Orodha ya bidhaa ambazo Serikali inatakiwa izizuie kuingia nchini

Orodha ya bidhaa ambazo Serikali inatakiwa izizuie kuingia nchini

Mbona Sukari ilizuiwa kuingia mwishowe tukapoteana hadi leo bei ipo juu tu
Ku install kiwanda cha sukar si sawa na ku install kiwanda cha tomato sauce au pipi au maj ya kilimanjaro kiongoz..kiwanda cha sukar ni ishi nyingne..ngoja cha bakhresa kimalizike tuone...watakapozuia kabisa ndipo speed ya kuwekeza viwanda itaongezeka.sasa hiv speed ndogo sabab vtu vyote viko bwelele vinakua imported...wakizuia utaona akil zitatukaa sawa. Tutakunywa uji wa chumv kwa siku kadhaa ila baada yahapo nauhakika viwanda vya bidhaa hyo vitatapakaa kila kona...wa Tz wamebadilka sasa hv si kama wa zaman. Watu wanachangamkia fursa vbaya mno
 
Naona wameusoma uzi huu jana .mwigulu alipita huku nn..ingawa naona kama bado maeneo meng hawagusa..wameongeza kod kwenye imported goods flan flan ila sio nying za kutosha..kama wanaogopa ogopa hiv. Au jicho halijaona sawasawa

Ila safi so far.
 
Furniture. Furniture. Furniture. Wakianza na hilo watakua wamefanya jambo kubwa sana

Huwa nashangaa watu kununua furniture kutoka nje wakati mafundi kitaani wanatengeneza furniture nzuri sana kwa bei poa. Imagine ofisi zote zingekua na furniture zilizotengenezwa nchini tungekua wapi.
Shida na mafundi wetu upuuzi ni mwingi. Mtu anaweza lipa fundi ila akazungushwa hadi akajuta kuingia nae mkataba wa kazi.
 
Nimeuliza tu ikiwa na wao wataamua kuzuwia wasinunue mazao itakuwaje kwa upande wetu ?

Ndio hata sisi hatuwezi kuzuwia hizo bidhaa.
Hapa tunazungumza endao zitazuwiwa.

Kuna bidhaa hazipo hivyo.

Mfano ukizuwia fagio zisitoke china utaagizia nini huko china ?

Ukizuwia miswaki istoke china utaagiza nini kama mbadala wa mswaki huko china kama ilivyokuwa mbadala wa mashati ni vitambaa ?

Kuna bidhaa ambazo ukizikatisha moja kwa moja uagizaji basi hakuna muamala mwingine unaohusiana na bidhaa hizo.

Sasa mimi ninachouliza ni kuwa,je na wao wakisema wazuwie wasinunue vya kwetu itakuwaje ?


Mbona vitu vyepesi hivi kueleweka?
Hatuna Mkataba na China au nchi yoyote Ile kuingiza kila bidhaa kwa kuitaja moja moja...

Ndani hatuna Mkataba na nchi yoyote kuingia mafagio...tukipiga marufuku tunapiga ban ya
Bidhaa hizo kutoka nchi zote..


Hakuna nchi itakayo kuja Ku complain eti tumezuia mafagio kutoka nje
Hakuna
 
Kuna bilateral na multilateral treaties.

Huwezi amka na kuzuia bidhaa zisiingie wakati kuna mikataba mmetia saini na nchi mbalimbali.


Malaysia walikuwa na policy ..
Mkataba wowote ule ukipingana na policy za ndani ..kitakachofatwa ni policy za ndani
 
Dawa sio kupiga marufuku.. Hivi umewahi compare bei ya bidhaa za ndan na nje?
Mi nadhan tupambane tu kwenye finishing ya kueleweka, na bei iwe rafiki.

Bidhaa za ndani tunauziana bei za ajabu ajabu sana na usanii ni mwingi, uaminifu hamna ndo maana mtu anaopt anunue tu meza au kabati la mchina.
 
Bado tatizo linabakia kuwa tanzania tuna gap au ombwe la uongozi. Watu waliopo serikalini na meza kuu za maamuzi hawana best interest at heart kwa vijana na taifa. Wanalenga kujenga maisha yao, familia zao na koo zao. Hii ni laana kwa taifa.
 
