Orodha ya ndoto (karibia zote) na maana yake
Habari ,huwa Mara nyingi naotaga vinyesi au vyoo vikiwa vichafu havijasafishwa ,hii ndoto ina maana gani
 
Hivi hadi siku hizi watu wapo wanao ota??mimi sioti ndoto yeyote yani,, huwa nalala kama saa moja tu basi
Sijui ndoto ikoje kabisa wakuu
 
Habari wana familia wa jamii forums

Nimekuwa nikiota ndoto za kurudi shule mara kidato cha 4/3/1/
Nakaribia kufanya mitihani
Wakati kwa uhalisia mimi ni mhitimu wa muda mrefu sana.

Na kwenye ndoto inakuwa nipo pamoja na watu ambao tulishawahi kusoma nao lakini walinipita vidato
lakin kwenye ndoto hutokea naona nipo nao kidato kimoja.

Ndoto za aina hii zimekuwa nyingi mno karibu kila siku naweza sema

Na kuna muda huwa nahisi ndoto ndo maisha halisi
Yaani ndani ya ndoto naona kama ndo maisha ya hapa duniani,nakuwa sitambui kama nipo kwenye mazingira ya ndoto kabisa
Mpaka inapelekea nachelewa sana kuamka hata kama niliwahi kulala

Naomba kufahamu hii inamaanisha ninia na utatuzi wake
maana too much is harmful.

Asanteni.
 
Aisee angalia usije ukawa upo shule halafu unaota upo kwenye maisha ya kawaida...

Labda umekuwa ukikumbukia enzi hizo au umepita katika mazingira ama umekutana na mtu aliyekukumbusha enzi unapiga kitabu
 
Usiombe ukaota unajisaidia please, hakika huu uzi utaukimbia kwa harufu for sure...🤣🤣
 
Habari,Shule ni sehemu ya kupata maarifa mapya ambayo ukuandaa kwa maisha ya sasa na ya badae. Umesema unaota unakaribia kufanya mitihani; Mosi,huenda kuna jambo au changamoto iko mbele yako na utatuzi wake unahitaji maarifa mapya hivyo usikurupuke kufanya maamuzi. Pili,kuota unasoma wakati ushavuka hiyo hatua maana yake level yako kufikiri iko chini kuliko inavyopaswa kuwa.hiyo huathiri hata maendeleo yako, yatakuwa nyuma kuliko yalivyotakiwa kuwa. Tatu,huenda ikamaanisha kunavitu kwenye ulimwengu wa roho haviko sawa,kuna mambo yamefanyika kukwamisha maendeleo yako. Kwa ufupi na hayo mkuu kwa upande wangu,samahani kwa mpangilio mbovu.
 
Asant kwa majibu wako kiongozi,yote uliyoyasema nikwel si ya kwanza (changamoto ni nyingi mno),
yapili
Ni nini nifanye ili niwe na uwezo mkubwa wa kufikir,

Na namba tatu
Ninini maoni yako ama nini kifanyike kujinasua kweny mitego yao
 
fikra mara nyingi huathiriwa na mtazamo tu juu ya mambo,niliposema huenda level ya kufikiri iko chini si kwamba huna akili,la hasha! Nina maana uone mambo kama Mungu anavyotaka uone.Ukishatambua wewe ni nani kwa Muumba utaanza kuona mambo kwa mitazamo tofauti na awali.kuna msemo kwamba change your mindset change your life.Unajua hata Kristo mission yake kubwa ni kutusanua kwamba haiko hivi,iko hivi,ka deal na ufahamu na fikra tu.
 
Huwa naota kucheza mpira tena nimefika level za juu kabisa.
Hizi hujirudia sana

Nlivokuwa under 23 age
Nlikiwasha sana.

Nikiwa zangu jogging madogo huniuliza "broo vipi unarudi dimban?"

Nimetoka nje ya mada[emoji23]
 
Hzo huwa ni ndoto zenye limitation in life pia la Kuna Jambo hujalitimiza kimekwama it's obvious utaota hizo ndoto, pray hard work hard ili kutimiza jambo lililogoma kwenye maisha ukishalitatua hizo ndoto zitakata automatic
 
Hakuna tajiri anaota yuko shule,hizo ni ndoto za watu waliofeli maisha maana yake kuna kitu hakiko sawa pambana ugraduate ni hayo tu
 
Ndoto yoyote ya kuota mambo ya nyuma au ambayo yalishapita hii ni ROHO YA KURUDISHWA NYUMA AU KUCHELEWESHWA kazi ya Roho hii ni kukuchelewesha kufikia malengo yako na 80% ya mambo yako yanakwama hasa jambo linapokaribia kupata mafanikio. Na kufanya mitihani ni kukumbana na majaribu au changamoto.kuna majaribu au mashambulizi unayoyapata. Kwa ujumla ukiota ndoto za nyumbani au kijijini n Dalili za kutumikishwa na mizimu ya eneo ulilotoka. Kumbuka ndoto ni Maisha. Unachokiota ni video clip ya Maisha yako halisi ambayo tayari yametokea au yatakayotokea. Kuwa makini sana usipuuzie ndoto unayoota
 
Hivi mtu afanyeje ka anaota ndoto za kijijini Mara kwa mara
 
Mi kuna wakati huwa naota niko kwenye paper( hesabu au Physics), halafu mara zote huwa sioni dalili ya kufaulu. Majibu nayajua ila huwa nashindwa kuendana na muda.
 
Lazima utafute MTU mwenye ufahamu kwanza akusaidie,maana ndoto hizo zinabebwa na Family spiritual. Ili kuzivunja ni lazima kwanza aelewe historia ya ukoo au familia ili angoe kabisa hiyo mizizi
 
Back
Top Bottom