Ona wanavyokuwa na adabu wakiwa nje ya nchi bila akina Sirro

Ulinzi anao pale pia.
Yeah, lakini siyo kama ule wa vitisho kama akiwapo nyumbani.

Halafu, huku unyamwezini hao walinzi wake hawawezi kufanya uonevu wowote ule.

Na sidhani kama kuna mwana-diaspora atakayekubali kuonewa kiboya kama ambavyo Watanzania waliopo nyumbani wanavyoonewa.
 
Kwaiyo Nyerere, Ali Hassan, Mkapa, Kikwete na Magufuli tu ndio waliokuwa na sifa za kuwa Rais. Acheni roho nyeusi watanganyika. Alipowekwa John mlisema chaguo la Mungu kwaiyo Samia kwa yote yaliotokea ni chaguo baya la Mungu si ndio
Hata Magufuli tukiacha ushabiki pembeni, hakuwa na sifa za kuwa Rais.
 
Amewakimbia huko atakuja "kuwasuta" akifika JKIA ambapo kuna vilaza wamelipwa tayari kwenda kupoteza muda pale kwenye mapokezi wakiwa na fulana na kofia za kufanana waanze kusema anaupiga mwingi !

Tukija kwa Mwigulu huyu nadhani pia kuna haja ya sisi kupatiwa historia ya afya yake ya akili.
 
Nikajua cha maana kumbe wahuni na wabeba mabosk wamebeba mabango ya kuombea kazi mbuzi kweli waje huku bongo ndio tutawaamini kweli wazalendo sio wabeba mabosk tumemtuma kuja huko kwa kazi maalumu kufungua nchi na kuitangaza nchi

Hao wabeba mabox ndio hawa mmewageuza mtaji wa kisiasa mnawaita wanyonge, ama watu wa chini. Au wanyonge kwenu ni watu wasioweza kuhoji lolote?
 
Rais anaweza kukifanya chochote akitaka, as long as una hold passport ya Tanzania.

Unaweza kuingia ubalaozini usitoke, Kama Kashoggi na ikawa imeisha hiyo.

Sema tu ukiwa Rais wa watu Milioni 60 unajua tu, Majuha hayakosekani unaamua kupotezea tu.

Kagame huyo hapo anafuatilia wabaya wake mpaka hoteli za huko Ng'ambo anaua.
 

Tanzania haina ubavu wa kukufanya chochote ukiwa nchi za ulaya magharibi. Labda ukiwa nchi zenye mitazamo ya kijamii kama China, Russia and the likes.
 
Rais hawezi kunifanya chochote anachotaka.

Hana mamlaka hayo.
 
Nilikuwa na maanisha ulinzi anao wa kuwasikiliza wanachosema bila kuogopa kupigwa kibao.

Manake sijaelewa kwanini kapitishwa mlango wa nyuma wakati angevuka tu barabara pale na kuingia ukumbini huku jamaa wanapiga kelele zao.
 
Tanzania haina ubavu wa kukufanya chochote ukiwa nchi za ulaya magharibi. Labda ukiwa nchi zenye mitazamo ya kijamii kama China, Russia and the likes.
Wewe ukiingia ubalaozini Nani atajua usipotoka?
 
Nilikuwa na maanisha ulinzi anao wa kuwasikiliza wanachosema bila kuogopa kupigwa kibao.

Manake sijaelewa kwanini kapitishwa mlango wa nyuma wakati angevuka tu barabara pale na kuingia ukumbini huku jamaa wanapiga kelele zao.
Hapo watalaumiwa wasaidizi wake.

Lakini ukweli ni kwamba yeye ndiyo Rais.

She can easily override them.
 
Dah!
..Ni eneo ambalo wageni wa hoteli hawatakiwi kufika, sembuse Raisi wa nchi.
Inafikirisha.

Lakini ni kumwonea tu huyu mama.
Mi ningeridhika kama hayo yangetokea kwa mtu kama Jiwe.
 
Hayo unayoyaeleza hapa ni ya ziada. Walichofanikiwa wakiwa hapo nje, katika ukumbi huo ni kikubwa zaidi ya huo ukumbi wa ndani.
 
K

Kadanganye wajinga wenzio kwenye vijiwe vya CHADEMA huu utoto
Hivi ni kweli huelewi unayoelezwa hapo, au ni kujikosha tu!

Kama ni kweli huyajui hayo, wewe utakuwa unaishi pangoni, tena mbali kabisa na mwanga unapopenyeza.
 
Mbowe Ikulu, what about you?. Japo rais ni kiongozi wetu mkubwa, ni mtumishi wetu, sisi Wananchi wa Tanzania ndio mabosi wake, tuliomuajiri kwa kura zetu na tunaomlipa mshahara kwa kodi zetu hivyo lazima atusikilize.
Usichanganye.
Ulimpigia kura lini huyu!

Expedience ya kumkaribisha Mbowe nayo unaiweka kama ndoana ya kuwanasa wajinga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…