1.Dkt. Omar Alli Juma
Huyu alikuwa VP kipindi cha BWM, baada ya kufariki akiwa madarakani, familia yake ilitakiwa kupisha nyumba rasmi ya VP iliyopo nyuma ya St Peters Oysterbay
ili Dkt. Shein VP mteuliwa aweze kuingia humo, wakawa hawana pa kuweka vyombo, hawana nyumba, ikabidi lori la serikali liwatoe kinguvu na kwenda kusitiriwa kwenye magofu ya Serikali
2. Gilman Rutihinda
Huyu alikuwa gavana wa BoT enzi za Mwinyi, tulimzika Buguruni Malapa maana kwao Ngara hakuwa na nyumba bali kijumba.
3. Moses Nnauye
Huyu alikufa mwaka 2000 kama sikosei, ilibidi msiba tuupeleke kwa mzee Makamba maana tulikosa sehemu ya kufunga turubai kwenye zile flats za NHC, utafunga turubai kwenye flats?
4.Dkt. Shaba
Huyu sijui yupo hai au ,anasifika kuufanyia post mortam mwili wa hayati Sokoine, mpaka anastaafu na kumaliza kiinua mgongo hakuwahi kujenga hata choo.
5. Steven Kanumba
Pamoja na kumiliki gari ya mamilioni kadhaa alikufa hajawahi kujenga hata kiosk
6. Ray Kigosi(yuko hai)
Bado anaishi kwa mama yake Sinza hajui hata mfuko wa cement inatoa tofari ngapi
Itaendelea