Opinion: Dr. Shika Ana Hali Fulani, Anahitaji Msaada, Huruma, Upendo na Protection of His Right to Privacy!.

Kitu pekee mpaka sasa kinanipa mashaka katika maelezo ya Dr ni hili swala la money transfer hasa kwenye inquiry aliyoipata kutoka kwenye hiyo Bank anayodai inamtumia pesa za kununua nyumba.

Ambapo anatakiwa alipe asilimia 25 ya billion kama tatu ambayo itakua sio chini ya million 725 sasa kwenye hoja kwamba bank samemdai bima ya hiyo pesa ambayo amesema ni dollar za kimarekani 150 kama sikosei, hapo pana utata

Sidhani kama million 725 zinaweza kulipiwa bima ya 332,500 hapa kidogo nilitaka maelezo labda kama nilimsikia vibaya nitarekebishwa.
 
Mkuu nimesoma bandiko lako japo naamini na wewe umeenda moja kwa moja kwenye judgement/ final conclusion lengo langu sio kukupinga ila kuna baadhi ya vitu nimetokea kuviamini kwake vinavyonifanya nipingane au nitofautiane na wewe kidogo ...nachoamini Dr Shika yuko fiti sema kakubariana na maisha anayoishi

Masomo aliyoyasoma na mimi naamini ni kweli kayasoma na nikirudi kwenye nadharia ndogo tuliyoizoea ata ile ya advanced level kipindi kile shule bado ziko shule kwa waliosoma masomo ya sayansi nikimanisha michepuo kama pcb ,pcm hasa hasa pcb simply tulikuwa tunawaterm/wanatuterm kama "vichaa" flani hasa kwa wale ambao walikuwa bize sana (wanajua wanachokifanya) kwa mantiki hiyo fikiria masomo ya M.D kipindi chao na uzuri au ubaya nchi aliyosomea ni ukweli usiopingika unaweza kuwa chizi flan hizi kimasomo ....kumaliza masomo yake yote kama anavodai automatically wengi tutamterm kama mtu ambaye alivo kama wengi wanavomjugde ....bad enough changanya na misukosuko aliyopotia .....

Nachoamini baada ya yote dr yuko very comfortable na maisha anayoishi ambayo nadhan ni sahihi kwake ...

"Yawezekana usione point nilichokiandika"
 

Hili ni kweli kabisa,kinachonishangaza ni hao wanaomuhoji kushindwa kuuliza maswali kuhusu baadhi ya taarifa kama alizozitafuta britanicca huko Russia.

Mfano:
1.Ni kweli alitibiwa Dnipro,Ukraine?
2.Ni watekaji wa aina gani waliomfanya mbali na kuingia Tanzania bado hakujiona salama akakimbila Malaga,Spain?
3.Alipata wapi mtaji wa kuanzisha kampuni kubwa katika kipindi kifupi tu cha kufanaya kazi ya kufundisha akifanikiwa kuvuka vikwazo vyote vya ubaguzi,communism nk?
4.Nani alifinance safari nzima toka Russia to TZ na kisha TZ to Malaga (Hapa ni pamoja na hifadhi ya huko Malaga for all his time of stay)?
5.Toka afike hapa Tanzania amewahi ripoti katika chombo chochote cha serikali kuomba msaada kuhusu mali na haki zake zilizo Russia?
6.Kwanini atembelewe na Mmarekani kwanza baada ya tatizo na si mwingine yeyote(kulikuwa na interest gani ya mmarekani kwake?)
Nk Nk
 
Nakuunga mkono ..."time " ndo tunachosubiria make kuna wengi walidhani mwanzoni huyu mtu kuna watu wako nyuma yake lakini sio kweli


Alafu wanaobeza kigezo cha kulipia pesa bima kabla ya kutumiwa nawashangaa ni kitu cha kawaida sana na kipo na mimi nina mfano hai kabisa
 
Ndio hapo ninapopata shaka na " nia" ya Paskali kutaka kutuaminisha vinginevyo, ukitafakari kwa makini ni kama vile Paskali ametumwa!!
 

Kaka katika maelezo yako naona kwa njia moja ama nyingine unakiri au unaamini kiwa Dr. Kishi alitekwa na kuingia kwenye mateso makali sana
Swali nalokuuliza kwa mtazamo wako, unahisi Dr.Shiki alitekwa na kuteswa hivyo kwa sababu gani au kwa madhumuni gani?
 
Mfano Leo hii bosi wa airtel atekwe apigwe au chukulia mfano dr olimboka apigwe ila sio kwa kiasi kile atashindwa kutoroka na kukimbia nchi za nje ?pesa atakua nazo na assist ya mke ,wenzake nk

Wakati ule bado pesa alikuwa nazo tu na connection mke ,marafiki nk..lakini kwenye mahojiano alisema alienda hospital kutibiwa so malaga alienda baadae kabisa

Huyu past inamsumbua ana tatizo la kisaikolojia na hakubali hivyo anajipa hope tu ,aidha alidhulumiwa stahiki zake au ahadi ,wee mtu tokea miaka 10+ anasubiri pesa kutoka urusi tu

Na huenda kwa panic yake akakutana na matapeli wa mtandao ndio wanamdanganya akate bima ya dollar mia na nusu eti atumiwe pesa ,huu ni utapeli kama ya wale jamaa mbagala wanachezesha kamari ya assets eti ukishinda utoe 100,000 upewe zawadi akina mama wanapigwa kweli

Dr asaidiwe kisaikolojia
 
Ni kawaida Tanzania kupelekeshwa na wagonjwa wa akili. Alianza babu wa Loliondo na sasa Dr shika. Wengine sitawataja. Kama ulivyosema kichaa siyo mpaka aokote makopo.
 

Kaka hivi unafahamu nchi zenye security tight? Yaani utoroke Russia kienyejienyeji tu? Kaka issue iko hivi, kavunjwa mbavu tano, kakatwa vidole viwili na kimoja kimepondekapondeka na jamaa kaweza kuruka ukuta, alijinyanyuaje juu ya ukuta huku mbavu zimevunjika?

Ndio maana nasema huyu Mzee anakitu kizito sana anachokijua, kaka hivi kweli unaweza kuniambia huyo mzee alitekwa kwa sababau gani hasa?
 
No way mzee anaongea kila kitu kwa mpangilio hajimix. Serikali si ichunguze mwaka alioondoka pia iwasiliane na Urusi watu anaowafahamu urusi wahojiwe ubalozi uhojiwe nimesikia story yake na naanza kumuamini
 
[emoji1] [emoji1] sawa mkuu
 
Hujasikiliza kwa umakini katekwa kisa watekaji wanataka hela usikimbilie kujudge kwani serikali itapoteza nini kumfuatilia huyu mzee in details waangalie je aliwahi kuwa huko urussi? Na aliondokaje ondokaje huko
 
The guys is simply sick
 
Hujasikiliza kwa umakini katekwa kisa watekaji wanataka hela usikimbilie kujudge kwani serikali itapoteza nini kumfuatilia huyu mzee in details waangalie je aliwahi kuwa huko urussi? Na aliondokaje ondokaje huko
ILI IWEJE?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…