Open Letter: Rais Samia, TRA isiyo na Support yako, ni Kifo cha Taifa

Mtu anapoleta hoja kinyume ya unavyofikiri wewe usimuattack yeye kama yeye, attack hoja zake. Btw mimi sio mfanyakazi wa TRA na sio mnufaika kwa namna yoyote ile. Ila nimetoa experience baada ya kuona realities na mjadala wa baadhi ya maafisa wa TRA ambao tupo nao mtaani.

In simple terms, I am doing this not for personal gain rather for National Interest.
 
Lovely
 
Asante
 
Watu wanataka kulipa kodi halali na rafiki badala ya kutegemea harrassment kama njia ya kukusanya kodi pamoja na faini.Badala ya TRA kumshauri Rais kuhusu maeneo mapya ya kodi ili kupanua wigo wao wanasusa ni kwa vile wamefika mwisho wa kufikiri. Waangalie vyanzo vipya eg kuna taxi bubu nchi nzima hazilipi kodi mbona hawajashauri walipe wao wanakazania traditional methods tu.Rushwa !Rushwa!
 
Mama alishasema hata makusanyo yakiyumba kwa muda mfupi si hoja wakati utaratibu mzuri ukitafutwa. Au ulitaka nyie TRA muendelee kuwa miungu watu?...
 
TRA ni taasisi muhimu sana. Ila waajiriwa wake wengi wamefanya kama ndio biashara yao binafsi. Wameua biashara halali za watu kwa kisingizio cha kukusanya kodi, huku wakineemeka na rushwa isiyosemekana.
TRA inajitaji kusukwa upya. Waende kuajiri watu wengine waadilifu na wanaolewa maana ya umuhimu wa kuwa na private sector.
Wanaodhani kama bila wao TRA haitakuwepo, ni wakati sasa wa kujitafakari. Wasituharibie nchi yetu kwa kuendeleza dhuluma kwa kiini macho cha kukusanya kodi
 

Kuna watu pale wamekaa ofisi za umma kama wako nyumbani kwao. Wakitaka kuongeza nyumba wanachukua mafaili na kuhangaika na wafanyabiashara ambao pengine hawana tatizo lolote, ili tu wapatiwe rushwa
 
Kwa mtu niliye na tajiriba na IRS [TRA ya Marekani], naona kama vile Watanzania bado hatuko serious na ukusanyaji kodi!

IRS ni moja ya tax collecting agencies zisizo na mzaha.

Ukitaka kukusanya mapato kupitia kodi, basi ni lazima uwe thabiti.

Upole haufai.

Lakini pia haina maana kuwa ndo uonee watu, ingawa ni kawaida ya binadamu kuona anaonewa hata kama si kweli.
 
Kulipa kodi ni takwa la sheria, hao wafanyabiashara wanatakiwa kulipa kodi kutimiza wajibu wao, wakigoma wacha sheria ichukue mkondo wake, hao maafisa wa TRA unaosema wameamua kukaa pembeni kwa kuogopa kubagazwa ni wazembe wanatakiwa kuadhibiwa.
Point.
 
Rais hajawazuia TRA kukusanya Kodi. Alichosisitiza mh.Rais ni weledi katika kutekeleza zoezi hilo.
Hata mimi nilielewa zile task force za kutumia mabavu kutoka DC. DSO. Takukuru and alike ndizi zisizotakiwa lakini kama mpaka enforcement ya kawaida tu ya TRA wenyewe nayo haitakiwi basi hapo shughuli ipo tena si ndogo.
 
Ku- abandon atafanya tu ikiwa anaona haina tija kwa taifa. Mbona A Mwinyi hakuendeleza viwanda vya Tanganyika Packers vya Shinyanga na Mbeya. Hata mwenywe Mwendazake ali abandon bomba la gas ya Mtwara na kuchagua STIGLERs.

Sidhani kuwa eti kigezo cha viatu kukutosha ni ku implement miradi blindly?? Mtu anaanzisha daraja la Mwanza Busisi wakati liko nje ya Mpango, unashindwaje kuliacha kama hilo.

I expect atafanya anayoweza kwa wakati wake na tutapiga hatua.
 
Ukikamata mkwepa kodi mfilisi kabisa ili wengine waogope! Vinginevyo we are bound to fail!

Na ukikamata mwenye kuonea mlipakodi kwa makusudi kwa lengo la rushwa NYONGA KABISA ili nchi iende smoothly.
 
Hii ni hatari sana.

KODI NDIO usalama na UHAI wa TAIFA bila kukusanya KODI basi tena ndio tunaenda kuzimu.

wafanya biashara walio wengi ni wa kwepa KODI kamwe hawawezi kulipa kodi bila kushurutishwa.

Kwenye suala la KODI viongozi wetu wawe imara.
 
Hayo yote ni sawa kabisa mkuu,TRA wabuni new revenue sources,hilo halina ubishi,ila under scrutiny here are President Samias' statement ambayo ina potential ya kupunguza mapato.
 
Rais hajawazuia TRA kukusanya Kodi. Alichosisitiza mh.Rais ni weledi katika kutekeleza zoezi hilo.
Hakustahili kabisa kuwaambia pale hadharani,kwa kuwa alikuwa keshateua Kamishna mpya,angekaa naye pamoja na wataalamu wengine wazungumze
 
Mbona Mapema sana nchi imeishamshinda Mama mtanipa majibu baada ya mwaka mmoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…