Wabongo ni wabinafsi mnalalama bidhaa za wenzenu zisiingie halafu nyinyi mnataka mkauze kwao. Hamjifunzi ziara ya Samia Kenya? kilichofanyika ni ruhusu niingize hiki kwako na mimi nikuruhusu uingize hiki kwangu 50/50 win-win.
mama aende nchi nyingine za afrika (Sahara kusini) tuwe na bilateral agreements mfano wewe malawi niruhusu kuingiza madekio malawi, mimi tz nitakuruhusu kuingiza mafagio tz, congo ingiza vumbi, mimi naingiza mkuyati. No free lunch
Tuna kaubinafsi fulani mwenye kututibu nacho atakuwa katusaidia sana.
Tuko kama matoto yaliyolelewa vibaya. Tunadhani wengine wote ni wajinga ila sisi.
"Ya kwamba ngoja wajifungie ndani sisi tuchape kazi. Tuje tuwauzie chakula kwa bei tunayotaka sisi." Haya wazi wazi na tunaowasema wanatusikia.
Hulka dhaifu sana.