Tetesi: P Diddy ahusishwa na kifo cha Notorious B.I.G

Ngoja kaka yenu niwasaidie sitaongea mengi labda mniulize niwasaidie

Aliyemuua B.I.G ni Amir Mohamad (Nationa of Islam)
Akishishirikiana na David Mack (LAPD)
NA Perez (LAPD)

David Mack na Perez walikua wanafanya kazi pia ya sidehustle Kwa V.I.P wa DeathRow

Ila walikua LAPD

Maswali yawe ya maana Angalau...

Usiniulize nani kawatuma...unganisha dots
 
Havoc Na Prodigy hawakua kweli na BadBoys ila iko hv, Puff Daddy alivyofukuzwa kazi nadhani Interscope alitaka awasaini kama wasanii wake wa kwanza...ila wakashindwana Maslahi...wakaenda label nyingine...!

Kama una swali niulize
 
Kwa hyo BB walikuwepo km wakina nani au ukaribu wao na Diddy ulikuwa ni wa nn au ulitokana na nn
Kwa mujibu wa article yako nanukuu "Diddy courted Mobb Deep". Tafsiri isiyo rasmi maana yake ni kwamba Diddy alikuwa anawafukuzia Mobb Deep ili awasaini. Inaonekana walishindwa kukubaliana. Mobb Deep wakaishia kusaini na Island kisha baadaye wakahamia Loud Records ya Steve Rifkind ambako ndiko walikopata mafanikio.
 
Havoc Na Prodigy hawakua kweli na BadBoys ila iko hv, Puff Daddy alivyofukuzwa kazi nadhani Interscope alitaka awasaini kama wasanii wake wa kwanza...ila wakashindwana Maslahi...wakaenda label nyingine...!

Kama una swali niulize
Uko sawa. Nikusahishe kidogo tu, Puffy alifukuzwa kazi kutoka Uptown Records na sio Interscope.
 
Hata hii theory yako ni nzuri
 
Kwenye mahijiano na vladtv keefe D anaulizwa vipi kuhusu ile kauli ya Tyson aliposema anahitaji dk 5 kwenye chumba na muuaji wa Pac Keffe akasema yeye anahitaji 2 tu huku akiwiggle kidole chake kama ishara ya kupull trigger na hiyo ni kama aliconfirm (indirectly kuwa yeye alihusika na tukio lile) huku akimalizia kusema "sasa hv kila mtu anajifanya muuaji, Tyson wewe ni boxer usijifanye kile ambacho wewe sio!"

Keefe D alikuwa ni member wa Southside Compton Crips ambaye alijipatia mkwnja mrefu kupitia michezo ya kusukuma kete. Huyu ndio mjomba wa Orlando 'Baby Lane' Anderson na siku ile walikuwepo Las Vegas ambapo Baby Lane alishambuliwa na Tupac na genge lake kwenye hotel ya MGM. Inasemekana siku chache zilizopita mmoja wa member wa death row alishambuliwa na Baby lane akanyang'anywa chain (zile cheni za death row) sasa siku hiyo Las vegas akaonekana ikabidi wahuni wa Deathrow wakachukue chao wakiongozwa na pac. Wakampiga Orlando wakamnyang'anya chain yao wakasepa. Orlando na yeye akaenda kusema kwa mjomba wake kuwa wahuni wa death row wamemjump. Ndio msako sasa ukaanza

Keefe D alikiri kuwa alikuwepo kwenye ile white Cadillac ambayo ndio iliyopaki pembeni ya bimmer ya Pac na Suge na inaaminika risasi zilitoka lwenye hiyo gari lkn alipoulizwa nani alishoot akasema hakuona maana yeye alikaa mbele siti ya pembeni ya dereva. Inasemekana Orlando ndio alipull trigger ijapokuwa wengine wanasema ni Keefe mwenyewe. Keefe pia anasema kulikuwa na bounty ya dollar 1m kutoka Badboys kwa atakayemmaliza pac.
 
Halafu inasemekana pia anapenda machoko zaidi na sio pisi Kali
 
Tafuta documentary inaitwa Murder Rap. Keefe D anakiri wazi kwamba nephew wake Orlando ndiye alikuwa shooter.
 
Hawa jamaa waliuliwa kwa mipango ya Suge Knight.Karma ilimlipa kwa kusababisha kifo akiwa ana driven akafungwa hadi Leo.
 
Big aligundua kwamba Diddy alikuwa anamnyonya sana, kwahiyo alikuwa amepanga akimaliza mkataba wao anaachana nae kitu ambacho Diddy hakupendezewa nacho na pengine kuamua kufanya kile anachohisi mama yake na Big.

Baada ya kifo cha Big Diddy umaarufu wake uliongezeka maradufu na pesa ikawa nyingi kutokana na kuuza nyimbo nyingi za Big ambazo bado zilikuwa studio kwake.

Pia akawahi fasta fasta kutoa ule wimbo wa 'I'll be missing you" akiwa amememshirikisha Faith Evans (ex wa Big) Nyimbo ile moja tu peke yake ilimpa pesa nyingi ambayo kama Big asingefariki basi angekaa zaidi ya miaka 5 bila kuishika.

So kifo cha Big kimemnufaisha zaidi Puff kuliko kilivyoinufaisha familia yake Big.
 
Pac hakupenda ujinga na unafiki ndo maana hata Dre aliposhindwa kufika mahakamani katika case ya Snoop Dog kama shahidi kwa upande wa utetezi Pac alimchana na kupelekea Dre kuachana na label deathrow record.

Katika baadhi ya nyimbo Pac alim diss Dre, ila Dree aliogopa kujibu

🎶What's up in 96? Fine tricks in drag, f.u..ck Dre, tell that b..i..tch he can kiss my a.ss🎶 2Pac - Let's be friends
 
Tafuta documentary inaitwa Murder Rap. Keefe D anakiri wazi kwamba nephew wake Orlando ndiye alikuwa shooter.
Hii ya kukiri au kusema kwamba fulan ndio alikuwa shooter baada ya mtu huyo kufariki wala haileti maana.

Ukishafariki lolote unaweza kupakaziwa iwe kwa kusifiwa au kupondwa.

Kwahiyo asimuamini kwa asilimia 100 alichokiongea.
 
Hawa jamaa waliuliwa kwa mipango ya Suge Knight.Karma ilimlipa kwa kusababisha kifo akiwa ana driven akafungwa hadi Leo.
2pac alishambuliwa huku akiwa na Suge ndani ya gari tena wote wakiwa viti vya mbele.

Sidhani kama Suge angeweza kuwa mjinga kuweka maisha yake hatarini kiasi hicho na ukizingatia mshambuliaji alikuwa anaagiza tu risasi kama mvua bila kujali ni nani na nani atakaepatwa na zile risasi ndani ya gari.

Kumbuka risasi haina macho kwahiyo pengine ingeweza kumpita Pac ikaenda kumpitua Suge kichwani. Sasa hapo angekuwa amefanya mission ya aina gani ambayo ingemuuwa mwenyewe?

Tutumie akili kutafakari kabla ya kuandika jambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…