6 Pack
JF-Expert Member
- Apr 17, 2022
- 2,819
- 5,996
Kitendo alichokifanya waziri wako wa kilimo, umwagiliaji, maliasili na mifugo mh Shamata Shaame Khamis sio cha kiungwana na kiutu. Kile ni kitendo cha kinyama ambacho hakutakiwa kumfanyia mtanzania mwenzetu au binadamu mwenzetu kwa sababu yoyote ile.
Mtu kaingiza chakula mnafanyia unyama ule, je angeingiza bange au madawa ya kulevya hali ingekuaje?
Waziri ameshajiuliza kwamba ingekuwa ni yeye ndio kafanyiwa ule unyama leo hii angekuwa katika hali gani?
Mh raisi Mwinyi wewe ni mzanzibara, jaribu kutumia cheo chako kutetea ndugu zako maana kuna siku na wewe au ndugu zako yatawakuta haya haya yaliomkuta mama yule. Na pia ukiwa huku bara kama mbunge na waziri nafikiri umeona jinsi wabara tulivyokuwa na mioyo ya upendo kwa watu wote bila kujali kama mtu husika amezaliwa visiwani au bara, sasa iweje sisi huko upange tubaguliwe.
Waziri wako kajidai kujitetea lakini utetezi wake hauna maana yoyote kwa sababu hili sio tukio la kwanza au la pili kutokea. Imeshatokea sana mpaka muda mungine watu wanachoka ku report.
Ubunge, uwaziri na hata uenyekiti wa serikali za mitaa msitupe, lakini pia hata tukijitahidi kufanya vibiashara vidogo vidogo hata vya ndizi pia tunakataliwa? Huu sasa ni muungano au mkanganyo?
Hii ni sawa na baniani (mtanganyika) mbaya, lakini kiatu chake (madaraka kwa upande wa bara) kizuri.
Asante.