Orodha ya Watanzania maarufu waliokufa bila kujenga nyumba

Orodha ya Watanzania maarufu waliokufa bila kujenga nyumba

1.Dkt. Omar Alli Juma
Huyu alikuwa VP kipindi cha BWM, baada ya kufariki akiwa madarakani, familia yake ilitakiwa kupisha nyumba rasmi ya VP iliyopo nyuma ya St Peters Oysterbay
ili Dkt. Shein VP mteuliwa aweze kuingia humo, wakawa hawana pa kuweka vyombo, hawana nyumba, ikabidi lori la serikali liwatoe kinguvu na kwenda kusitiriwa kwenye magofu ya Serikali


2. Gilman Rutihinda
Huyu alikuwa gavana wa BoT enzi za Mwinyi, tulimzika Buguruni Malapa maana kwao Ngara hakuwa na nyumba bali kijumba.


3. Moses Nnauye
Huyu alikufa mwaka 2000 kama sikosei, ilibidi msiba tuupeleke kwa mzee Makamba maana tulikosa sehemu ya kufunga turubai kwenye zile flats za NHC, utafunga turubai kwenye flats?


4.Profesa Shaba
Huyu sijui yupo hai au ,anasifika kuufanyia post mortam mwili wa hayati Sokoine, mpaka anastaafu na kumaliza kiinua mgongo hakuwahi kujenga hata choo.alipostaafu aliigomea serikali kuachia nyumba iliyokuwa mitaa ya Shaaban Robert karibu na Gymkhkana DSM
akiwatisha kuwa ataanika kilichomuua sokoine if at all they try to vacate him,wakampotezea


5. Steven Kanumba
Pamoja na kumiliki gari ya mamilioni kadhaa alikufa hajawahi kujenga hata kiosk

6. Ray Kigosi(yuko hai)
Bado anaishi kwa mama yake Sinza hajui hata mfuko wa cement inatoa tofari ngapi

7.Ruge Mutahaba
Huyu ni kama alijua atakata moto mapema akaona isiwe taabu

Itaendelea
Unauhakika kuwa Boss Ruge Hakujenga ama Unajilimbwasa tu...!? Acha kukariri licha ya kuwa na mijengo mikali Dar, Mwanza, Arusha na Bukoba Boss Ruge alikuwa anamiliki Mashamba makubwa saana kule Morogoro, Mbeya na Iringa..... Ruge akili kubwa kuliko unavyofikiria wewe
 
Unauhakika kuwa Boss Ruge Hakujenga ama Unajilimbwasa tu...!? Acha kukariri licha ya kuwa na mijengo mikali Dar, Mwanza, Arusha na Bukoba Boss Ruge alikuwa anamiliki Mashamba makubwa saana kule Morogoro, Mbeya na Iringa..... Ruge akili kubwa kuliko unavyofikiria wewe
Mkuu acha kupotosha toka hapo clouds fm
 
Huu Uzi wako ungenoga zaidi baada ya kumaliza Kuwananga na Kuwacheka Wenzako na Wewe hapo chini ungetuwekea idadi ya Nyumba zako unazozimiliki na alizojenga Baba yako Mzazi.

Otherwise unaonekana ni Mswahili, mpenda Majungu, una Chuki Binafsi, mwenye Wivu na Ujuha mwingi Kichwani mwako.
Aaah,kumbe hujajenga game change?ndo uanze kujenga sasa
 
Back
Top Bottom