Open Letter: Rais Samia, TRA isiyo na Support yako, ni Kifo cha Taifa

Kodi imekusanywa kuanzia Serikali ya Mkoloni na itaendelea kukusanywa.

Mwendazake alikosea sehemu moja. Aliwafirisi wafanya biashara wakubwa then akakosa mahali pa kukusanya kodi, ndiyo akaja na wimbo wa KIJINGA wa EFD machine.

Mkapa na Kikwette ndiyo waliojenga uchumi imara bila hiyo EFD yenu ambayo mumeifanya ndiyo collection driver.

Ukiwa kiongozi unapswa ufuate Pareto principle kwenye kujenga uchumi. Pareto Principe inasema ni Asilimia 20% tu ya walipa kodi ndiyo huleta 80% ya mapato yote. Hao ndiyo una deal nao kama Twiga Cement, TCC, TBL, BAKHRESSA, MODEWJI, IPP etc. Hawa akina kajamba nani waliobakia ambao ni 80% wanachangia 20% tu ya mapato ambao ni vituo vya petrol station, maduka ya Kariakoo, mabaa, guest house, mabasi etc.

Yaani nguvu kubwa inatumika kwenye chanzo kikubwa cha kodi. Hiyo ndiyo AKILI

Lakini akili mbovu ya Mwendazake iliwakera na kuwa harass wafanyabiashara kama Yusuf Manji ikasahau kuwa ni mlipa kodi kupitia wafanyakazi aliowaajiri, bidhaa anazo nunua na ku export as well as anazo import.

Tuna Imani na Rais SSH tutakusanya kodi iliyo ya haki na maisha yataendelea
 
UMEPOTOSHA ALICHOSEMA MH.RAIS MAKUSUDI HALAFU MATAGA WENZIO WANAKUSIFIA.

MAMA ALISEMA TUNAHITAJI KODI ZIKUSANYWE ILA SIO ZA DHULUMA.

ALISEMA, KUNYANG'ANYA WATU PESA KWENYE AKAUNTI ZAO, KUSINGIZIA KESI ZA UHUJUMU UCHUMI NA KUTOA MAKADIRIO YASIO SAHIHI HIYO HAIKUBALIKI.

MAGOFOOL ALIKUSANYA KODI KWA MUDA MFUPI TU MIAKA MITATU YA KWANZA BAADA YA HAPO BIASHARA ZIKAFA AKAANZA KUKOPA HELA NJE NA KUTOA TAKWIMU ZA MAKUSANYO ZA UONGO.

KAMA ALIKUSANYA PESA NYINGI MBONA MIRADI YOTE INAFANYIKA KWA MIKOPO AU MISAADA KUTOKA NJE? MBONA AMESHINDWA KUAJIRI NA KUPANDISHA MISHAHARA?

JIULIZE MAGOFOOL DENI LA TAIFA ALIKUTA SH.NGAPI NA KAACHA SH.NGAPI. UKIJUA HILO HUWEZI KUJA KUANDIKA UHARO HAPA TENA.
 
Weka clip aliposema wabembelezwe msitupotoshe nyie maafisa wa TRA. Hakuna Mhe.Rais aliposema watu wabembelezwe kulipa kodi, alisema tumieni akiri kwa maslahi mapana ya Serikali na mlipa kodi pia.
Hawa ni sukuma Gang mkuu
 
Kama wewe ni mwislamu, jioni pata futari nutalipa. Kama mkristu pata soda weekend imeanza.

Hawa watu ni wajinga Sana na wanajifanya wasahaulifu. Wanamtukuza mtu aliyekuja kuharibu uchumi wetu kwa kukosa mipango sahihi na kutosikia ushauri
 
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Huna point yoyote!

Pumba tupu!

Raisi Samia Suluhu Hassan hataki kodi za dhuluma.

HAKI HUINUA TAIFA
 
Na wewe unawatisha kama Task Force,au wewe ni Task Force ya kutisha TRA🤣🤣🤣
 
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji106]
 
Kama wewe ni mwislamu, jioni pata futari nutalipa. Kama mkristu pata soda weekend imeanza.

Hawa watu ni wajinga Sana na wanajifanya wasahaulifu. Wanamtukuza mtu aliyekuja kuharibu uchumi wetu kwa kukosa mipango sahihi na kutosikia ushauri
Mwendazake adi magari ya kuchukua maiti alitaka yawe na EFD machine eti ni vyanzo vya kodi na hili ni alipoona Corona inaua sana yule mzee dah
 
Observation makini kabisa. Wafanyaji Biashara wadogo wakipangiwa kodi rafiki bila shaka watalipa,hili limedhibitika nchi ya jirani.
 
Mama hataki kodi za dhuluma. Period.

HAKI HUINUA TAIFA
 
Unawaza kizamanizamani! Pole!

Mama hataki kodi za dhuluma

HAKI HUINUA TAIFA
 
Hizo zama zenu za kutumia ubabe na nguvu kukusanya kodi za dhuluma zimepita! Tambueni kwamba hizi ni zama mpya za serikali ya kutumia akili na weledi!

TRA wanajua how to be professional. Na kodi ya kutosha itakusanya kwa weledi.

HAKI HUINUA TAIFA
 
Sikubaliani na mfumo wa kuwaumiza walipa kodi hasa wafanyabiashara wakati na wakubwa kwa sababu tu ya kwenda kufanya dili za kununa mandege na mareli ili wazungu na matajiri wanaotoka Ulaya wapande kwa bei rahisi nabiuwaumiza watanzania wa kawaida wenye vifuso vyao na kirikukuu za kubeba viazi kutokea mbea na kwengineko.

