Uchaguzi 2020 Ombi: Tume ya Uchaguzi tunataka mdahalo wa Wagombea Urais

Uchaguzi 2020 Ombi: Tume ya Uchaguzi tunataka mdahalo wa Wagombea Urais

Wakuu habari za jioni poleni kwa kutafuta na mihangaiko ya kutwa nzima. Mimi sina mengi ila nina imani humu kuna watumishi wa tume ya uchaguzi basi wafikishe salamu hizi, tunaomba mdahalo wa wagombea wote watakaoteuliwa kugombe Urais kuanzia, CCM, CHADEMA , ACT - Wazalendo nk ili tuwapime kwa hoja zao tuulize maswali yetu wakiwa pamoja kwenye ukumbi mmoja tupate mgombea ambaye ni cream ili wanachi tuchague Rais makini ambaye atatavusha kwenye umaskini tulionao na kuweka sera zinazotekelezeka kwa weledi na maarifa yaliyotukuka.

Nawasilisha.

View attachment 1527961

View attachment 1527962

View attachment 1527963

Ufanywe kwa kiingereza ili Bwana yule aume ulimi.
 
1597279395938.png

Wakuu habari za jioni poleni kwa kutafuta na mihangaiko ya kutwa nzima. Mimi sina mengi ila nina imani humu kuna watumishi wa tume ya uchaguzi basi wafikishe salamu hizi, tunaomba mdahalo wa wagombea wote watakaoteuliwa kugombe Urais kuanzia, CCM, CHADEMA , ACT - Wazalendo nk ili tuwapime kwa hoja zao tuulize maswali yetu wakiwa pamoja kwenye ukumbi mmoja tupate mgombea ambaye ni cream ili wanachi tuchague Rais makini ambaye atatavusha kwenye umaskini tulionao na kuweka sera zinazotekelezeka kwa weledi na maarifa yaliyotukuka.

Nawasilisha.

View attachment 1527961

View attachment 1527962

View attachment 1527963
 
Utakusaidia nini badala ya kufanya kazi zako uongeze kipato cha familia yako
 
Mdahalo utakyongezea niji hasa ktk maisha yako kama siyo ukuwadi wenzio wako kazini
 
Watanzania tulikuwa tunataka na bado tunamtaka mtu ambaye anatenda zaidi kuliko kuzungumza.Kati ya matendo na maneno matendo ya mtu ndo yanachukua nafasi kubwa kwa umma kufanya maamuzi juu ya kumkubali au kumkataa mgombea husika.Mdahalo unaweza kutupa muelekeo wa maamuzi kwa asilimia 10,zinazobaki zinategemea sana utendaji.Ila kwa utawala huu wa sasa unaomaliza awamu yake ya kwanza Wazaramo wanasema "ZILONGWA ZITENDWA" hivyo watanzania tunaotaka kupima mgombea kwa matokeo(ndo tuko wengi)tushajua uelekeo
 
Tume haijawahi kulazimisha uwepo wa mdaharo huru. Siasa za bongo zina ujinga mtupu ndani yake. 2015 ni Chadema waliokimbia mdaharo coz walijua mgombea wao hawezi kujieleza hata kwa dakika 10 tu, this time ndio mnajifanya mko moto na midaharo.
Kila chama kifanye kampeni kwa style yake
Kwaio hauwezi kutofautisha kati ya mdahalo na mdaharo?
 
2010 upinzani walitaka mdahalo,2015 Ukawa (CHADEMA,NCCR,CUF) na CCM walikukataa mdahalo,ACT walikubali (sijui kwa nini?),2020 wanataka tena mdahalo.Siasa za Tz hazina tofauti na komedi......walicho kikataa juzi wanakikubali leo,sasa unajiuliza kwa nini juzi walikataa.
Wewe huelewi chochote, sio siasa za Tanzania, ndio dunia ilivyo.

Lowass alivyokuja Chadema ccm waligeuza santuri na kusema ni fisadi, sasa amerejea nyumbani wako kimya.

That's politics guy, you will realize this when you come of age.
 
Ccm hawawezi kukubali mdahalo wowote ule.

Mdahalo wowote katika mazingira ya sasa itakuwa ni maangamizi makubwa kwa ccm na itaifanya tume ya uchaguzi iwe ktk mazingira magumu sana kuwabeba.
 
