Ona wanavyokuwa na adabu wakiwa nje ya nchi bila akina Sirro

Ona wanavyokuwa na adabu wakiwa nje ya nchi bila akina Sirro

Mama anaupiga mwingi ndani ya ushungi.

Ametokomea kusikojulikana kwa spidi ya radi. Amekula kona (si ajabu alienda kujibanza kwa lile lizungu lake).

Hili libibi hata sio president material. Tunajilazimisha tu.
Mnajilazimisha wewe na Sukuma gang wenzako. Sisi huyo ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
 
Kwani Tanzania hamna watu wenye hali mbaya????

Hivi mtu akiwa na hali mbaya,unamwambia ana hali mbaya ili iweje?
Warudi walime hata bustani, maana huko hata kakihamba ka kulima hata muhindi hakuna
 
Hivi wale wafanyakazi wa pale HOTELINI wanaionaje nchi ya TANZANIA?

..watakuwa wanatushangaa na kumuona Raisi wetu ni kituko.

..kumpitisha Raisi uani ni jambo la hatari sana kwa usalama wake.

..huko uani ndiko kuliko na jiko, ndiko ziliko stoo za hoteli, eneo la kufua nguo, eneo la kupokea mizigo, eneo la kutupa mataka[dumpster], na ndipo vilipo vyoo vya wafanyakazi.

..Ni eneo ambalo wageni wa hoteli hawatakiwi kufika, sembuse Raisi wa nchi.

..Waliofanya hivyo wamemuaibisha Raisi, na zaidi wamehatarisha usalama wake.
 
Kweli Rais kazingua Sana hapo kama angewasikiliza angepata heshima kubwa Sana kama mtu anayetetea demokrasia,waliomshauri kula Kona wamemhalibia pakubwa sana ,ingempa political booster kama angewasikiliza na kuongea nao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Well Noted Mkuu.....

Washauri HAWAFAI kabisa less Intelligence!!!
 
tatizo hao wlio kusanyika hapo ni wahuni wabeba maboksi ndio maana walikataliwa hata kuingia ukumbini, unawaingizaje wahuni/machokoraa ukumbini karibu na Rais.....
unajua makundi kama hayo wengi wao ni watumiaji wa madwa ya kulevya akili hazijawakaa sawa.
Naona wanalalamika wamekataliwa kuingia ndani na ma Tshirt yao. Na wao kukaa kote Marekani hawajui jinsi ma-heckler wanaingiaje ukumbini kufikisha ujumbe wao?

Wengine wangeingia ndani. Wange vaa mavazi ya heshima kuandamana sio lazima uonekane mchafu mchafu ndio ujumbe ufike. Wengi wanafikiri kuandamana lazima uonekane kama chizi.

Wangevaa vizuri ata suti, kati kati ya mkutano mmoja anasimama anatoa ujumbe wake wana mtoa nje. Baada dakika kumi mwingine ana simama hivyo hivyo tu ujumbe unafika.

Sema wakitolewa nje wasigome hapo ndio sheria haikulindi utakamatwa.
 
Washauri hilo watanzania waliopo Tanzania ambao hawawezi ku afford milo mitatu kwa siku....bustani ya nini uko Udisporani kuna kuhangaika na bills sio chakula...acheni kudanganyana kwenye vijiwe vyenu...
Tanzania bado Ni nchi nzuri mnooo na ndio maana watanzania walio wengi Ni wagumu sana kukimbia hapa nchini.

Nchi nyingi zenye Diaspora wengi Ni zile zenye HALI TETE ya Kimaisha na USALAMA Kama Nigeria, Ethiopia, DRC na SOMALIA.

Tanzania mtu anaweza kutoka Bukoba, akaenda Ruvuma huko akalala kwa mtu asiye mjua, akala, akaoga, akanya na akapewa shamba la kulima bure.

Na anaweza akaoa kabisa akaanzisha familia huko huko, na akagombra kabisa uongozi hata wa mtaa akapata huko huko.

Suala hili huwezi kuliona hata Hapo Kenya.

Na ndio maana, Kutokana na mteremko wa Maisha ulivyo hapa bongo, watanzania wengi wakiendaga huko Ng'ambo Maisha huwa YANAWASHINDA.
 
Hapo ndio watu wapate akili, ile kauli ya Samia juzi kuwa yupo tayari kutoa ushindi kwa upinzani kwa kutengeneza mazingira mazuri ya kisiasa ilikuwa ni usanii mtupu.

Huyu aliyeonesha uroho wa madaraka kwa kuwashughulikia "wapinzani" wake ndani ya serikali yake, na kuwasogeza karibu watoto wa marafiki zake kwa ajili ya ulinzi wake, hawezi kufanya hivyo.

Kitendo chake cha kukimbia hapo kinaonesha vile mind yake ilivyo, kwake mtu anayedai Katiba Mpya ni kama adui yake, ndio maana akampa Mbowe kesi ya uongo ili kumfunga mdomo.
Na amefanikiwa kufunga mdomo kweli
 
..inawezekana ni fashion ila wewe kwa ushamba wako hujui.

..usione nguo au kiatu kimepauka ukadhani ni cha bei rahisi, wakati mwingine ni fashion na bei yake ni aghali.
Illusion, and the struggle to perfume faeces and trying to fit in.
 
hao ndio wabeba maboksi wanao ishi marekani.....wamechoka!!

yaani afadhali hata machinga wa K.koo
Rudini nyumbani.....acheni kupoteza muda huko na kushindia mikate na ukoko wa ubwabwa.
Tulieni muone wazalendo wenyewe. Huku nyie si mpaka Mbebe Mabomu
 
Rais anawakimbia watanzania wenzake tena ugenini hii ni aibu kwake
Hatuna Rais hapa.
Kama aliweza kukubaliana na Kauli ya mzee Yusuf Makamba ya " Wakati wa kulamba Asali"

Na Mbuzi kuenjoy majani said ya urefu wa kamba. Nini kinafuata.

Amewaingiza wezi wote jikoni wamefunga mlango wanakomba kwa kwenda mbele. Hii nchi CCM wanatakiwa wawekewe moto shingoni.

Sent from my SM-A115AZ using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom