Orodha ya Miji yenye hadhi isiyostahili

Orodha ya Miji yenye hadhi isiyostahili

Hizo zote ulizotaja ni makao makuu ya mikoa. Ni suala la kisera makao makuu ya Mkoa kuwa Manispaa. Hata Kibaha na Njombe zitapata hadhi hiyo siku za karibuni.

Aidha kimiundombinu ya pale mjini Tabora na Kigoma Ujiji huwezi kubeza. Kwa area na population Tabora na Shinyanga huwezi kuziondoa.

Lakini pia kama Tunduru, Korogwe, Mbinga, Babati ni Town Councils, hizo Manispaa zilizopo hapo haziwezi kuwa kundi moja na Town Councils.
Dah! Population haimake sense
 
Kumekuwepo na mjadala kuhusu Majiji.

Ukweli ni kwamba sio Majiji tu ambapo yapo yenye hadhi hiyo ilihali kiuhalisia ilipaswa yawe manispaa Tu.

Leo nakupa orodha ya manispaa zisizostahili hadhi hiyo.

1. Lindi
2. Shinyanga
3. Tabora
3. Singida
5. Kigoma
6. Songea
7. Musoma
8. Bukoba

Manispaa hizo kimiundombinu na maendeleo ya mtu mmoja mmoja bado Sana. Mfano Shinyanga nilipofika nilibak mdomo wazi.

Taja manispaa zingine
Ongeza sumbawanga
 
mim nipo kigoma mda huu na ndo naishi huku haifai kuitwa manispaa ilifaa iwe mji wa kigoma, maana hata mji wa Same unapazidi Manispaa ya Kigoma
Duh Same Vs Kigoma
 
Ndio tanga ilikuwa jiji enzi kuna viwanda na watu wengi sana walienda kule kufanya kazi viwandani lakn viwanda vilivokufa na tanga pakafa kilichopo sahv ni magofu japo utawala wa huyu mbunge wa sasa ameanza kupabadilisha
 
kuna wilaya ina itwa mwanga wanahadhi ya mji mdogo pale tambarare ila kiukweli ni kama kakijiji naenjoy kufika na kukaa kwakua ni home ila sio siri hata hadhi ya mji mdogo haipo labda ilikuja kwa heshima ya baadhi ya viongozi na wadau wa chama wenye heshma.....
Mwanga hii hii au nyingine?
 
Mwanga haijawahi pewa hadhi hiyo.
haijawahi kivipi wakati ina hadhi ya mji mdogo na najiuliza mji mdogo kwa lipi hasa..,.... sikatai haina hiyo hadhi ila mamlaka husika zinatambua mwanga ina hadhi ya mji mdogo ila ukiangalia maendeleo mzunguko wa pesa makazi ya watu huduma za kijamii alooo utapagawa..... ni home ila dah sio mchezo upare mwingi
 
Back
Top Bottom