ONYO kwa akina dada wote kuhusu huduma ya kukuza makalio itakayoanza kutolewa Mloganzila

Mxiuuuu!!
WAGONJWA WANNE WALIOPANDIKIZWA FIGO MLOGANZILA WARUHUSIWA

Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila kwa mara nyingine kwa mafaniko makubwa kwa kushirikiana na Korea International Foundational for Health Care na Africa Future Foundation imefanya upandikizaji wa figo kwa wagonjwa wanne ambao figo zao zimeshindwa kufanya kazi.

Upandikizaji huo ni wa kipekee hapa nchini kwa kuwa umetumia utaalamu wa kisasa Duniani ambapo figo imevunwa kutoka kwa mchangiaji kwa kutumia njia ya matundu madogo (Hand assisted Laparoscopic Donor Nephrectomy).

Akizungumzia upandikizaji huo katika hafla ya kuwaaga waliopandikizwa figo, Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi amesema utaalamu uliotumika kuvuna figo kwa kutumia matundu unafanyika Mloganzila pekee kwa Hospitali za Umma nchini na Afrika Mashariki na Kati.

“Kwa kutumia njia ya matundu mchangiaji anakuwa na kovu dogo, anakaa hospitali kwa muda mfupi takribaini siku mbili hadi tatu kitu ambacho kinasaidia kupunguza gharama kwa hospitali na mchangiaji pia” amebainisha Prof. Janabi.

Aidha, Prof. Janabi ameishukuru Serikali kwa uwekezaji ilioufanya ambapo amefafanua kuwa Mloganzila kuna vyumba vya upasuaji vya kisasa na vyumba vya uangalizi maalumu vyenye mashine na vifaa vya kisasa na pia kuna wataalamu bingwa na bobezi waliojengewa uwezo na Serikali katika nyanja tofauti tofauti.

Kwa upande wake Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania Dkt. Kim Sun Pyo amesema nchi yake itaendelea kushirikiana na Mloganzila katika kuwajengea uwezo wataalamu, na kufanikisha huduma za kibingwa hapa nchini kwa lengo la kuendelea kuboresha afya za Watanzania.

Naye, Mtaalamu Mwelekezi kutoka Korea Kusini, Prof. Park Kwan Tae amesema ataendelea kuwajengea uwezo wataalamu wa Mloganzila ambapo ameongeza kuwa huduma za upandikizaji kwa njia ya matundu zitafanyika mara kwa mara na hatimaye hospitali hii kuwa kinara katika upandikizaji kwa kutumia njia ya matundu Afrika.

Naye Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo, Dkt. Antony Gyunda ameishauri jamii kuwasaidia ndugu zao wenye changamoto ya maradhi ya figo kwa kuwa mtu akichangia figo hawezi kupata changamoto zozote za kiafya.
 
Bado hizo plastic surgery zina risk kubwa sana, hata huko kwa wenzetu walio mbali kiteknolojia na ujuzi. Angalizo la mleta uzi ni vyema likazingatiwa na watakaoamua kufanyiwa aina hiyo ya upasuaji. Hata Asia jambo hili limewatesa sana waliokwenda kufanyiwa upasuaji huko.
 
Ni muhimu kuanza kuliko kuogopa kuanza watakao fanikiwa ni sawa ambao hawatafanikiwa wafanya operation watapata uzoefu kupititia wao,miaka itakavyokwenda ndivyo ubora utakavyo ongezeka ,narudia ni bora kuanza kuliko kuogopa kuanza
Unahimiza wenzako wawe Guinea pigs!!!
 
Nchi za Kiafrika zimejaa madaktari fake, mloganzila hata jina lenyewe reflection yake ni mauaji au kifo, nakazia tutawapoteza wanawake wengi wengi sana
 
Mimi nadhani kwa matibabu amabyo ni ya urembo, wanatakiwa wapate ridhaa ya Serikali kwanza, na si kwa wao kujiamulia tu
Nina shaka kama leseni za kazi zao zinawaruhusu pia kufanya matibabu ya urembo ambayo hatukuwahi kuwa nayo hapo kabla
Kama mpaka imetangazwa au kuandikwa kwenye vyombo vya habari basi hizo taratibu zote zimeshafanyika.
 
Mungu huyo, Hakujua kwamba binadamu watakuja kumkufuru kwa kuwapa maarifa mengi?
 
Mtoa mada angetoa angalizo kuhusu complications au risks zinazotokana na operations au procedures za urembo lakini siyo kukandia na kukashifu Madaktari kama vile hakuna mazuri waliyowahi kuyafanya. Hatukatai makosa huwa yanaweza kutokea lakini je, makosa ni asilimia kubwa kuliko yaliyofanikiwa mpaka mtu ana-rule out kuwa wote ni vilaza? Au mwenzetu anatibiwa nje ya nchi akiugua?
 
IWE UPASUAJI NDANI YA NCHI AU NJE YA NCHI, ACHA WAFANYE.
MWILI WAKE,
PESA ZAKE,
MUONEKONO MZURI WAKE,
MAUMIVU NI JUU YAKE.

NAAM NA WAKIAZA KUOZA WANAKIMBILIA KWA MWAMPOSA.
ACHENI WAFU WAZIKANE WAO KWA WAO.
 
Nchi za Kiafrika zimejaa madaktari fake, mloganzila hata jina lenyewe reflection yake ni mauaji au kifo, nakazia tutawapoteza wanawake wengi wengi sana
Ni kweli usemayo. Hapa bongo kila kitu kinaendeshwa kimagumashi
 
Makosa ni mengi kuliko mazuri ndiyo maana viongozi wetu wakipatwa hata na mafua wanaenda kutibiwa nje ya nchi kwenye tiba za kiwango bora. Siyo kama hapa wanapobahatisha..
 
Hajui huyu tunavoumia Muhas. Na course work za prof kahamba
 
wana risk maisha yao ili kutufurahisha sisi wanaume ,najivunia sana kuwa mwanaume , NB marekani kwenyewe upasuaji huu haufanikiwi kwa asilimia 80,huku tz si ndo wataoza kabisa
 
Ahsante sana kwa kutoa ufafanuzi mzuri sana tunamkaribisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…