Shida na mafundi wetu upuuzi ni mwingi. Mtu anaweza lipa fundi ila akazungushwa hadi akajuta kuingia nae mkataba wa kazi.
Mafundi wetu chenga sana.. Mimi siku hizi sitaki kusumbuana nao.
 
Imagine hakuna fagio kutoka nje..halaf lina uhitaj wa kufa mtu..watu wanaotengeneza watakua weng..kama matikit yanavyofurikaga au mananas. Bei ztashuka had jero.fagio jero..simple maths tu..serikal haijataka bado wakwamua watu wake....wafanye hivyo waone...

Nchi kama nchi kwa sasa watu wameamka..we are ready for change...hata mafuta ya kula...wapige marufuk mafuta ya nje waone...utaanza ona alizet inalimwa mpaka Dar...chezea njaa wew
Viongozi waliopo wasiposoma nyakati, muda c mrefu watakalia kuti kavu. Kizazi cha sasa kukidanganya ni ngumu sana wanakuwa michezo yote nje ndani. Sasa hizi siasa za mwaka 40 wanazoleta miaka hii wanachemka balaa.
 
Unaweza kuvioona vipo vingi..lakini vikizuiwa asubuhi mchana hutaviona mtaaani.
 
Viongozi waliopo wasiposoma nyakati, muda c mrefu watakalia kuti kavu. Kizazi cha sasa kukidanganya ni ngumu sana wanakuwa michezo yote nje ndani. Sasa hizi siasa za mwaka 40 wanazoleta miaka hii wanachemka balaa.
Wanyonge wa kuwaproganda mbona bado ni wengi tu
 
Baadhi ya bidhaa hazihitaji hilo
Kwani mafagio yakikosekana ndo nchi ita taabika?

Bidhaa ambazo sio za ulazima sana..tuzuie moja kwa moja..

Acha simu ziingie lakini zuia cover za simu
Hakuna atakae andamana kisa kakosa cover
Scarcity yake italeta ubunifu watu wataanza tengeneza wenyewe
Then watakaonzisha hivyo viwanda ni hao hao wachina nchini.
Made in tanzania mmiliki mchina
 
VIBIRITI
Mjembe
Wheelbarrows
Mapanga

Kawa kifupi zana zote za kilimo!! Mbona zamani tulikuwa na viwanda vinatengeneza?

Selective protectionism helps the growth of budding industries.
Umenikumbusha ZZK MBEYA

ova
 
Baadhi ya bidhaa hazihitaji hilo
Kwani mafagio yakikosekana ndo nchi ita taabika?

Bidhaa ambazo sio za ulazima sana..tuzuie moja kwa moja..

Acha simu ziingie lakini zuia cover za simu
Hakuna atakae andamana kisa kakosa cover
Scarcity yake italeta ubunifu watu wataanza tengeneza wenyewe
Mkuu The Boss ,naunga mkono hoja 100%.
Naomba mods Maxence Melo ,muuweke uzi huu uwe "sticky" kwenye majukwaa yote ili "wafanya maamuzi" wauone hata wale wanaopenda kutembelea jukwaa la watu wazima tuu.
 
Furniture. Furniture. Furniture. Wakianza na hilo watakua wamefanya jambo kubwa sana

Huwa nashangaa watu kununua furniture kutoka nje wakati mafundi kitaani wanatengeneza furniture nzuri sana kwa bei poa. Imagine ofisi zote zingekua na furniture zilizotengenezwa nchini tungekua wapi.
Tatizo mafundi wetu hawajielewi hawana professionalism kbsa wameendekeza sana uswahili, usipokuwa makini kabati tu utajengewa kwa miezi hta nane!...ndio maana watu wengi hawataki usumbufu wanaamua kwenda dukani kununua furniture za mchina.
 
Mimi la kuona tunanunua mafagio kutoka China linaniumiza sana
fagio sasa hivi zina tengenezwa hapa kuingiza ushuru wake ni mkubwa sana huwezi uza kwa faida!
Furniture nazo ni hivyo hivyo ndio maana Waturuki wana zitengeneza kwa wingi apa bongo kwa sasa kuingiza kutoka nje ushuru ni zaidi ya manunuzi!
 
Back
Top Bottom