchaguzi
 
Yaani haki ni hisani kwa watanzania na siyo sharti la kikatiba
Kwa Tanzania, haki ni hisani!, na it's very unfortunately hatuna upinzani wowote wa maana wa kudai haki au kuipigania. Angalia hapa nilichosema
View: https://youtu.be/A_YPEHtM9WM?si=3Cm92lS5twafkRko
Watanzania wanategemea kuhisaniwa haki zao kwa hisani ya Mkuu wa nchi.

Ndio maana alipopiga marufuku mikutano ya vyama, tuliuliza
View: https://youtu.be/Ta0URHvUlko?si=3vP9ZC99u3XU_Sy6
Mama aliporuhusu mikutano ya siasa, pia tumeuliza, Anayekuja pasi na hodi, huondoka pasi kuaga. Kuzuiwa bila kifungu, kuruhusu bila Kifungu. Ni hisani ya Rais Samia. Haki kuhisaniwa hadi lini?

Mimi mwenyewe najihesabu ni mtetezi huru wa haki, huu ubatili wa katiba nimeuzungumza sana.

View: https://youtu.be/3a4SjkV46JY?si=rS6X-ttZFwtlbcyy
View: https://youtu.be/PBpjDhH2XiA?si=y3wvuR5p0UBD03cn
View: https://youtu.be/lBC3xKODSvY?si=SNx0DquDv8knTt1p
P
 
Huwezi kusema hakuna upinzania na wakati Lisu na team yake kila siku wanashambulia na CCM wanafanya ziara ambazo hata wao hawajui wanafanya ajili ya nani
 
HBD Rais Samia!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…