Orodha ya Watanzania maarufu waliokufa bila kujenga nyumba

Orodha ya Watanzania maarufu waliokufa bila kujenga nyumba

Mtoe Ray Kigosi kwenye list.... Yeye hahusiki ana nafasi ya kujenga. Au anzisha Uzi mwingine wa watu maarufu wanaopata hela nzuri lakini hawajajenga
Mwenyewe yupo humu na amekuwa mkali kweli alipoliona jina lake,,unamiliki ndinga BWM Ya milioni 500 halafu unajibana na Mzee wako kwenye nyumba moja huo Ni ufala sisi sio Wahindi,,, Tunampa challenge ajenge aache udwanzi
 
1.Dkt. Omar Alli Juma
Huyu alikuwa VP kipindi cha BWM, baada ya kufariki akiwa madarakani, familia yake ilitakiwa kupisha nyumba rasmi ya VP iliyopo nyuma ya St Peters Oysterbay
ili Dkt. Shein VP mteuliwa aweze kuingia humo, wakawa hawana pa kuweka vyombo, hawana nyumba, ikabidi lori la serikali liwatoe kinguvu na kwenda kusitiriwa kwenye magofu ya Serikali


2. Gilman Rutihinda
Huyu alikuwa gavana wa BoT enzi za Mwinyi, tulimzika Buguruni Malapa maana kwao Ngara hakuwa na nyumba bali kijumba.


3. Moses Nnauye
Huyu alikufa mwaka 2000 kama sikosei, ilibidi msiba tuupeleke kwa mzee Makamba maana tulikosa sehemu ya kufunga turubai kwenye zile flats za NHC, utafunga turubai kwenye flats?


4.Profesa Shaba
Huyu sijui yupo hai au ,anasifika kuufanyia post mortam mwili wa hayati Sokoine, mpaka anastaafu na kumaliza kiinua mgongo hakuwahi kujenga hata choo.alipostaafu aliigomea serikali kuachia nyumba iliyokuwa mitaa ya Shaaban Robert karibu na Gymkhkana DSM
akiwatisha kuwa ataanika kilichomuua sokoine if at all they try to vacate him,wakampotezea


5. Steven Kanumba
Pamoja na kumiliki gari ya mamilioni kadhaa alikufa hajawahi kujenga hata kiosk

6. Ray Kigosi(yuko hai)
Bado anaishi kwa mama yake Sinza hajui hata mfuko wa cement inatoa tofari ngapi

Itaendelea

Hawakujua kupamba dinia
 
Kama kujenga ni uamuzi wa mtu kwa nini uwekwe kwenye orodha, yaani maamuzi yangu yanawahusu nini? Kwa nini uhangaike kujua kama sikujenga ama nilijenga?

Nadhani watu tuache maisha ya kiswahili ya kufuatiliana, ishi maisha yako, sikujenga ama nilijenga is non of your business.
Mkwafano hao viongozi, maisha yao yote ya uongozi walikuwa wanaishi kwenye nyumba za hadhi za serikali, wajenge ili iweje? Usikute waliacha vibunda vya kutosha kwa wanafamilia wao ili waamue wenyewe.
Mbaya ikukute umefariki ukiwa kwenye nyumba ya kupanga mtaani😀🙌
 
Back
Top Bottom