Hivi huoni kuwa awamu ya tano ilikua inawaumiza watu wanaojitafutia fedha wenyewe huku ikitumia fedha nyingi kununua wapinzani na kulipa mamishahara makubwa wakurugenzi wa Tarura,TRA ,Bandari,Tanapa, Sumatra, Ewura, Tanroad na wabunge, mawaziri huku wakiwa hawazalishi chochote zaidi ya kuwaumiza wafanyabiashara ili wao waishi maisha ya kifahari kwa mishahara mikubwa na rushwa nono.
Mwacheni mama Samia afanye kazi aliyotumwa na Mungu kuwafariji watanzania walioletwa duniani kuifurahia dunia kwa haki sio kuumizana kwa sababu ya kujenga masanamu na mapiramidi yasiyo na uhai wala roho wala hayajui kumsifu na kushukuru Mungu.

Unashangaa nini kuona mtaji mkubwa unatoa faida ndogo?
Mbona ATCL ina mtaji wa matrilion ya fedha lakini haipati faida ?

Kama mtu hatoi risiti sheria si ipo afikishwe mahakamani kama anakaidi sio kwenda kufunga akaunti zake na kuiba fedha zake huku mkifikisha kidogo mnakojua na nyingine kuweka mifukoni mwenu.
Nani anajua mlikopelela fedha zote mlizokwapua kwa wafanyabiashara ? Je, mlitoa risiti au Tax clearance kwa wenyewe hasa wale waliokufa kwa presha.

Tusimamie sheria kwa haki na kuongeza wigo wa walipa kodi.
 
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Sio kweli, tuwe tunaandika Vitu vyenye uhalisia. ungeweka ushahidi wa mfanyabiashara aliyedaiwa kodi akagoma au akakataa kutoa risiti. Tusizushe mambo kwa faida zetu binafsi

Chief, kweli unadhani it’s that easy kutoa “evidence” ya mkwepa kodi mashuhuri?

Unakumbuka issue ya watu wa oil ambayo ilimeletea Chief Max kadhia ya mahakamani mpaka leo?

Speechless!
 
Acha kiherehere mkuu. Wafanyabiashara wasisumbuliwe kabisa.
 
Kulipa kodi ni takwa la sheria, hao wafanyabiashara wanatakiwa kulipa kodi kutimiza wajibu wao, wakigoma wacha sheria ichukue mkondo wake, hao maafisa wa TRA unaosema wameamua kukaa pembeni kwa kuogopa kubagazwa ni wazembe wanatakiwa kuadhibiwa.
👊👊
 
Mimi ni miongoni mwa pro-Magufuli kindakindaki na niliyeamini na bado naamini katika sera za Magufuli nyingi. Ila miongoni mwa vitu vilivyonipa/vinavyonipa ukakasi katika utawala wa Magufuli ni inshu ya kodi na nifafanue.

Naamini katika kodi na ni lazima kila mfanyabiashara na wafanyakazi tulipe kodi. Tusipolipa kodi nchi yetu tuipendayo itajengwaje? Lakini kuna suala la kulipa kodi na kuna suala la unyanganyi katika kodi. Mtazamo wangu katika kodi ni kwamba kodi anazostahili kulipa mfanyabiashara au mfanyakazi ni zile kodi za msingi na zinazolipika. Mfanyabiashara hawajibiki kwa serikali peke yake, anawajibika pia kwake mwenyewe, kwa familia yake, kwa wafanyakazi anaopaswa kuwalipa mshahara, rejeshi benki kama amechukua mkopo na wakati huo huo ahakikishe biashara yake haifi bali ikue siku hadi siku.

Mama Samia alishauri TRA wajiongeze katika kupanua tax base badala ya kuwakomalia wafanyabiashara hao hao. Ng'ombe unaye mmoja, huyo huyo unamkamua hadi damu, hutaki kuongeza ng'ombe wengine, si atakufa huyo? Maana ya kuongeza tax base ni kwa TRA kuwa wabunifu na kuhakikisha inatengeneza au kuwafikia walipa kodi wengi badala ya kujikita tu kuwafuata walipa kodi hao hao tu.

Mimtu ya TRA ni miongoni mwa wafanyakazi wazembe sijapata kuona. Yaani yenyewe inajua kukaa kwenye computer na kukadiria watu kodi tu wale wafanyabiashara wa mjini walio karibu karibu na ofisi za TRA. Ukiwa mfanyabiashara wa ndani ndani huko pembezoni ambako TRA hawajiongezi kufika (watafikaje na mitambi yao?) labda ujipendekeze mwenyewe kujipeleka TRA kulipa kodi. Hiyo ndiyo maana ya kuongeza tax base. Hii nchi ina watu milioni 60, haikufutwa kodi ya kichwa ili mzigo uwaelemee vichwa vichache.

Kama tunajenga nchi moja tukubaliane kwamba watu tulipe kodi wote lakini inayolipika. Serikali pia ijue kwamba kodi ni jasho la watu. Hatulipi kodi ili itafunwe na matakataka yaliyomo serikalini kwa kujinunulia magari ya kifahari, kujilipa miposho na mishahara minono. Nina uhakika kwamba kuongeza tax base pia ni kutumia kodi kwa matumizi sahihi katika huduma bora kwa walipa kodi. Utamshawishi vipi mfanyabiashara kulipa kodi kwa moyo wakati barabara zinazotengenezwa hazifiki mwaka zinaanza kuharibika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…