Upinzani ilani yenu ya uchaguzi imetoka?

Bring forward your election manifesto.

CCM inayo tayari ilani yake ya uchaguzi.

Waleteeni wananchi waichambue ilani yenu ya uchaguzi.

Acheni blahblah zisizo na tija.
Naitafuta ilani ya ccm, unaweza kuweka humu au link yake?
 
Tume haijawahi kulazimisha uwepo wa mdaharo huru. Siasa za bongo zina ujinga mtupu ndani yake. 2015 ni Chadema waliokimbia mdaharo coz walijua mgombea wao hawezi kujieleza hata kwa dakika 10 tu, this time ndio mnajifanya mko moto na midaharo.
Kila chama kifanye kampeni kwa style yake

Ni kwa sababu mgombea wenu hawezi kujieleza hata kwa dak 10?
 
Wewe huelewi chochote, sio siasa za Tanzania, ndio dunia ilivyo.

Lowass alivyokuja Chadema ccm waligeuza santuri na kusema ni fisadi, sasa amerejea nyumbani wako kimya.

That's politics guy, you will realize this when you come of age.
Nani walikuwa wa kwanza kumwita Lowasa fisadi mpaka wakajitamba ushahidi wanao,wakazunguka mikoa yote ya Tanzania wakimwita Lowasa fisadi kwa miaka zaidi ya mitano.

Baadaye wakayalamba matapishi yao na kuyala hatimae wakampigia kampeni NA NDIO MAANA WALIKATAA MDAHALO.Walitumia miaka zaidi ya mitano kumchafua wakatumia dk 5 kumsafisha,CCM waliongea walichoongea wao miaka mitano iliyopita.

Ila si shangai ukitaka kuwa ng'ombe wa mwanasiasa lazima uwe msaulifu,ila kwa sisi watu wazima hatusahau na ndio maana tunajiuliza kwa nini leo 2020 na si 2015.
 
Ndio maana nakwambia, That's politics, no permanent friends or permanent enemies but permanent interests. Kama huelewi ndio utaongea hivyo. Iko siku utaelewa tu when you come of age.
 
Ndio maana nakwambia, That's politics, no permanent friends or permanent enemies but permanent interests. Kama huelewi ndio utaongea hivyo. Iko siku utaelewa tu when you come of age.
Ndio maana kama ukiwa mtu mwenye akili,makini huwezi waelewa wanasiasa kwanza Waongo,Wanafiki,Wasahalifu.

Ila kama kilaza au bendera fuata upepo labda utawaelewa,HONGERA KWA KUWAELEWA wanasiasa,ila mimi siwahelewi sababu wengi HAWANA MISIMAMO NA HAWAJUI KUKISIMAMIA WAKICHOONGEA JUZI NA JANA (Vigeugeu).
 
Mdahalo utakuwepo, kama tu mgombea mmoja akiruhusiwa kuingia na jangili lenye silaha ya kivita, maana mgombea huyo husifika sana kwa kujibu hoja kwa risasi!
 
Nashauri tu kuwa mwaka huu kabla ya kuanza kuzunguka kufanya Kampeni kuwepo mdahalo kwa wagombea wakuu watatu.

Dr. John Pombe Magufuli aelezee mambo makuu aliyowatendea watanzania na mipango yake ya mbeleni.na lengo lake la kutaka kupanua zaidi. Huyu ni mgombea ambaye anapenda kuongea ila hajui aongee nini.

Tundu Antipas Lissu aelezee wapi aliposhindwa Magufuli na nini yeye ana mpango wa kuwafanyia watanzania.huyu ni mgombea mwenye sifa ya kuwa machachari na wakati mwingine anakimbia hadi kupitiliza kwao.

Bernard Camilius Membe aeleze wapi aliposgindwa Magufuli na nini yeye ana mpango wa kuwafanyiwa watanzania. huyu ni mgombea ambaye ana sifa za kuwa jasusi.amekosa mvuto kisiasa pamoja na jaribio la kumpamba sana.kifupi amepoa kama mate /udenda wa mgonjwa wa asubuhi.

Wawekwe hapo masaa mawili Taifa liwasikilize baada ya hapo kipyenga kipulizwe tukutane nao mitaani.
 
Back
Top Bottom